Diana Bundala aka Mfalme Zumaridi, afikishwa Mahakamani akikabiliwa na kesi tatu ikiwemo usafirishaji haramu wa binadamu

Ushauri kwa serikali usajili makanisa yote upitiwe upya, pili wachungaji wote wawe na digrii ya theology ,kila kanisa la kilokole lifunge sound proof , muona Kama utitiri wa makanisa uchwara ya kina Diana Bundala na Zumaridi yataonekana tena , Rwanda wamefanya hivi baada ya kuwakuta ya kuwakuta , sisi serikali yetu inasubiri yatokee ndio ipate akili .
 
Ushauri kwa serikali usajili makanisa yote upitiwe upya, pili wachungaji wote wawe na digrii ya theology ,kila kanisa la kilokole lifunge sound proof , muona Kama utitiri wa makanisa uchwara ya kina Diana Bundala na Zumaridi yataonekana tena , Rwanda wamefanya hivi baada ya kuwakuta ya kuwakuta , sisi serikali yetu inasubiri yatokee ndio ipate akili .
Serikali ya Tanzania haina dini haisajili dini
Kuhusu kuwa na digrii za theology Rwanda mapadri na maaskofu walikuwa nazo wote na ndio walisababisha na kushiriki maji ya kimbari Rwanda hadi papa akaomba msamaha

Hawakusabisha viongozi wasio na digrii za theology!!!

Uhalifu wa mtu binafsi kuna sheria zake shehe akibaka mtu hufungi msikiti unamfunga yeye
 
Hivi wewe umeishia darasa la ngapi kwanza ? Usisumbue watu vitu simple tu huelewi vimeanishwa hapo juu ,kila kitu kina sheria na taratibu zake , makanisa , misikiti Yana sheria na taratibu zake . Huelewi nini sasa ? Huo ulokole wenu muwe mnasoma muelimike , kifupi kanisa lazima lisajiliwe , pili liwe na kibali cha kuendesha ibada , kama linajengwa liwe na kibali cha ujenzi kutoka manispaa au mamlaka husika , hata kibali ukipata kina masharti yake jinsi ya kuendesha ibada ikiwemo sheria no 147 ya mazingira inayataka sauti za muziki na mahubiri yasizidi desibeli 40 , sasa kanisa lako halina hata kimoja ,kuna fitina gani hapo ? Hayo ni kwa kifupi , muhurumieni Yesu Kristu kwa kutapeli waumini kwa kutumia jina lake tafadhali .
Tunachopinga ni uongo wako uliokubuhu kuwataja hao wa Tabora kuwa wafiasi wa Zumaridi umebweka sana humu kuhusu hilo kanisa la Bethel muda mrefu kwa michuki yako binafsi ya kishetani unaona wanaendelea tu kuwepo

Umesingizia hadi viongozi wa Serikali kuwapaka motope na kuwachafua kuhusu hilo

Hangaika na maisha yako yaliyochoka achana na Bethel
 
Hili la huyu mama mungu ni kiki za kiccm kunapotokea jambo kubwa iliwatu wagawanyike propoganda nchi hii zimezidi usikute kitengo ndicho kilicho fadhili nguvu za huyu mungu mke kama lile gazeti la yule mdaiwa sugu wa Membe na shangazi!
Kwa Tanzania chochote chawezekana
 
Ushauri kwa serikali usajili makanisa yote upitiwe upya, pili wachungaji wote wawe na digrii ya theology ,kila kanisa la kilokole lifunge sound proof , muona Kama utitiri wa makanisa uchwara ya kina Diana Bundala na Zumaridi yataonekana tena , Rwanda wamefanya hivi baada ya kuwakuta ya kuwakuta , sisi serikali yetu inasubiri yatokee ndio ipate akili .
Acha roho mbaya wewe..huduma ya injili usiiwekee mipaka hivyo..mana injili ni popote penye watu unataka kuleta habari za serikali ya ccm kuwa hakuna mikutano ya vyama vya siasa huku wao wakifanya mikutano ya hadhara..acha injili ihubiriwe watu waokolewe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu wachungaji wengi , manabii , mitume ni matapeli wa kutupa wanatumia ulaghai , utapeli , ushirikina kuhadaa mbumbumbu ndio hakuna kiongozi wa dini hata mmoja aliyetoa tamko kulaani yanayofanywa empty set Zumaridi na wengine wengi .

