Diamond Platnumz kuzungumza na vyombo vya habari kesho saa 5 asubuhi

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,220
12,933
Jioni hii Diamond (Chibu) ameripoti kuwa kesho atazungumza na vyombo vya habari nchini.

Je, Chibu anaenda kujibu mawe anayorushiwa juu Million 500 ya Konde boy?

Usikose kesho saa 5 asubuhi kupitia Wasafi TV na Wasafi FM (88.9).

 
Hivi kweli mtu mzima mwenye akili zake unaweza kuamini Konde Boy anaweza kumtetelesha Chibu..!!!!

Kabisa, tuone kesho kama hataongea mambo ya harmonize, nakumbuka mwanzoni kabisa niliandika humu harmonize kapeleka milioni 600 WCB tena cash ikiwa kwenye buti ya BMW X6 Diamond akakataa kupokea watu wakanishambulia sana...mwezi mmoja baadae harmonize kaja kuthibitisha milioni mia tano na ushee baada ya majadiliano
 
Hyatt Regency had I ile saa1 usiku ilikuwa imejaa hakuna sehemu hata ya kukanyaga

na mkutano wenyewe ni dk 30 tu.

Hadi BBC,CNN n.k wamewekapo kambi hapo

Ally Kiba atasubiri sana!
 
Alaah, ngoja uone watu wenye talents za figisu wengi mlikua mnasubiria downfall ya konde boy ila ndio hivyo mmeshafeli...diamond anatafuta relevance tuu kwa sasa
Kuna method ya kuua ushindani kwenye soko haswa kama mnaona kuna mshindani anayeteteresha mauzo yenu, Hapa unaanzisha kampuni jingine halafu unatengeneza hali ya ushindani FAKE kati ya hizo kampuni na mwisho wa siku watu watamsahau mshindani kama hatosoma alama za nyakati mapema..
 
Alaah, ngoja uone watu wenye talents za figisu wengi mlikua mnasubiria downfall ya konde boy ila ndio hivyo mmeshafeli...diamond anatafuta relevance tuu kwa sasa

Sio mmoja ya watu waliowahi kusubiri downfall ya yeyote hata kama ni adui yangu sembuse ya hao ambao sijawahi kufahamiana nao in person,Never!

Je wajua konde amechelewa sana kupata mashabiki wake mwenyewe? mpaka kipindi fulani tulipenyeza maoni usafini kuwa ufanyike mkakati maalumu wa ku rectruit mashabiki wa konde na Rayvanny, hii ilikuwa before mboso, Lavalava na nani sijui yule hawaja sign wasafi?

Rayvanny na konde ni watu waliobebwa na mashabiki wa DP kwa muda sana mpaka mzigo wa kutoa support ukawaelemea mashabiki, hivyo usifikiri Konde au yeyote ana Jeshi kubwa kiasi aweze kufanikisha fitna dhidi ya wasafi. Jeshi lake ni dogo sana, anatakiwa akaze sana kusimamisha jeshi lake kama lile lililo nyumba ya DP, uzuri amepata bahati ya kukokota pia haters wa DP the same kilichokuwa kinatokea kwa kiba.

DP sio mwepesi anaweza kuacha kuimba leo hii lakini ataendelea kuwa na influence kwa muda mrefu sana, kum- underrate ni kujipa moyo tu.
 
Back
Top Bottom