Diana Chilolo awabwaga wapinzani wake nafasi ya Mwenyekiti CCM UWT - Singida | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diana Chilolo awabwaga wapinzani wake nafasi ya Mwenyekiti CCM UWT - Singida

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 8, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=3]MH. DIANA CHILOLO AWABWAGA WAPINZANI WAKE NAFASI YA MWENYEKITI WA UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA UWT (CCM) MKOA WA SINGIDA.[/h][h=3][/h]  [​IMG]
  Mbunge wa viti maalum (CCM) mkoa wa Singida Diana Mkumbo Chilolo akiwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT mkoa wa Singida kwa kumchagua tena kuwa mwenyekiti wao kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.Chilolo alipata kura 431 dhidi ya kura 451 zlizopigwa.
  [​IMG]
  Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa UWT CCM mkoa wa Singida akitoa maelekezo kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi huo.
  [​IMG]
  Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata (waliokaa mbele anayesikiliza simu) na baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UWT mkoa wa Singida.Kulia kwake ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Diana Chilolo.
  [​IMG]
  Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UWT mkoa wa Singida.Uchaguzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).

  Diana Mkumbo Chilolo ametetea kwa kishindo nafasi yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT (CCM) mkoa wa Singida baada ya kupata kura 431 dhidi ya 451 zilizopigwa.


  Kwa ushindi huo, Chilolo ambaye pia ni mbunge wa viti maalum mkoani Singida amewaacha kwa mbali wapinzani wake Pendo Kone aliyepata kura 11 na mwalimu Sundi Samike aliyeambulia kura nane.

  Msimamizi wa mkutano huo mkuu wa uchaguzi Dkt. Parseko Kone amemtangaza mkuu wa wilaya ya Manyoni Fatuma Towfiq kuwa amaechaguliwa katika nafasi ya mjumbe wa baraza kuu taifa UWT.


  Amesema mfanyakazi wa TANROADS mkaoni Singida Sara Mkumbo, amememgaragara vibaya mpinzani wake Mwajuma Shaa kwa kura 247 dhidi ya kura 153.


  Dkt. Kone ambaye ni mkuu wa mkoa wa Singida amewataja washindi wa baraza la UWT kutoka wilaya ya Singida vijijini kuwa ni Halima Kundya na Debora Andrew.


  Amesema kutoka wilaya ya Ikungi ni Mariamu Limu na Tatu Dahani, wilaya ya Iramb ni Monica Samwel na Elimaba Lula, wilaya ya Mkalama ni Mariamu Kahola na Helena Kitila, Manispaa Singida ni Aisha Matembe na Sara Mkumbo wakati wilaya ya Manyoni ni Magreth Mlewa na Rehema Chizumwa.


  Aidha Dkt. Kone amesema Hadija Nyuha ameshinda nafasi ya uwakilishi wa jumuiya ya wazazi kwenye mkutano mkuu wa UWT, wakati Mwakilishi wa UVCCM ni Janet Mughwai.


  Jane Kishari amechaguliwa kuwa mjumbe kwenye mkutano mkuu wa CCM mkoa.
   
 2. P

  Paul S.S Verified User

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hongera yake lakini hii habari ya wakuu wa mikoa kuwa makada kwakweli haijakaa sawa kabisa
   
 3. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwenye kundi la vipofu alwayz mwenye chongo ana afadhali. Magamba ni magamba ata akishinda still ni gamba tuu.
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  Umeona eeh?
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa mkoa anasimamia uchaguzi wa ccm katika kudhihirisha kauli ya waziri mkuu Pinda kwamba ma RC na ma DC wanafanya kazi za chama.
  Tunazidi kupata sababu ya kutokuwa na hivi vyeo vya DC na RC kwakuwa hawana kazi za kufanya zaidi ya propaganda za ccm.
   
 6. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Jamani ina maana huyu mama Martha Mlata hakugombea maana hakuna kitu anachogombea ndani ya CCM asipate. Kweli mama Martha Mlata ana nyota ndani ya CCM sema atakua ameamua kupumzika mambo ya chama maana hata kama ukitokea uchaguzi wa kufuga ngombe ndani ya CCM huyu mama atagombea na atashinda tu
   
 7. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Amehonga sana huyu mama.katoa kanga na ef 30 kwa kila mjumbe.huo ni ushindi wa kununua
   
 8. m

  mwitu JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 857
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  mkuu wa mkoa kavaa nguo za ccm hii hatari
   
 9. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [/COLOR] [/QUOTE]

  Kwanini asishinde wakati yeye ni mtoaji mzuri wa ile rushwa maarufu.....? Huwa hana hiyana na mtu! Hongera sana mama Chilolo!
   
 10. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kwanini asishinde wakati yeye ni mtoaji mzuri wa ile rushwa maarufu.....? Huwa hana hiyana na mtu! Hongera sana mama Chilolo![/QUOTE]

  Asante kwa kunijuza maana nilikua nafikiri eti ana nyota ndani ya chama kumbe anasafiria nyota za wengine.Siku wapokeaji wakikichoka du mtaji kwisha
   
Loading...