Diamond hivi huyu Mzee ni baba yako kweli? Mama anasemaje?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Nimefuatilia mahojiano ya huyu Mzee Abdul baba yake Diamond katika TV ya Carrymastori. Mzee anajikaza kiume.

Chini katika maoni nimeona comments za visichana na vivulana vya kizazi hiki vikimponda Mzee kuwa anastahili kupitia anayopitia kwa vile alimtelekeza Diamond akiwa mtoto.Inasikitisha!

Katika maisha,wanaume tunakabiliwa na mengi ila wengi huwa hatulii lii hovyo.

Kuna wanawake umezaa naye, unampa pesa ya matumizi huku anakutukana. Una kipato cha kawaida, unampa mzazi mwenzio pesa, ila anakutukana kuwa unatoa pesa gani ya mboga Unapigania umchukue mwanao,anafanya kila awezalo usifanikiwe. Inafika mahali anakuatambia ana bwana mwenye hela hivyo hababaishwi na vihela unavyomtumia.Unajikuta moyo unakufa ganzi. Mtoto anakuwa mkubwa, amelishwa sumu ya kutosha. Anakuona kama kibaka tu

Diamond unatakiwa kumjali sana baba yako. Ukiangalia hata kitambaa alichojifunga kama barakoa,utaona kiuhalisia aina ya maisha aliyonayo.

Mzee mwenye mtoto anayeweza kulipia kodi watu 500, na wakati huo umenunua hoteli ya mamilioni ya pesa, mzazi wako anafanya biashara ya umachinga wa kutembeza Viatu na corona hii! Ni nini hiki?

Wengine wanashindwa kuwajali wazazi kwa sababu ya uwezo mdogo, wewe una sababu gani ya kuruhusu mzazi aishi kwa unyonge jinsi hiyo?

Hivi haya masharti ya illuminat mbona yanakuwa ya ajabu sana? Au mama Diamond kwa nini usimwambie mwanao amjali baba yako kama anavyokujali wewe?

Au ulishamwambia ana baba mwingine?
 
Duu kwa hiyo kumkataa baba ndio masharti ya Illuminat,manake Mwana FA na Ommy Dimpoz hawana time kabisa na baba zao waliowakataa na wala hawa zungumziwi.

Ila si shangai tatizo moja la Diamond alilolikosea maisha yake ya familia kuyaweka mtandaoni.Ndio maana kila mtu anajiona ana haki kukosoa maisha ya Diamond,ila kaa ukijua haya mambo ya familia.
 
Angekuwa upande huu ningemshauri aifate ile WAHESHIMU BABA NA MAMA UPATE MIAKA MINGI NA HERI DUNIANI bila kujali walimfanyia nini ila kwa kujali bila wao asingekuwepo hapo na hivyo alivyo.

Kila kitu kinatokea kwa sababu ukute angemlea angemkomalia na shule tuuu asiwahi kujua kipaji chake na wala tusingewahi kumjua. Maisha haya ya mpito tu mwisho wa siku yeye aishi kwa raha zoooote na mzee wake naye aishi kwa raha au ateseke ni kufa tu. Duniani Hakuna Faida ya Kudumu kila kitu cha muda tu, tuishi kwa Amani na Kufarijiana.
 
Nisingeweza kumlaumu mwana FA kwani sijui uwezo wake ama Ommy dimpoz.After all sijui hata kama wanaishije na wazazi wao.

Kuhusu Diamond nimeshawishika kuandika kwa kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakimhoji baba yake na tunaona uhalisia wa maisha yake.Sasa tunalinganisha na "ukarimu" wa Diamond kwa watu baki wa kuwalipia kodi wakati baba yake mzazi anahangaikia mlo wa siku?Hii haiingii akilini.

Asamehe na asahau!Mungu kesharuhusu awe bilionea,roho mbaya ya nini?
Duu kwa hiyo kumkataa baba ndio masharti ya Illuminat,manake Mwana FA na Ommy Dimpoz hawana time kabisa na baba zao waliowakataa na wala hawa zungumziwi.

Ila si shangai tatizo moja la Diamond alilolikosea maisha yake ya familia kuyaweka mtandaoni.Ndio maana kila mtu anajiona ana haki kukosoa maisha ya Diamond,ila kaa ukijua haya mambo ya familia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nisingeweza kumlaumu mwana FA kwani sijui uwezo wake ama Ommy dimpoz.After all sijui hata kama wanaishije na wazazi wao.

Kuhusu Diamond nimeshawishika kuandika kwa kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakimhoji baba yake na tunaona uhalisia wa maisha yake.Sasa tunalinganisha na "ukarimu" wa Diamond kwa watu baki wa kuwalipia kodi wakati baba yake mzazi anahangaikia mlo wa siku?Hii haiingii akilini.

Asamehe na asahau!Mungu kesharuhusu awe bilionea,roho mbaya ya nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe umesema kumkataa mzee ni masharti ya Iluminat ina maana FA na Ommy ni Iluminat?

Hivi unajua FA na AY wameshinda kesi na Tigo wameingiza 2bilion?

Ommy Dimpoz corona tuu lkn kila siku ana kwea pipa.

Ndio maana na kwambia vipi wewe unajiona una haki ya kumkosoa Diamond,sababu Mondi kosa alilo lifanya kuyaweka maisha yake ya kifamilia mitandaoni,ila haya mambo ya familia huwezi jua yaliyo ndani.

Soma thread hii
Mwana FA amkana Baba yake mzazi - JamiiForums

Soma na huu

Ommy Dimpoz muombe msamaha baba yako mapema - JamiiForums
 
Alafu jambo la kushangaza anamchukia baba yake huku upande mwingine mama yake anakula bata na kajamaa flani, kwahiyo Mond yuko tayari hela zake ziliwe na kijana mwenzake anayeishi na mama yake kuliko baba yake mzazi.

Hatujui mama na baba yake walikosana nini sasa Diamond anarithi adui wa mtu mwingine, mama kamlisha sumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kupanda mbegu kwenye shamba halafu ukaitelekeza ukategema utakuja kupata mavuno mazuri. Ili liwe funzo kwa sisi wanaume tunaotelekeza watoto halafu wakifanikiwa tunaanza kulilia.
We unadhani asingekuwa juu angemhitaji kwani huyo mzee ana watoto wangapi? WHy Diamond?
 
Mzee mwenye mtoto anayeweza kulipia kodi watu 500, na wakati huo umenunua hoteli ya mamilioni ya pesa, mzazi wako anafanya biashara ya umachinga wa kutembeza Viatu na corona hii! Ni nini hiki?

Haijalishi Sana ni nini diamond kafanyiwa na baba yake Lakini Mzee hastahili hii Adhabu kabisa
Pia nikumbushe tuu
Wanawake ni viumbe wakatili Sana Sana watu wanasema They are devils

I'm on that good kush and alcohol
 
Huwezi kumlazmisha afeel kama we unavyo feel anastahili maana alimterekeza naye diamond aliumia kama ambavyo huyo mzee anaumia kuwa na baba mwenye pesa halafu anahangaika baba hana time naye
 
Haijalishi Sana ni nini diamond kafanyiwa na baba yake Lakini Mzee hastahili hii Adhabu kabisa
Pia nikumbushe tuu
Wanawake ni viumbe wakatili Sana Sana watu wanasema They are devils

I'm on that good kush and alcohol

Kwani hiyo adhabu anapewa na Diamond? Wako wapi wanawake aliowanunulia bia enzi za ujana wake, awatafute wamrudishie chenji.

And women are not devils. I'm sure there are milions of devils out there with dicks
 
Back
Top Bottom