Dhuluma Hii Kwa Wana-Mbarali Ikomeshwe Sasa ( Makala Raia Mwema)

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
( Makala Hii Imechapwa Kwenye Raia Mwema juma hili)

Na Maggid Mjengwa,

KAMWE huwezi kuyazuia maji yatokanayo na chemchemi kwa kumwagia mchanga. Na kuna namna mbili za mwanadamu kuula mkate: Ama aukate slesi (slices) kwa maana ya vipande vipande, au aufakamie. Hilo la mwisho hufanywa na mtu mlafi, mtu mchoyo. Mtu mbinafsi.Watanzania tuna bahati mbaya ya kuwa na baadhi ya viongozi wenye hulka za kibepari miongoni mwa jamii ya watu wengi wanaoishi maisha ya kijamaa. Viongozi wenye kuendekeza tamaa ya mali na hata kufikia kuwatelekeza wananchi wanaowaongoza.
Naam. Kwa Serikali kubinafsisha yaliyokuwa mashamba ya taifa ya mpunga; Kapunga na Mbarali, kisha waziri mhusika, mwaka 2006 kujibu manung’uniko ya wananchi kwa kuwaambia “Serikali imeuza chake”, ni sawa kabisa na kujaribu kuzuia maji ya chemchemi kwa kumwagia mchanga. Manung’uniko ya wananchi hayakupungua, yanaendelea kutolewa. Ni chemchemi ya ukweli, haikaushwi kwa kumwagia mchanga.
Juzi hapa nilikuwa Mbarali. Nilifika hadi kijijini Nyeregete. Pale nikutana na kuzungumza na wananchi wenye kusikitishwa na namna Serikali inavyoshindwa kuwaelewa. Inahusu ardhi ya mashamba yao. Serikali imeyauza mashamba ya mpunga ya Kapunga na Mbarali kwa wafanyabishara wawili kupitia makampuni yao; yaani Highlands Estates Limited kwa shamba la Mbarali, na Export Trading Company Limited, kwa shamba la Kapunga.
Kilimo kina falsafa yake. Mkulima ni shamba lake. Pale kijijini Nyeregete nilielewa zaidi kuwa hakuna faraja na heshima kubwa kwa mkulima kama kurudi nyumbani akiwa ametoka shambani kwake. Na hakuna fedheha kubwa kwa mkulima kama kurudi kutoka kwenye kibarua cha shamba la mtu mwingine. Kwamba hana shamba. Kwa mkulima kutokuwa na shamba analolimiliki, hata kwa kukodi ni sawa na kupoteza sehemu ya uhai wake.
Kule Mbarali wananchi wana kilio cha haki. Wamebaini dhuluma waliyofanyiwa na Serikali yao kwa kushirikiana na wanaoitwa wawekezaji. Pamoja na kuwa zaidi ya ekari elfu saba (7000) za mashamba ya mpunga ya iliyokuwa NAFCO kubinafsishwa, wawekezaji ama wachukuaji hao wa mali ya umma wamefikia hatua ya kuchukua maeneo nje ya mipaka ya yaliyokuwa mashamba ya NAFCO.
Wameingia kwenye maeneo ambayo wananchi wamekuwa wakijilimia mashamba yao ya mpunga. Wakulima wa kata za Songwe, Rujewa na Ubaruku leo ni mfano wa wanaoishi kwa mashaka kwenye bonde la Usangu. Walichofanyiwa ni dhuluma kubwa. Ni uonevu mkubwa. Umefanywa mchana wa jua kali.
Wananchi wa Mbarali wanajiuliza: Wameikosea nini serikali yao? Miaka ya sitini wazazi na babu zao waliambiwa waondoke kwenye maeneo ya makazi na mashamba yao ili wapishe mradi mkubwa wa taifa wa kilimo cha mpunga. Walikubali. Sio tu kukubali na kukaa kando, walishiriki kwa hali na mali kufanikisha mradi huo.
Serikali ilipoamua kubinafsisha mashamba hayo, walitegemea nao wangepewa nafasi ya kuingia ubia na wawezekaji kupitia vyama vyao ya ushirika. Hilo halikutokea. Mawaziri wale wawili wakishirikiana na viongozi wa wilaya walikuwa mstari wa mbele kufanikisha zoezi lililowanyima haki wananchi.
Ninavyoandika hii leo, mawaziri wale wawili hawapo bungeni. Mkuu yule wa wilaya naye hayupo kwenye utumishi wa serikali. Lakini, watatu wale wamewaachia wana Mbarali dhahma kubwa na majonzi makubwa.
Kimsingi, uamuzi wa kubinafsisha mashamba ya Kapunga na Mbarali ulikuwa ni uamuzi wa makosa na ulioharakishwa kwa sababu za kutanguliza maslahi binafsi ya viongozi walioongoza zoezi hilo. Na historia itawahukumu wote walioshiriki na wanaondelea kushiriki kuitenda dhuluma hii kwa wananchi.
