Diamond ataka siku ya ndoa yake iwe sikukuu ya kitaifa

mashakani

JF-Expert Member
Aug 15, 2018
615
990
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz, inadaiwa kuwa amependekeza serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuitambua siku atakayo funga ndoa na mpenzi wake Tanasha raia wa Kenya na kuifanya kuwa sikukuu ya kitaaifa ‘’Public Holiday”, ikiwa na maana kwamba siku hiyo watu wasifanye kazi wala wanafunzi wasiende mashuleni.

Taarifa hizo zimeenea kwenye mitandao mbalimbali nchini Kenya na kujadiliwa na watu wengi, ambapo mtandao wa Ghafla umeandika kuwa Diamond amehairisha kufunga ndoa na Tanasha siku ya wapendanao kama alivyokuwa amepanga awali kwa kuwa siku hiyo mama wa mpenzi wake huyo atakuwa kazini, huku akiitaka serikari ya Tanzania kutizama uwezekano wa kufanya siku ya ndoa yake kuwa Sikukuu.

“Sababu ya kwanini imenibidi kubadili tarehe ya ndoa ni kwasababu mama yeke Tanasha atakuwa kazini siku ya Valenine’s Day. Sitaki iwe sherehe ndogo. Ikiwezekana ningependa serikali ya Tanzania kufikiria kuwa sikukuu ya kitaifa’’ umekaririwa mtandao wa Howwe Buz

Source: Times FM
 
Eeeeeh
Ni Bikira anamuoa Bikira?

Watu tupo busy na ya show ya Davido wiki hii.. yeye ni wanawake tu.. wanawake tu.. kituko

Analazimisha apendwe na huyo nyapu mpya.. ila imebumaaaaa.

Aache kutafuta kiki kwa kuongea upupwu..

Kuimba siku hizi ni kuvizia za wenzake naye aimbe.. hataki kuwaacha wapete wenyewe..

Abadilike shaaaaa
Zari ameendelea na yake na anapendwa zaidi na zaidi.. rozi jeusi lile lina nguvu haswaa
 
Back
Top Bottom