Diamond Platnumz na Wasafi hununua viewers? Wasafi wakubali kuwa wasanii wananua viewers, wahaha kuona wanunuzi wapya

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,206
42,067
Wasafi Fm kupitia ukurasa wao wa instagram waliweka maneno ya msanii kutoka Nigeria ambaye alikuwa anasema kuwa wasanii waache kununua viewers wa youtube na akasisitiza kuwa anawambia wasanii wengine sio wanigeria maana wa uko Nigeria awawezi kununua viewers wa Youtube.

Kwenye hili sikubaliani nae msanii husika kwani kama kweli kuna utapeli wa kununua watazamaji youtube basi ni ngumu kuamini wasanii wa Nigeria washindwe kununua viewers kwa walivyo hodari kwa utapeli.

Baada ya msanii huyo kuweka hiyo post wengi wakiwemo wasafi media waliweka hiyo post kwenye mitandao yao kwani walikuwa wanaamini anaambiwa Harmonize lakini wakasahau wao walisha ambiwa wananua viewers wakasema haiwezekani kununua viewers youtube. Nini kimegeuza msimamo wao?

Ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi wa nne Director Hansacana alisema wazi kuwa wasanii wananunua viewers na akaoneshwa jinsi inavyo wezekana kununua viewers.

lakini Director huyu alishambuliwa sana wakiwemo wafuasi wa Diamond ambao walisema haiwezekani na wakajitokeza wataalam wakasema haiwezekani kununua viwers na Maneneja wake Diamond na Wasafi walisema wazi kuwa haiwekani kununua viewers na kama inawezekana basi kila mtu anunue na waliendelea mbele na kusema msanii Diamond na wasafi wanaonewea wivu

Baada ya majuma Machache tena Mkurugenzi wa EFM bwana Majizo akihojiwa na Gerald Hando alisema wazi kuwa kuwa msanii kuwa na viewers wengi sio kigezo cha kuwa na wimbo mzuri au kuwa msanii mkubwa kwani kwenye viewers wa youtube kuna siasa nyingi

Baada ya hii kauli Diamond na Mameneja wake walimshambulia sana Majizo wakisema anawaonea wivu wasanii wa wasafi na Diamond kupitia ukurasa wake alionesha na kuandika umuhimu wa viewers na umuhimu wa kuwa na viewers wengi hata hivyo wafuasi wa Diamond na wasafi waliendelea kuwashambulia wote waliosema kuwa wasanii wananunua viewers wakisema ni watu wanao muonea wivu msanii Diamond na hawamtakii mema.

Watu wameshangazwa wasafi kukubaliana hoja ya kununua viewers wakati walikuwa wanapinga vikali kabisa wakisema haiwezekani kabisa sasa tunaanza kujiuliza kwanini wamekubali leo?

Kwa sababu sio Diamond anaye ongoza kuwa na viwers?

Kwa sababu sio wasanii wa wasafi wanao ongoza kwa Viewers uko Youtube?

Kwa sababu Wasafi hawapendi kuzidiwa na wana muhaho?

Kinyago wanacho pambana nacho sasa wasafi walikichonga wenyewe kwa hiyo kama kinyago kina nunua viewers basi kimepata ujuzi wa kununua viewers uko uko wasafi si kwingineko.

Kwa hiyo kwa Muktadha huo Wasafi wanakubaliana nasi kuwa viewers zinaweza kununuliwa? nashutuma juu ya wasanii wao kununua viewers zilikuwa za haki kabisa?

Je, ni kweli Diamond ananunua viewers?
 
Sasa kwa akili yako wewe, upi ni umuhimu wa views katika video ya msanii?
Tuanzie hapo kwanza
 
Kununua views unanunuaje,hebu tupe mchakato jinsi ya kununua?

Hivi ununue YouTube wanakutizama tu? Yaani kitendo cha kuwa na uwezo wa kununua views ni tusi kubwa sana kwa YouTube. Endeleeni na story zenu za vijiweni.
 
Inawezekana kununua views ila ukinunua views likes haziwezi kupanda lazima kuwe na uwiano mtu akipewa hizo lawama tazama lazima likes zimfunge kwamba ziko vilevile wakati views wamepanda.
 
ah, mi mambo ya viewers haya naona yananichanganya mpaka nafikiria kuacha tu sasa kuzungumzia habari zenyewe, sielewi tu. sijui ni slow learner mimi?!!!!

zuchu yuko no.1 katika kutrend, views zake ni 2m

diamond yuko no.2 na viws zake ni 3m (km sikosei)

alikiba yuko no.3, viws zake ni 2.6m na

harmonize yuko no.6 kiwa na viws 4.5m. tukumbuke huyu views zilikuwa 1.5 tu hapa juzi........sasa hii kutrend sijui ndo ipoje ipoje? ngoja ninyamaze tu
 
Inawezekana kununua views ila ukinunua views likes haziwezi kupanda lazima kuwe na uwiano mtu akipewa hizo lawama tazama lazima likes zimfunge kwamba ziko vilevile wakati views wamepanda.
Leo nimeangalia clip za Lionel Mess anavyotoaga pass kama 6 hivi lakini akuna ata moja niliuolike
 
Kununua views unanunuaje,hebu tupe mchakato jinsi ya kununua?

hivi ununue YouTube wanakutizama tu ? Yaani kitendo cha kuwa na uwezo wa kununua views ni tusi kubwa sana kwa YouTube. Endeleeni na story zenu za vijiweni.
hahahahaha
 
ah, mi mambo ya viewers haya naona yananichanganya mpaka nafikiria kuacha tu sasa kuzungumzia habari zenyewe, sielewi tu. sijui ni slow learner mimi?!!!!

zuchu yuko no.1 katika kutrend, views zake ni 2m

diamond yuko no.2 na viws zake ni 3m (km sikosei)

alikiba yuko no.3, viws zake ni 2.6m na

harmonize yuko no.6 kiwa na viws 4.5m. tukumbuke huyu views zilikuwa 1.5 tu hapa juzi........sasa hii kutrend sijui ndo ipoje ipoje? ngoja ninyamaze tu
Kama kweli viewers wananuliwa sasa watashindwa vipi likes? hahahaha
 
Ukiwa na akili huitaji kubishana na tabia hii. Unapohitaji kubaini msanii alinunua viewers mwanzoni jaribu kufuatilia consistency ya views bada ya mwezi na kuendelea. Mfano

1. Angalia wimbo wa Harmonize ft Awilo. Wimbo huu ndio unaosemwa umevunja records za Diamond kwa kutazamwa ndani ya siku 3 za mwanzo, pamoja hiyo kasi huu mwezi wa pili Bado una views 12m. Zuchu 4 months sukari 43m, Diamond ft Koffi 75m in 7 months. Ukiangalia kasi ya utazamaji ya mwanzoni ya ngugu Harmo haireflect uhalisia. Same na anachokifanya sasa katika Sandakalawe.

2. Angela, Nobody siku 4 za kwanza 2m views na ikasemwa Anjela kamshinda Rayvan. Baada ya mwezi Anjela 3.7m, Rayvan 4.7m
 
Back
Top Bottom