Diamond Platinumz: Kwa nini nipo VEVO? Nasaha kwa wasanii

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,761
Yawezekana wengi tulikuwa tunajiuliza kwa nini Diamond Platinumz kauweka wimbo wake wa Marry You kwenye Youtube Channel mpya kabisa ya DiamondPlatnumzVEVO badala ile tuliyoizoea ambayo ipo verified ya Diamond Platnumz. Kupitia Instagram post, Diamond katolea maelezo na kutoa ushauri kwa wasanii wengine wanaotaka kujiunga na VEVO. Haya hapa chini ni maelezo yake.

“Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo Vevo... Nikawambia: "uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida.. Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale,

na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo...na mbali tu ya kumlipa VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo".....

hivyo nikawambia: "siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida....

SABABU YA KUYASEMA HAYA:

Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu,

vilevile umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichkua juu ya sanaa zetu kwa sasa, maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae... nafaham wasanii wengi hawakuwa wakilifaham hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao..."

kwa uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine nimekosea Tafadhali mnisameh... –SIMBA”

Na kuongezea tu VEVO hawalipi msanii binafsi ni lazima awe kwenye record lebo yenye shareholder kama universal , sonny au rock nation. Wasanii wa Tanzania ambao awako kwenye record lebo hawanuafaiki zaidi ya kuwa na status tu yupo VEVO. Kuna siku mwaka Jana Flaviana Mtata aliuliza kwanin wasanii wa Tanzania wako VEVO wanajua haki zao? Wengi walimtukana ila nakumbuka wakazi alijitaidi kueleza kwaninn yeye hayupo VEVO,

 
mbona video za vanesa mdee kitambo huwa naziona na hiyo vevo, kwa nini kwa huyu ndio iwe kitu cha ajabu na iwe stori kama vile ni kitu kipya.
Tushangae wote, tatizo watoto wa tandale ulimbukeni, kila kitu kwao wanashikilia bango mfyuu
 
mbona video za vanesa mdee kitambo huwa naziona na hiyo vevo, kwa nini kwa huyu ndio iwe kitu cha ajabu na iwe stori kama vile ni kitu kipya.
Mkuu ukisoma vyema maelezo ya Diamond utamuelewa. Hakatai watu kuwepo VEVO, bali uwepo wao VEVO uwe na faida kwa pande zote mbili, kwamba msanii afaidike na pia VEVO wafaidike. Katika hilo maana yake ni jukumu la kila upande kuipromote nyimbo. Sio jukumu aachiwe msanii peke yake wakati faida wanapata wote. Ndio maana kama umegundua, VEVO wamekuwa msatari wa mbele kuupromote huu wimbo wa Diamond kwa sababu makataba wao unawataka hivyo. Ni kama ilivyo kwa mkataba wa Universal Music Group.
 
Rudia kusoma alichoandika mdau na kama bado utabakia na mawazo hayohayo...basi wew ni killlaza
Ahsante mr "Genius, a most intelligent one", bado nimeshindwa kuelewa "mbona video za vanesa mdee kitambo huwa naziona na hiyo vevo, kwa nini kwa huyu ndio iwe kitu cha ajabu na iwe stori kama vile ni kitu kipya."
 
Ahsante mr "Genius, a most intelligent one", bado nimeshindwa kuelewa "mbona video za vanesa mdee kitambo huwa naziona na hiyo vevo, kwa nini kwa huyu ndio iwe kitu cha ajabu na iwe stori kama vile ni kitu kipya."
Kwanini sasahivi? Jibu ni kwamba ukipitia a/c za VEVO za twitter na instagram utaona wanafanya Kazi ya kupromote wimbo wa marry you wa diamond ft neyo kote wamepost
Ndo maana diamond anakwambia kabla hajajiunga alitaka VEVO wenyewe watambue kina msanii wa Tanzania anaitwa diamond, hats kiwango cha pesa owe sawa na wasanii wa marekani per view,
Sasa sijui wewe hujaelewa wapi?
 
Unaposoma kitu kuwa makini hebu rudia kusoma upya utaelewa tuu na sio unaropoka tuuu
sina uhakika kama naropoka na nimerudia kusoma lakini bado nashangaa "mbona video za vanesa mdee kitambo huwa naziona na hiyo vevo, kwa nini kwa huyu ndio iwe kitu cha ajabu na iwe stori kama vile ni kitu kipya."
 
mbona video za vanesa mdee kitambo huwa naziona na hiyo vevo, kwa nini kwa huyu ndio iwe kitu cha ajabu na iwe stori kama vile ni kitu kipya.
Na Rose Muhando yupo vevo toka kitambo,but people know how to exaggerate things.
 
Tushangae wote, tatizo watoto wa tandale ulimbukeni, kila kitu kwao wanashikilia bango mfyuu
Mpwa bhana!

Alichosema Chibu ni sahihi. Mosi, huwezi kui-access VEVO from Tanzania na sidhani kama kuna nchi yoyote Africa unaweza kui-access... maybe SA. Na ndio maana hata ukiiangalia Marry You from Tanzania unaipata kupitia VEVO Youtube Channel na sio VEVO per se. Hii maana ni kwamba, majority wanaotumia VEVO kwa huku wanapitia kwa watu; tofauti na wewe unavyoweza kuingia Youtube popote pale na kufungua channel!

Moja ya kampuni zinazofanay hiyo shughuli (middlemen) ni JVT Digital.

Sasa hapo ndo linafuata swali... je; huko wanakopitia wanapata maslahi? Kwa mfano, mimi nikiwa na uwezo wa kuingia as admin kwenye Youtube channel ya kwako, nina uwezo wa kuweka code za matangazo na pesa nikalipwa mimi bila wewe kupata hata senti tano!!!
Na Rose Muhando yupo vevo toka kitambo,but people know how to exaggerate things.
Rose Mhando kuwa VEVO si ajabu kwa sababu Sony Music ni mmoja wa shareholders wa VEVO huku Universal akiwa ndie largest shareholder.

So, kwavile Rose yupo au alipata kuwa Sony Member kuwa na VEVO Account si jambo la ajabu!!!

Sasa hawa UMG, Sony and the like; kazi za wasanii walio chini yao ni kawaida kuzipitishia VEVO kwa ajili ya kudhibiti copyright issues ambazo ni kimeo kwa upande wa Youtube!!!
 
Na Rose Muhando yupo vevo toka kitambo,but people know how to exaggerate things.
Ishu siyo kuwa VEVO, ishu ni namna gani hao VEVO wanapromote kazi za msanii. Je ulishawahi kuona VEVO wamepost kazi za Vanessa, Alikiba au hata Rose Muhando? If hujui, hata Alikiba yupo VEVO, angalia kazi yake ya Aje remix. Alichoandika Diamond si kukuza mambo, bali kuwafumbua macho wasanii kwamba wasiingie mikataba kichwa kichwa bila kutathmini au kuhakisha hiyo mikataba inawafaidisha pande zote mbili.
 
Back
Top Bottom