Diamond Platnumz inabidi apewe uwaziri au ukuu wa mkoa, amelifanyia makubwa taifa hili

Jay z kafanya mangapi kule!!! Umeona kuna fala yeyote kaomba jay z apewe uongozi!!!! Aisee hii ngozi nyeusi tunaiaibisha sisi wenyewe2 mbona tuna uwezo wa kufikiri ila2 ndo kama hivi
Viongozi wa kule wanaleta maendeleo kwa wakati ila kwa hapa TZ bora ya Mondi kuliko viongozi wenye dhamana.
 
Hivi Unadhani cheo ni Zawadi tena cheo cha kuongoza wananchi !!!.

Kweli akili zinatofautiana sana, Tungekuwa na mwanamziki kama Michael Jackson si ungesema apewe mkoa wake aishi mwenyewe, dunia ina mambo ya burudani, michezo siasa na mengine kila sehemu inahitaji watu wake Maalumu au husika.
 
Huu unazi wako jomba sio wa nchi hii.

Ni kweli D mpaka hapo alipofikia kafanya makubwa kwa nafasi yake pengine kuliko hata wanamuziki wengine wote waliomtangulia na waliopo, lakini kwa hilo unalopendekeza ni BIG NO.

Tukifanya hivyo basi siku akitokea mwingine wa kufanya makubwa zaidi yake na akadai kupewa cheo kwa misingi hiyo atakuwa kwenye haki ya kupewa na akitokea mwingine tena itakuwa hivyo hivyo.

Hatuna haja ya kufanya hilo unalolitaka, badala yake hili kuenzi na kuutukuza mazuri yake tutakachokifanya ni kumuweka kwenye HALL OF FAME itakayokuwa na iconic figures wa muda wote.
 
Au tunaweza kuteua kiwanja chochote cha Starehe kikubwa hapa nchini na kukipachika jina lake rasmi.

Kama walivyofanya wareno kwa kuibadilidha MEDEIRA INTERNATIONAL AIRPORT na kuiiita CRISTIANO AIRPORT.
 
Ndo shida watu kutuandikia uzi na miswaki mdomoni. Alichotete nini?
Hiyo ni kazi kama kazi zingeni anachokifanya ni maisha yake ni sawaa campuni kuhitaji kukua ili kulinda brand yake no more
 
Sasa mkuu lengo la kupewa uwaziri au ukuu wa mkoa liwe ni shukrani kwa misaada yake au kumpa nafasi ya kusaidia zaidi?
 
Back
Top Bottom