Elections 2010 Dialo na masha walijikaanga kwa mafuta yao?

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Inasemekana kutoolewana kwa wabunge wawili (CCM) wa jiji la Mwanza kumechangia kwa kiasi fulani kushindwa kwao. Nasikia mmoja alimwaga mboga, na mwingine akamwaga ugali.

Nyepesi zinasema, Dr.Diallo alimsaidia Wenje katika kufuatilia rufaa yake ili Masha asipite bila kupingwa. Kisha Masha kujua hilo, naye akaanza kumsaidia kimkakati Haines ili amshinde Diallo. Diallo naye akazidi kumsaidia Wenje. Umaarufu wa Dr. Slaa nao ukamwaga petroli juu ya moto unaowaka.

Hizi ni tetesi, ila kama ni kweli, VITA VYA PANZI NI FURAHA YA KUNGURU:israel:. CCM itabomoka hivi hivi; maana ivumayo haiudumu.
 
kwa sasa hatuna tena muda wa kujadili hawa wapuuzi waliopita tunaangalia mbele zaidi kaka ila endelea kutupa habari pindi uzipatapo pamoja na hoja maridhawa.
 
Inasemekana kutoolewana kwa wabunge wawili (CCM) wa jiji la Mwanza kumechangia kwa kiasi fulani kushindwa kwao. Nasikia mmoja alimwaga mboga, na mwingine akamwaga ugali.

Nyepesi zinasema, Dr.Diallo alimsaidia Wenje katika kufuatilia rufaa yake ili Masha asipite bila kupingwa. Kisha Masha kujua hilo, naye akaanza kumsaidia kimkakati Haines ili amshinde Diallo. Diallo naye akazidi kumsaidia Wenje. Umaarufu wa Dr. Slaa nao ukamwaga petroli juu ya moto unaowaka.

Hizi ni tetesi, ila kama ni kweli, VITA VYA PANZI NI FURAHA YA KUNGURU:israel:. CCM itabomoka hivi hivi; maana ivumayo haiudumu.

Huja kosea hata kidogo wao ndio walijikaaanga nasio mwingine sasa hapo kumsaidia Kinana na Mkamba haya wayajue vyema kuwa mchawi wa Jimbo la ILEMELA ni MASHA na NYAMAGANA ni DIALLO.

Na ndivyo hivyo watakavyo jikaaanga na kukiua chama (CCM) kuanzia 2012 chaguzi zingine za Chama hicho zitakapo fanyika,

Na katika Chaguzi hizo lazi ntawafunga TAKUKURU kwani nasi twajiaanda na mtandao wetu wa kuwachunguza jinsi wanavyotoa siri na wanavyopokea mrungura hawato amini subirini mtaona tuuu

Back
Top Bottom