Wewe ndio mjinga, unamwitaje mtu anayetapeli na kutumia uchawi mchungaji?. Huyo Ni mchawi sio mchungaji. Nyie ndio mnapenda kuchafua ukristo kisa matapeli wachache walioingia kanisani ambao wenyewe sio wakristo. Tofautisha ukristo na cult. Usilazimishe cult na ukristo ukawa pamoja.
 
Acha kukariri maisha wewe.

#MaendeleoHayanaChama

Mwanzo wa kuwa brainwashed ndio huu kukataa ukweli. Yani Mfalme Ni kwa jinsia ya kiume lakini tunalazimishwa ni jinsia ya kike. Kesho tutaambiwa kuna wanawake wake wa kiume.
 
Ndugu yeye na wachungaji wengi ,manabii , mitume wengi ni wajasilia dini a .k.a wajasilia kanisa wajinga ndio waliwao .

Wewe nimekufatilia nimegundua una chuki na ukristo sio kidogo. Kosa amefanya Zumaridi lakini umekazania wachungaji wengi nk. Hai wachungaji wengi unawajua?. Yani matapeli wachache ambao hata sio wachungaji, umekazania tu. Zumaridi anajiita mungu na Wala sio mchungaji. Taja mchungaji aliyekutapeli au kamshtaki polisi. Maana utapeli Ni kosa la jinai.
 
Uongozi wa ukraine nao ulikuwa hivi hivi. Nchi yetu viongozi wake wamekosa vitu vya msingi vya kufanya na ndio maana kutwa wanashinda kuchunguza mambo binafsi ya raia wake. Majukumu pekee wanayoweza kuyatimiza ni kuonea na kutesa raia wa chini wasio na meno. Mwingine anazuia michezo mtaani mwingine anatuma polisi akakamate watu kanisani. Wamewamaliza chadema ila ile toho tesi bado inaendelea kuishi. Hii nchi inatia kinyaa sana na bora walio Ukraine wanaunafuu sana. Raia tumewakosea nn polisi?
 
Hivi mtume Issa Bin Mariam, Kristo hakujua kama jamaa kamsariti na baadaye wakaja kumkamata ili asepe?.

👉🏾 Comment nyingine huwa napima akili naona hapa kutakuwa na watoto wa Sunday School.

Wewe ndio mtoto wa Sunday school. Unataka kumlinganisha Yesu Kristo na Mfalme Zumaridi?. Kasome Biblia vizuri uelewe hasa kitabu Cha Isaya. Kuzaliwa kwa Yesu Kristo na kifo chake kulitabiriwa miaka mingi nyuma.
 
Serikali ya Tanzania haina dini haisajili dini
Kuhusu kuwa na digrii za theology Rwanda mapadri na maaskofu walikuwa nazo wote na ndio walisababisha na kushiriki maji ya kimbari Rwanda hadi papa akaomba msamaha

Hawakusabisha viongozi wasio na digrii za theology!!!

Uhalifu wa mtu binafsi kuna sheria zake shehe akibaka mtu hufungi msikiti unamfunga yeye
Hapa tunataka kuzuia karaha na usimbufu usio wa lazima kwenye makazi ya watu.
 
Mchungaji Diana Bundala maarufu 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 92 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayokabili.

Msafara wa magari matatu aina ya difenda zilizolindwa na askari waliojihami kwa silaha umewasili katika mahakama hiyo saa 9:00 mchana kisha watuhumiwa hao kuamuriwa kuingia ndani ya mahakama hiyo.

