Diamond kurudisha kwa jamii kwa kujenga hospitali ya Moyo Tandale

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Mnyama.png

Katika harakati za kurudisha kwa jamii kile anachokipata, mkali wa wimbo ‘Marry You’, Diamond Platnumz, ameweka wazi mpango wake wa kujenga hospitali ya moyo na magonjwa mengine katika mtaa aliozaliwa, Tandale Jijini Dar es salaam.

Muimbaji alisema tayari amefanya mazungumzo na wadau mbalimbali na wamemuahidi kumpatia vifaa kwa ajili ya hospitali hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii wakati akizindua perfume yake mpya ‘CHBU’, Diamond alisema hospitali hiyo itawasaidia Watanzania wa hali ya chini.

“Mafanikio yote tunayopata hatusahau kurudisha kwa jamii kile tunachokipata,” alisema Diamond. “Ukiachana na misikiti ambayo nimekuwa nikiijenga katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania habari nje kwa ndugu zangu wa Tandale ni kwamba nataka kuwajengea hospitali ambayo itakuwa inatoa huduma pale kwa bei nafuu,”

Aliongeza, “Kuna wadau wangu wanakaa nje, nimezungumza nao wameniambia nijenge tu nay wao kuna baadhi ya vifaa wataleta. Kwa hiyo nikaona hii ni fursa na tayari kuna baadhi ya mambo ya mwanzo tumeanza kuyashughulikia. Nataka ufike muda watu waache kwenda kusafiri nje kutibiwa magonjwa mbalimbali kama moyo na mengine ambayo yamekuwa akitufanya tusafiri nje kwa ajili ya matibabu,”

Chanzo: Bongo5
 
Yeye kasema anajenga hospital.. Ili awarahisishie wanainchi.. Sasa tena anasema kaongea na wadau mbali mbali wampe VIFAA...HIVI.. HOSPITAL NI VIFAA au JENGO?
 
Kumbe chibu pafyumu zake ni mkakati wa free mason <br /><br />Yale maji ya maiti yamechanganywa na damu za paka na binadamu <br /><br />Kwa mtu atakaye tumia atakuwa ananyonywa damu bila kujua na baada ya muda ataandamwa na mikosi .
 
Acheni ushamba watu maarufu huanzisha na kufanya vitu kama hivyo vya kijamii kupitia foundation zao. Hata akiwa tu hata na 20 percent ya gharama zote. Jambo litakwisha tu. Matajiri wapo wanasubiri ukianzisha tu.
 
Back
Top Bottom