Diamond platnumz na Kasimu mganga nani mkali wa nyimbo za mapenzi?

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,456
25,375
Kwa wale wapenzi wa nyimbo za mapenzi watakubaliana na mimi kwa 100% kwamba kwa hapa Tanzania ukitaka kusikiliza nyimbo kali za mapenzi zenye kubembeleza,kuliwaza,kufariji na kusuuza moyo basi sikiliza nyimbo za hawa magwiji wawili ambao ni Kassimu Hemed au Kasimu Mganga na Naseeb Abdul au Diamond Platnumz .

Kila mmoja kwa wakati wake amekuwa akitamba kwamba yeye ndio fundi au tajiri wa nyimbo za mahaba
Kassimu kwa upande wake amesumbua na ngoma kali kama vile Awena ,Usiende kwa Mganga ,Subira aliyomshirikisha king of the best melody hapa namzungumzia Christian Bella nk

Kassimu kwa sasa anatamba na ngoma ya Somo aliyowashirikisha Kilimanjaro band (wananjenje ) waliotamba na ngoma yao ya kinyau nyau
Naseeb kwa upande wake ametamba na ngoma kama vile nimpende nani, tatizo kwetu mbagala , lala salama,moyo wangu nk

Kwa sasa Naseeb anatamba na ngoma yake ya marry you aliomshirikisha mwanamuziki Ne-Yo

Screenshot_2017-03-04-18-55-57_1.jpg

Screenshot_2017-03-04-18-57-15_1.jpg

Haya sasa wakuu kazi kwenu nani fundi hapo kwenye upande wa nyimbo za mapenzii tuuu basiiii ?
 
Acha kumlinganisha baba Tifa na mambo ya ki...nga
 
Mtakufa kwa kiki vipi unataka ku release song nn bila mond hamuwiki mjini umezungukaa kumbe lengo lako ni kiki ili kijimbo chako kisikike mondiiiii vijana hawalali wanakuwaza chibuuu mjini bila mondi kiki hakuna
 
Mkuu povu la nini

Wewe sema tu kama dai ni mkali au huyo kassimu basi na si hivyo unavyotoa povu
 
Wote nyimbo zao ziko poa sana ila nahisi diamond amezidi kwasababu moja tu, yeye nyimbo zake anatumia maneno rahisi sana ndio maana nyimbo zake zikubalika sana na rika zote kuanzia watoto!
Mfano salome,lala salama,nalia na mengi,moyo wangu, mawazo, ukimwona etc

Hata hutumii nguvu kuzisikiliza na kuzielewa
 
Hapana mkuu

Diamond hutumia misamiati mingi sana kwenye nyimbo zake kuliko kasimu

Mfano kwenye wimbo wa salome

"eeh mapenzi yananipa shida ,shida mamaaa

ni gonjwa lisilokuwa na tiba ,tiba bwanaa

usije baby ukanicharanga ,ukauchambua moyo kama karanga

mie baby kwenye msambwanda ,huwa siendagi nge nge nge ni nga nga nga"
 
Hata kama unampenda Diamond lakini hupaswi kumdharau Kassim, embu pitieni hizi ngoma muone;
1.Awena
2.Haiwezekani
3.Usiende kwa mganga
4.Subira ft.Bella
5.Tajiri wa mahaba
5.Ndoa ndoano ft.Blue
6.Manuari
7.Sijali
8.Majeraha ft.Akili the brain
9.Somo ft.Kilimanjaro Band
 
Yaah Kasimu yupo vizuri sana kwenye sekta hiyo sema members wengi wameona kama nimemshusha diamond kumlinganisha naye
 
Back
Top Bottom