Diamond Mfalme wa Youtube kwa wasanii Kusini mwa Jangwa la Sahara, aweka rekodi nyingine

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
3,391
2,000
Msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amepiga hatua nyingine kubwa katika kazi yake ya muziki.

Screen-Shot-2021-04-05-at-18.02.00.png


Diamond kwa jina halisi Naseeb Abdul amekuwa mwanamuziki wa kwanza kusini mwa jangwa la sahara kupata subscriber milioni tano katika mtandao wa Youtube, kupitia chaneli yake ya youtube.

Mbali na kufikisha Subscriber mil 5 pia ndio msanii anayeoongoza kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi kwenye akaunti yake akiwa na watazamaji zaidi ya bilioni moja 1,356,274,369 views.

Diamond anafuatiwa kwa karibu na msanii Ryavanny mwenye subscriber milioni 2.6 huku Harmonize akiwa na milioni 2.4.

Wasanii wengine wengine wenye subscriber wengi ni Davido mwenye milioni 2.3 huku wasanii kama Burna boy akiwa na mil 1.8 na Wizkid akiwa na mil 1.6.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom