Dialo: Elimu bure inatekelezwa nje ya Bajeti

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Dk Anthon Dialo amesema sababu kubwa ya fedha za maendeleo kutotumwa kwa halmashauuri ni suala la elimu bure kutekelezwa nje ya bajeti.

Diallo, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, amesema sababu nyingine ni Uchaguzi Mkuu uliopita na mchakato wa Katiba mpya ambao ulitumia fedha nyingi.

Mwenyekiti huyo amesema hayo baada ya mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Yanga Makaga kuiomba Serikali kuharakisha kutoa fedha za miradi ya maendeleo kwa kuwa hakuna hata mmoja ulioanza kutekelezwa.

Makaga ametoa kauli hiyo katika kikao cha wakuu wa idara kilichoitishwa na mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole kwa ajili ya kujadili uwajibikaji. “Kitendo hiki kinawafanya madiwani kuacha kufanya mikutano ya hadhara katika kata zao wakikwepa kuulizwa maswali ya miradi waliyoahidi,” amesema Makaga.

Kuanzia Julai hadi sasa halmashauri hiyo imepokea Sh45 milioni ambazo hazitoshi kutekeleza miradi iliyopo, hali inayosababisha wananchi wawalaumu watendaji kwa kushindwa kutimiza ahadi za Serikali.

Chanzo:Mwananchi

Mbowe kasema serikali imefilisika alafu kuna watu wanabisha!!
 
Eeeh jana si JPM alisema wamepeleka bil 177 kwenye halmashauri zote nchini na wakasema wanaosema hela hazijafika ni hela za chai na wamezoea kula kula
 
Tatizo lenu Watanzania U know Nothing About Vission.Coz Hamjui Rais We2 Mpendwa Kapanga Nn kwa ajil Ya Taifa Hili.Subilin Mtamkubali saaaana
 
Tatizo lenu Watanzania U know Nothing About Vission.Coz Hamjui Rais We2 Mpendwa Kapanga Nn kwa ajil Ya Taifa Hili.Subilin Mtamkubali saaaana
Sio kazi ya rais kupanga nini kwa ajili taifa, atekeleze ahadi alizozitoa kipindi anagombea urais. Hizo pesa anazosema Diallo kwamba zinatekeleza mpango wa elimu bure nje ya bajeti zinatoka wapi bila kuidhinishwa na bunge lw bajeti ya serikali?
 
Mungu mkubwa sana

Bahati nzuri Tamisemi ambayo inabeba na halmashauri za wilaya,majiji,miji, ZIKO OFISI YA RAIS!!! zamani zilikuwa ofisi ya waziri mkuu,hii ilisaidia rais kukwepa lawama.

Awamu hii rais kaamua kuzoa mamlaka yote na kumpoka waziri mkuu. Tuliona kuanzia kutangazwa

wakurugenzi,kuapishwa,kutumbuliwa,waziri mkuu na ofisi yake hawakuhusika kwa karibu kama tulivyozoea.Tukumbuke huyu kwa.mujibu wa katiba ndio mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za serikali.

Sasa wa kumlaumu kwa halmashauri zetu kukosa maendeleo ni rais moja kwa moja kwa kuwa halmashauri ziko chini yake,yeye ndiye haleti fedha huku kwa ajii ya maendeleo

watasingizia elimu,kwamba inafyonza hizo hela,lakini mbona elimu bure inapewa bilioni 18 kati ya makusanyo ya trilioni 1.3?

Namshauri rais arudishe Tamisemi kwa waziri mkuu haraka sana....haya mabango yaliyozagaa kuanzia shule za msingi yaliyoandikwa "ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa....." yanaitia aibu ofisi ya rais,hebu fikiria darasa limejengwa kwa miti lakini lina bango "ofisi ya rais",darasa la tope, hizi shughuli aachiwe waziri mkuu ambaye katiba inamtambua kama mtendaji wa kila siku

La mwisho,hivi waziri mkuu KABAKIZIWA kazi gani? maana hata la maafa hasikiki,inamaanisha pia si lake vinginevyo tungemuona bukoba!!
 
Sio kazi ya rais kupanga nini kwa ajili taifa, atekeleze ahadi alizozitoa kipindi anagombea urais. Hizo pesa anazosema Diallo kwamba zinatwkeleza mpango wa elimu bure nje ya bajeti zinatoka wapi bila kuidhinishwa na bunge lw bajeti ya serikali?
Hata mimi nina wasiwasi na hizo bilioni 18 kama zina uwezo wa kuhudumia maelfu ya shule za nchi hii,kuna kitu kinafichwa hapa either ni mabilioni zaidi ya hayo,mengi tu au shule zetu ziko hoi sana na elimu inaporomoka kwa kasi kwa kukosa resource,tusubiri matokeo ya shule miaka miwili kuanzia sasa
 
Tatizo lenu Watanzania U know Nothing About Vission.Coz Hamjui Rais We2 Mpendwa Kapanga Nn kwa ajil Ya Taifa Hili.Subilin Mtamkubali saaaana
vision ilishapangwa tangu enzi za jk,vision 2025,kama mpendwa wako naye ana vision yake,basi miluzi mingi humpoteza mbwa
 
nia ya kuiletea Tza maendeleo anayo,afanyaje fanyaje ndio kivumbi
 
nia ya kuiletea Tza maendeleo anayo,afanyaje fanyaje ndio kivumbi
kama una mipango,lakini huna mikakati ya kutekeleza ni sawa na bure tu,unataka kwenda dar es salaam lakini hujui njia,na hutaki kuelekezwa,huwezi kufika
 
."nasema hivi mtu yeyote atakae lalamika kua hela aliopewa kwenye miladi ya maendeleo haitoshi ,atakua amejifukuzisha kazi mwenyewe"by ----------------.
 
."nasema hivi mtu yeyote atakae lalamika kua hela aliopewa kwenye miladi ya maendeleo haitoshi ,atakua amejifukuzisha kazi mwenyewe"by ----------------.
unatakiwa uipokee hivyo hivyo,kama ya kuchimba kisima wewe chimba,ukimaliza kaa ule bata usubiri nyingine mwakani,

unalalamika.kwani hao wananchi uliwazaa wewe?
 
Hata mimi nina wasiwasi na hizo bilioni 18 kama zina uwezo wa kuhudumia maelfu ya shule za nchi hii,kuna kitu kinafichwa hapa either ni mabilioni zaidi ya hayo,mengi tu au shule zetu ziko hoi sana na elimu inaporomoka kwa kasi kwa kukosa resource,tusubiri matokeo ya shule miaka miwili kuanzia sasa
Wewe unafikiri zile ndege alizosema zitanunuliwa na kufanya idadi ziwe sita pesa zimetengwa na kuidhinishwa na kikao gani cha bunge?
 
Back
Top Bottom