KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Usimlilie Mbowe, ililie nchi yako Tanzania.Huyu mbowe huyu mtu asiyejua kutukana mtu, mbowe ambaye hajawahi kumdhalilisha mtu, kuna mtu mstaarabu kama mbowe hapa Tz
Mshawahi muona mbowe akimtukana au kumchafua mtu?Mshawahi kumuona mbowe akijikweza japo katokea familia ya kishua?
Mbowe ni gaidi?Haimake sense kabisa, mbowe ana ugaidi gani jamani?Mbona mnamnyanyasa sana?
Naombeni niongee tu kibinadamu
-Mbowe ana moyo kama nyie
-Mbowe anahisi maumivu kama nyie
-Kibinadamu mbowe ni baba na ana mke na watoto nani aisimamie familia yake?
-Ni upumbavu kumuweka mtu ndani kwa makosa ambayo ni ya uongo
-Nakwambia dhuluma mlizomfanyia mbowe mungu atawalipa mchana kweupe
-Kwanza mliharibu mali zake, mkatuma dc mmoja akaharibu green house zake kule hai, hamkumchoka mkamuharibia biashara zake zote, mkaua bilcanas kila kitu mmeharibu
Basi hamkuridhika sasa mmempea kesi ya ugaidi....nyie ni binadamu gani aisee?hivi mna moyo ninyi....Ila sirro weweOne day mungu atakulipa....You will pay for what you did....Ulitumwa na mwendazake leo yuko wapi
Na mungu alivyo fundi hakuna alowahi mgusa mbowe akabaki salama,jiulize why,,,mbowe ni hai na hai mbowe mtaikuta na mtaiacha na jimbo litabaki tu la chadema
Mama nakushangaa sana, hivi inakuaje unakubali jambo hili linakutia doa utawala wako?Mama unaheshimika ujue, huko nje wanakukubali mnoo but kwa hili unajiharibia sana, unatengeneza maadui mama pls stop this kuna nafsi inaniambia labda hauna mkono katika hii kesi lakini pls can you stop this oppression?Ondoa huu ukandamizaji
Kwanini bado tunaruhusu makesi yaloanzishwa na mwendazake yazidi kulitonesha kidonda hili taifa?Mama plz makesi yenye asili ya mwendazake yapigwe chini pls hakua na utu yule
Mimi nitakua wa mwisho kuamini mbowe ni gaidi kwanza haimake sense na hakuna igp anayenisikitisha kama sirro ila hakuna marefu yasiyo na ncha
Mateso alopitia mbowe ni magumu, na still akavumilia huyu jamaa ana moyo wa kimwamba aisee mimi hata robo siwezi narudia I can't! Wamemtesa sana wamemfanyia kila hujuma ila mungu atalipa soon
Mbowe ni chachu, ni sehemu ya kuitakasa nchi yetu iondokane na hizi najisi zilizojitokeza katika hii miaka ya hivi karibuni.
Mbowe atakuwa salama, na alama za uwepo wake katika taifa hili itakuwepo daima.