Diamond mkanye sana baunsa wako bila huruma yako juzi ningempa kichapo

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,122
11,110
Jumapili iliyopita hii ya juzi nilikuwa supermarket ya Game pale mlimani city na familia Famillia yangu, ile nipo kwenye mizunguko yangu huku na kule nikiangalia bei za bidhaa mbali mbali zilizokuwepo pale mara paap nikashangaa tu limkono limeshiba na misuli minene eti linanizuia nisipite njia ile.

Kumbuka hapo nlikuwa sijui kama Diamond na Dem wake Tanasha wapo pale pale kwenye ule uchochoro nnaopita mimi, Baada ya yule Baunsa kunizuia nikamuangalia juu mpaka chini, juu kajazia na chini alikuwa mwembamba hivi alikuwa kavaa suruali Modo ,Chafu chafu hivi, kama fuko la mashineni.

Baada ya kumuangalia vizuri yule baunsa ndio ikabidi nitazame kushoto na kulia kuangalia ni nani aliyekuwa anampa jeuri yule Baunsa, kuangalia vizuri ndio nikamuona Diamond na dem wake Tanasha kumbe walikuwa pale pale,

Nikamwambia yule baunsa anipishe nipite pale sio nyumbani kwa mama yake, huku usoni nikiwa nimeshabadilika, nipatwa na hasira gafla, ile nataka kupita akanizuia tena ikabidi nimpe kikapu nilichokuwa nimekishika mke wangu, ili nimpe vitasa yule bausa pale pale maana hakujua kuwa sio kila mtu ana shobo na wasanii, so nilitaka nimshikishe adabu

Ile nataka kumrukia tu Diamond ndio akaingilia ule ugomvi akinisihi nimsamehe na niendelee na mishe zangu, kwa kisingizio kuwa atamkanya yule baunsa na ndio ikawa pona pona yake

Ushauri wangu kwako Daimond ajiri baunsa mmoja ambaye ni smart na ana elimu kuliko kubeba mabaunsa ya vichochoroni huko ambayo hayajui mipaka ya kazi zao, sio kila mtu anapenda kushobokea wasanii, tunakupenda lakini kwenye maisha ya mtu private huwa hatushobokeagi mtu wengine sisi ni watu wazima

Mkanye sana baunsa wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi Sana ungemtoa ngeu kwanza ili next tym asiparamie watu hovyo hovyo akijua wote washobokea wasaniii.
 
Back
Top Bottom