Diamond Platnumz aahidi kuwafanyia kufuru wanatandale

Ukilitizama jambo hilo Kwa jicho la tatu la kiroho kuna kitu utakiona lkn kwa waliolemaa kiakili na kiupeo wanaona ni misaada iliyotolewa na mwema, haya yetu macho!!!
 
Dada kuna watu wanatumia mtaji wa elfu 50 na wanalaza elfu 20 faida kila siku ... Sio lazma awape nyingi ..kama hauna plan ya biashara ata upewe milioni 20 zitapotea tu .
Acha zako? faida ya Elfu 20 watu wa wapi mkuu
 
Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz amewaahidi mambo yafuatayo wakazi wa Tandale (mahali alipozaliwa na kukulia)...

1. Kulipia BIMA ya Afya kwa watoto 300,na wakazi wengine 700 (Jumla watu 1000) ndani ya mwaka mmoja....

2. Kutoa mitaji kwa akina mama 200, ya shilingi za kitanzania 100,000/= mpaka 200,000/=

3. Kutoa Boda boda 20 kwa vijana wasio na ajira na kuwatengenezea aina fulani ya menejimenti ambapo kila siku kila kijana itampasa akabidhi sh. 10,000/= ambayo itatumika kununua bodaboda nyingine kwa ajili ya vijana wengine....

4. Kukarabati Shule zote za msingi zilizopo ndani ya Kata aliyozaliwa ya Tandale ikiwa ni pamoja na kuweka matank kwa ajili ya kuhifadhia maji...
maxresdefault.jpg
Diamond Platnumz
Diamond akiongea kwenye sherehe fupi iliyofanyika Live kupitia Wasafi TV, amesema kuwa siku ya Ijumaa Tarehe 5 Oktoba 2018 atatimiza ahadi hiyo ikiwa na pamoja kuchinja ng’ombe na kusherehekea na watu wake wa Tandale pamoja na wasanii wenzake, wageni mbalimbali kutoka serikalini na mashirika binafsi waliojitolea kumuunga mkono.
Kabla hayo je yule Mdada Hawa kafikia wapi !!??? Hzi ni Kiki tu
 
Back
Top Bottom