Diamond atuhumiwa kumloga tanzanite...soma hapa tanzanite akifunguka kuhusu hili

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,281



Tanzanite, msanii aliyeibuka na kusikika zaidi katika masikio ya fans wengi wa bongo fleva baada ya kutoa wimbo wa ‘Uchawi na Wanga’ ambao ulifanana melody na ‘mbagala’ wimbo uliomtoa Diamond, amesema Nasibu Abdul a.k.a Diamond Platinum alimloga ili kumpoteza kabisa na alifikia hatua ya kukohoa damu na nywele za binadamu!

Tanzanite ambae pia jina lake linaendana na jina la Dimond (yote madini) alifunguka haya katika interview aliyofanya na Lucas Maziku, mtangazaji wa radio SAUT ya jijini mwanza.


“Dah, unajua msema kweli ni mpenzi wa Mungu na siwezi kuficha kwa sababu nikificha ntakuwa sijengi nabomoa, halafu mimi naweza kusema ni ulimbukeni tu wa baadhi ya wasanii wa Tanzania. Mimi nilipata matatizo flani hivi nilikuwa naugua tangu kipindi kile nimeachia wimbo wa wachawi na wanga.

Yeah, nimeugua kwa kipindi kirefu ugonjwa ambao yaani tumehangaika sana hospitali bila kupata matatizo yoyote kwa sababu nilikuwa nasumbuliwa na kifua, wazazi wangu walikuwa wanajua labda ilikuwa TB kwa sababu nilikuwa na hali mbaya kiukweli.

Nilikuwa nimepungua nilikuwa nakohoa, nilikuwa natoa makohozi yenye damu. Lakini hayo makohozi yalikuwa yanashangaza sana kwa sababu yalikuwa yanatoa nywele, nywele za binadamu za kichwani.” Alisema Tanzanite.


Aliendelea kufunguka “Hali ilikuwa mbaya ikabidi wazazi wangu waangalie upande wa pili (waganga wa kienyeji), sasa tulivyoangalia upande wa pili napo mambo yakawa magumu, lakini kila sehemu tuliyokuwa tunaenda, si unajua tena mambo ya upande wa pili siyaamini moja kwa moja lakini kwa nini kwamba kila sehemu niliyokuwa naenda nilikuwa naambiwa mtu flani, mtu flani, mtu flani...

Tumeenda sehemu kama 9 tena mikoa tofauti, umeelewa, lakini kila sehemu tunayoenda tulikuwa tunaambiwa bwana Nasibu Abdul ndiye anaefanya mambo haya, sasa Nasibu Abdul ni Diamond.


Na nikiangalia kisa labda au sababu, hao wazee walikuwa wananambia kuna vitu mlikuwa mnagombania na huyo mtu, hao wazee wenyewe hawajui kwamba ni vitu gani nilikuwa nagombania na huyo mtu, umenielewa vizuri eeh.” That’s Tanzanite akifunguka.


Jamaa kafunguka mengi, ikiwa ni pamoja na kilichomkuta alipokutana uso kwa uso na bwana Nasibu Abdul a.k.a Diamond Platinum, ilikuwa ni full vitisho kwa mujibu wa Tanzanite mwenyewe.



 
Chezea vya Watu Dogo.... Usione vinaelea tu... hichi kisa na kile cha kamanda BArlow vinaendana kiasi fulani..... Wivu tu ndio Umetawala basi hata Adam angewaroga watu kwa kumgeza Kutembea kwa Miguu... Tusiwe hivi ndugu japo wahenga walisema geza geza humshindi muingereza Diamond waache watoto wadogo waje kwangu wewe Songa mbele ushatoka.... waondolee mawe wakufuatao
 
Mimi mgumu sana kuamini hayo makitu wanaoyaita mauchawi ila nalazimika kuamini tu kwa sababu nikisoma bible nakuta upo. Kwa hiyo hapa kama kuna ukweli au hakuna shauri zao. Inakuwaje majina yawe na maana moja (MADINI) na wimbo wa kutokea ufanane?
 
Maumivu ya kichwa huanza polepole.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Na yeye ni mchawi tu maana amekili kwenda kwa wachawi wenzie kuaguliwa! Chaezea waganga wasikuhizi lazima wakugombanishe!
 
kweli mtu akitafta umaarufu haangalii, sa diamond akamroge huyu kijana ambaye ni watanzania wachache wanaomfahamu aache kuwaroga akina alikiba.
Dogo atakuwa ana matatizo ya akili aisee sijui haoni soo kwa aliyoyasema.
 
Mbona mnamtetea sana Diamond kwani yeye kakamilika? Mnaamini haendi kwa waganga? Mbona nasikia na yeye yumo kwenye ile kitu ya waashi huru? Kama kuna muumin mwenzie humu atuhakikishie maana najua hawakosekani.
 
Huyo dogo muongo mimi naishi nae huku tabata kisukuru kweli ni huu baba yake ni muislamu wa itikadi kali mithili ya sheikh ponda naalisha mwambie kama ataendelea muziki kitachompata asimlaumu..
Na kama ni kuumwa kaanza kabla hajafahamika; kutokana na kukiuka matakwa ya mzee wake.

Na ilifika kipindi hadi hadi akwa anataka kuchanganykiwa na laana hiyo ya mzee wake
 
Wakati Diamond amegombana na Wema Sepetu, demu alifunguka kua Diamond ana Chale nyingi sana mwilini.

Hii inamanisha ni Mlozi wa kiwango cha juu, yawezekana kuna kaukweli hapa!!
 
Sasa haya mambo ya usanii na ulozi sijui kama yatatupeleka popote kwenye karne hii ya Sayansi na Teknolojia. Ni vyema wasanii wetu waangalie kuboresha zaidi kazi zao badala ya kuleta longolongo kuwa nimelogwa oooh, nilikuwa nashindana na mtu. Mie sikubaliani kabisa na kulogwa hata kama huyo Diamond ana chale mwili mzima ni zake kwa faida yake huyo Tanzanite aseme mengine!
 
Wakati Diamond amegombana na Wema Sepetu, demu alifunguka kua Diamond ana Chale nyingi sana mwilini.

Hii inamanisha ni Mlozi wa kiwango cha juu, yawezekana kuna kaukweli hapa!!

ata Ali Kiba nae wanamuogopa sana,ana mapete yale ya kishirikina vidole karibu vyote na huwa anayavaa akiingia studio na akipanda stejini...muulize Lamar anajua mchongo wote wa Ali k,mpaka watu wakifika studio wakimkuta Ali wanahairisha kurekodi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom