Diamond azindua Pafyum yake ya Chibu, bei yake ni balaa

Huyu nae sifa zitakuja zimfilisi abakie historia tu.....kipindi shigongo anamdisi kuhusu gharama za show nilimuona kama hater kumbe alikuwa sahihi......toa bidhaa ambayo hata shabiki yako wa kawaida ataimudu....ingekuwa za buku ten au angalau twenty iv tungejichanga.....akanunue mwenyewe na wasafi wenzio.
Perfume zipo nyingi kuanzia tshs 2000 hadi 5mil. Sioni kama hiyo bei ni mbaya. Kikubwa ni quality. Na pia yeye ame target soko kubwa sio machinga. Tusimkatishe tamaa. Tumuunge mkono kwa wale watakaiweza kununua.
Kama tutakuwa na mentality za kimaskini kiasi cha kuona perfume hiyo ni bei kubwa bila hata kuangalia ubora tutakuwa hatumtendei Haki. Bravo diamond. Go on.soko lipo Tanzania na na nje ya mipaka. Naamini ni moja ya biashara itakayostawi. Hii ni surprise kwa wengi na hawakujua kama ungeweza kuwa na wazo LA Kijasiliamali kama hili. Big up.
 
Hii inanikumbusha 50 cent alivyotoa energy drink..watu walimbeza sana ..ooh huwezi kushindana na red bull wako sokoni kitambo..kufunga na kufumbua macho Coca cola wakainunua kwa $100m...sasa CHIBU itanunuliwa na kampuni kubwa wote mtakuja kushangaa..kama alivyotusua kimuziki bila ya kuwa na kipaji kikubwa hivyo hivyo kwa Chibu...mark my words
 
Ina ujazo wa lita ngapi?

Kwa uchumi huu wa magu ni watanzania wangapi wanaweza kununua perfume ya elfu 50? achilia mbali hiyo laki moja!
 
Market segmentation wachumi tunaita price discrimination, ukiona unalalamika ujue haujalengwa wewe,wapo wabongo ambao wananunua mpaka perfume za laki 4+,Na bidhaa kama hizi hawaangalii volume of sales wanaangalia revenue generation. That's why kuna Carina Ti na Bentley Continental.

Im neither his fan nor hater ila kwa hili nampongeza.
Wachumi mnaitaje?
Market segmentation.......price discrimination...???????
 
Huyu naye tuache kujipulizia ma perfume yetu yameenda shule tujipulize ushuzi huu toka tandale..kwanza kuna mtu kaniambia ina harufu kama mavi
 
perfume laki na ushee ndo kwnza watu awaijui ata sifa zake, unaanzaje kuintroduce kitu cha gharama kias icho bila kuelewa soko kubwa la wanunuzi ni rika lipi na watu wa aina gani

majority ya watu awana pesa kama hiyo kuchana misimbaz kumi kisa perfume, tena ndo ata aijaanza kusifika

uyu jamaa akahudhurie kozi ya commerce, ajui target market uyu
Mbon Zipo perfume za bei mbaya kuliko hiyo hapa bongo nao hawajui biashara?
 
Ubunifu bila plan ni upuuzi unazindua perfume unauza 105,000/=what is your target, inaamaana unafanya jambo bila kutazama nani unaekwenda kummuzia,mtanzania shabiki wa Diamond ana uwezo wa hiyo hela.
Kwani show zake mashabiki wake wanaweza kuingia? Mashabiki wengine hawana pesa hata kama kiingilio kingekuwa buku. Mashabiki wapo wa aina nyingi kuna wale wa mitandaoni kuna wa kwenye tv na redio kula wa callet tunes na kuna wa kuingia kwenye show za mamilioni na kununua bidhaa za malaki na kuna wa kununua bidhaa za bei ya kati kama tshts alizotoa. Mashabiki wote hao wana mchango wao kwa namna fulani.
 
Eeeh nimemuuliza mama lisa kasema inanukia harufu kama ya banda la kuku...
 
Diamond amezindua rasmi pafyumu yake ya Chibu, itauzwa kwa bei ya 105,000 bei ya rejareja ameomba sapoti kwani anatoa ajirakwa vijana
Zitapatikana GSM Mall, Mlimani City, pia zitakuwa zikipatikana kwenye ndege


Ingredients zake please
 
Tatizo mnapenda cheap stuff.
Amewaletea kitu kinakaa kwa muda.
Hope wanaume wa bongo wataacha kunuka jasho
Unakuta mtu kavaa shirt na suruali imenyooshwa vizuri Lkn ananuka jasho.
Du nakumbuka siku moja nilienda jengo la Airtel, Nikapanda elevator na vijana wa airtel, nilitamani kushuka maana vikwapa vilikuwa vinapuliza dampo scent
 
Chibu....jina baya kwa kwel haljanivutia kabisa
Bora hata angeiita diamond au platinums
Siez kutumia perfume et inaitwa chibu NO not me
...huna hela wewe,debe tupu acha mashauzi;
.ila wewe mndengereko kutumia username ya kichina yenye maana ya mk.und.u unaona fahari;
....hopeless!
 
Back
Top Bottom