Diamond Platnumz inabidi apewe uwaziri au ukuu wa mkoa, amelifanyia makubwa taifa hili

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,415
21,098
Mnyonge mnyongeni jamani ila haki yake mpeni.

Huyu bwana mdogo Diamond Platunumz amefanya mambo mengi makubwa makubwa sana hapa nchini kuliko hata viongozi wemye dhamana hiyo tena amemzidi hata rais magufuli kwa kujitolea misaada mbalimbali kwa wananchi wenye uhitaji.

Kwa haraka haraka ukipiga mahesabu misaada aliyoitoa kwa miaka kadhaa inafikia Bilioni 20+.

Asilimia kubwa ya mapato yake hutumia kusaidia vijana na wazee wasiojiweza.

Wasanii chipukizi wengi wamepewa sapoti ya kimawazo na kifedha na diamond platnumz ingawaje wakishatoka wanasahau fadhila .

Screenshot_2017-09-22-14-43-07.jpg

Hapa Diamond akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ndugu Daudi Albert Bashite msaada wa madawati 600.

Screenshot_2017-09-22-14-52-21.jpg

Hapa Diamond akitoa msaada wa milioni 20 GSM kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji upasuaji wa vichwa.

Screenshot_2017-09-22-14-46-02.jpg

Hapa Diamond akimkabidhi zawadi ya gari Marehemu Muhidin Gurumo

Screenshot_2017-09-22-15-41-09.jpg

Diamond alimwaga mamilioni ya shilingi kwa kijana aliyetobolewa macho na scorpion.

Screenshot_2017-09-22-15-45-46.jpg


Screenshot_2017-09-22-15-45-46.jpg

Hawa watoto wamepata bahati ya kusomeshwa shule ya kimataifa inayofanya mtaala wa Cambridge na ada isiyopungua milioni 20 kwa mwaka mpaka watakapo fika ngazi ya chuo kwa kitendo chao tu cha kuibuka washindi kwa kucheza ngololo.

Mbali na haya Diamond pia amechimba visima vya maji visivyopungua 15 kwa shule mbalimbali hapa nchini hususani kwa mkoa wa Dar es salaam.

Katika kusaidia vijana Diamond pia hayupo nyuma, kuna wakati alikuwa anamlipa Haruna Moshi Boban nusu ya mshahara anaolipwa kipindi anachezea timu ya Friends Rangers.

Vilevile amesaidia kwa kiasi kikubwa sana kukuza na kuibua vipaji vya wasanii mbalimbali hapa nchini kwa mfano Rayvanny kipindi yupo Tip Top alikuwa hajulikani sana na ila Mondi akamchukua na kumsaidia kumtangaza mpaka akafanikiwa kuchukua tuzo ya BET mwaka huu. Wasanii wengine kama vile Harmonize, Lavalava, Queen Darleen nk.

Pia Diamond hayupo nyuma kusaidia wasanii wenzake. Mara kwa mara amekuwa akiwasaidia kuwapa pesa za kufanyia video wasanii wenzake na vilevile huwapa ofa ya kuchagua mavazi kwenye maduka yake ya nguo mara kwa mara.

Diamond pia alimsaidia Diva kumnunulia simu yenye thamani isiyopungua milioni moja.

Pia hata zile milioni 13 alizotoa Wema kumdhamini Kajala inasemekana zilitoka mikononi mwa Diamond ila hakutaka ijulikane kwa watu wengi.

Diamond mara kwa mara amekuwa akisifika kuwanunulia magari wasanii wenzake hasa katika sherehe za siku zao za kuzaliwa.

Diamond vilevile hayupo nyuma kwenye kusaidia mambo ya dini. Kuna kipindi alitaka kujenga msikiti utakao kuwa mkubwa kushinda yote hapa Africa Mashariki ingawaje suala hilo lilipingwa vikali sana na viongozi wa dini kwa kudai kuwa pesa zake ni haramu hazifai kujengea msikiti na hata kama akijenga yeye diamond hatopata thawabu zozote kwa hiyo itakuwa sawa na bure tu .

Diamond mara kwa mara amekuwa akisaidia wakina mama wasiojiweza kwa kuwapa misingi ya biashara ili kuweza kuendesha maisha yao.

Diamond pia amekuwa akiwapa motisha walimu kutoka shule mbalimbali anazozitembelea kwa kuwapa pesa na nyenzo za elimu za elimu kama vile vitabu nk.

Diamond pia hayupo nyuma katika kusaidia watoto yatima.

Screenshot_2017-09-22-16-11-34.jpg


Screenshot_2017-09-22-16-11-41.jpg


Screenshot_2017-09-22-16-11-57.jpg


Hakika Diamond Platnumz ni tunu ya taifa!
 
Labda apewe ubalozi wa nyumba kumi kumi Tandale

Sabodo anachimba visima 300 kila mwaka na anatoa mabilioni ya pesa toka zamani na hatusikii akiutaka ubunge

Huyo kutoa vijisaada tudogo mnataka apewe ukuu wa mkoa
 
Mlinga alisema Askari Monument iondolewe iwekwe sanamu ya Diamond, na wewe unasema apewe ukuu wa mkoa. Sikatai Diamond ni entertainer lakini haya mengine sina mengi ya kusema.
 
Back
Top Bottom