Akishuka katika gari ya polisi iliyokuwa imembeba, Zumaridi amesikika akisema "Mimi ndiyo Mfalme’ huku akionyesha ishara ya kuomba.

Miongoni mwa waliofanikishwa mahakamani hapo wakiwa na mhubiri huyo ni vijana wanaokadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi 45 na wazee wa jinsia zote wanaodhaniwa kuwa na umri kuanzia miaka 45 hadi 65.


Source: Mwananchi

View attachment 2137530

=====

Mfalme’ Zumaridi, waumini wake kizimbani, wakataa dhamana

Mwanza. Diana Bundala maarufu kama ‘mfalme Zumaridi na wenzake 92 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mwanza wakikabiliwa na kesi tatu ikiwemo usafirishaji haramu wa binada, shambulio la kudhuru mwili na kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu.

Mwendesha mashtaka wa serikali amesema katika kesi namba 10/2022 inayomkabili Zumaridi peke yake akidaiwa kusafirisha binadamu wakiwemo watoto wenye umri chini ya miaka 18 kinyume cha kifungu namba 4(1) (A) na 6(2) (A) cha sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu namba 6 ya mwaka 2008.

Katika kesi namba 11/2022, Luvinga amesema Zumaridi na nwenzake wanane wanadaiwa kufanya shambulio la kudhuru mwili askari wa Jeshi la Polisi waliofika nyumbani kwake kutekeleza wajibu wao kinyume cha kifungu namba 241 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Washtakiwa hao pia wanadaiwa kuwazuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao kinyume cha kifungu namba 114(A) kifungu kidogo B cha Kanuni ya Adhabu.

Katika kesi namba 12/2022, mwendesha mashataka huyo aliiambia Mahakama mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Monica Ndyekubora kuwa Zumaridi na wenzake 92 wanadaiwa kufanya kusanyiko lisilo halali kinyume cha kifungu cha 74(1) na 75 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.

Washatkiwa walikana mashtaka yao katika shauri namba 11 na 12 huku upande wa Jamhuri ukiieleza Mahakama kuwa upeleleza kuhusu mashauri hayo mawili umekamilika na kuomba kupagiwa siku ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Kuhusu shauri namba 10 la usafirishaji haramu wa binadamu linalomkabili Zumaridi, mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Licha ya mashtaka namba 11 na 12 kuwa na dhamana huku baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamejitokeza kuwadhamini, washtaki wote wanaowakilishwa na Wakili Erick Mutta walikataa dhamana wakisisitiza kuwa wako tayari kwenda mahabusu kuungana na kiongozi wao anayekabiliwa na kesi ya usafirishaji haramu wa binadamu isiyo na dhamana.

Kutokana na uamuzi huo, Hakimu Ndyekubora ameamuru washtakiwa wote kupelekwa mahabusu hadi Machi 17, shauri hilo litakapotakwa kwa ajili ya washatakiwa kusomewa maelezo ya awali katika shauri namba 11 na 12.

Pia, soma;

1). Mwanza: Polisi yamkamata Mfalme Zumaridi. Anatuhumiwa kwa kosa la usafirishaji haramu wa watu wapatao 149

2). Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

3). Mfalme Zumaridi ni nani haswa?
View attachment 2137726
View attachment 2137728View attachment 2137729
Mfalme Zumaridi (Mwenye sweta la bluu)na wenzake 92 wakitoka kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Mh huyo binti wa nyuma ya mfalme naona kaumbika haswaa kishunduu hataree
 
Hapa tunataka kuzuia karaha na usimbufu usio wa lazima kwenye makazi ya watu.
Anzac kampuni na bar kwanza ndizo zenye kelele nyingi zikifuatiwa na misikiti usiku unaamshwa mtu usingizini na achana ya msikiti
 
Back
Top Bottom