Ndio, kule Mbarali mwaka 2006 walifika mawaziri wawili; mmoja mwenye dhamana ya uwekezaji na mwingine wa kilimo. Waliwapa wananchi majibu ya kukatisha tamaa juu ya madai yao ya haki. Na mawaziri hao wawili wote wametupwa chini kwenye kura za maoni ndani ya CCM kuwania ubunge kwa mwaka huu. Leo hawakubaliki hata na wananchi huko walikotoka.
Wananchi wa Mbarali hawakukosea, miaka minne iliyopita, kutilia shaka dhamira mbaya za mawaziri wale wawili. Na hata aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali naye, hadharani alitiliwa shaka dhamira yake mbaya. Naye alitupwa chini kwenye kura za maoni jimboni Ubungo. Hakubaliki hata huko alikotoka.
Uamuzi wa makosa wa kuyabinafsisha mashamba ya mpunga ya Kapunga na Mbarali umesababisha kuporomoka kwa uchumi wa Mbarali. Mathalan; mji mdogo wa Rujewa uliokuwa ukikua kwa kasi sasa umeanza kusinyaa. Shughuli za kiuchumi zimepungua. Hakuna mzungunguko wa fedha kama zamani.
Umasikini wa kipato umeongezeka.
Na si tu uchumi wa watu wa Mbarali unaporomoka kutokana na ubinafsishaji huu kipofu, bali hata umaarufu wa chama tawala CCM nao unaporomoka miongoni mwa Wana-Mbarali.
Matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yametuma ujumbe mkubwa kwa CCM kutoka kwa watu wa Mbarali. Wakati mwaka 2006 Mwenyekiti wa CCM, Mbarali alitamba sera za ubinaifshaji za CCM zinakubalika maana CCM ilipata ushindi jimboni humo kwa asilimia 85, mwaka huu CCM imeambulia nusu ya asilimia ya mwaka 2006.
Kisiasa, unapoona mgombea wa chama cha upinzani asiye na jina kubwa, mwananfunzi wa Chuo Kikuu, anaingia ulingoni bila fedha nyingi za kampeni, na bado anapata kura zaidi ya elfu kumi na tano, basi, ujue kuna jambo hapo.
Leo kule Mbarali tumeambiwa na Waziri mwenye dhamana kuwa “serikali imeuza chake”. Ni kweli, kama mwenye basi ameamua kuuza basi lake, kondakta hana kauli. Lakini, hapa kuna tofauti kubwa, tunazungumzia ardhi ya kilimo, uhai wa mtu. Anayeupigania uhai wake huwezi kumfananisha na kondakta wa basi.
Aliyesema serikali “imeuza chake” alipaswa kutafakari kabla ya kusema na si kinyume chake. Ni kauli ya dhihaka, imejaa kejeli kwa mwananchi mnyonge. Wananchi hawakutarajia kauli kama hiyo itolewe kwao na waziri mwandamizi wa serikali waliyoiingiza wenyewe madarakani.
Bila shaka Watanzania ni wapenda amani sana. Katika nchi za wenzetu kiongozi anayetoa kauli ya namna hii kwa wananchi wenye matatizo na wenye njaa, basi, angekuwa na wakati mgumu sana. Mdomo wenye njaa ni mdomo wenye hasira. Tukubali, kuwa uvumilivu una kikomo hata kwa Watanzania. Busara si kusubiri kuona ukomo wa uvumilivu huo.
Katika nchi zetu hizi, ufisadi hujificha katika zinazoitwa sera za serikali kama hii sera ya ubinafsishaji. Ndani ya ubinafsishaji huu kuna ufisadi uliojificha. Akili ya kawaida inatuambia kuwa hakuna mantiki ya kuwanyima haki ya kumiliki mashamba wazawa walioonyesha uwezo mkubwa wa kuendesha kilimo endelevu na kutoa mazao mengi yenye kuyajaza maghala ya vyakula.
Tangu mwaka 2001 wananchi wa Mbarali wameomba kutaka kuyamiliki mashamba ya iliyokuwa NAFCO. Sababu ya kuyamiliki mashamba wanazo, nia ya kufanya hivyo wanayo na uwezo wa kuyamiliki mashamba hayo wanao. Kinachokesekana ni dhamira ya kweli kutoka kwa wanasiasa na watendaji wengine ya kuwamilikisha mashamba hayo wananchi.
Kwa kiasi fulani, hii inachangiwa na ufisadi. Na tujiulize: wakati wananchi wa Mbarali hawajaonyesha kushindwa kuyamiliki na kuyaendesha mashamba hayo, iweje leo waje kumilikishwa wengine kirahisi tu?
Tufanye nini?
Kama Serikali inavyofanya katika maamuzi mengine yaliyofanyika nyuma na yaliyo na mapungufu, serikali hiyo hiyo haina budi kupitia upya uamuzi huu wa kuyabinaifsisha mashamba ya Mbarali.
Tujiulize; hivi ni wawekezaji gani hawa wanaokuja kuwekeza wakati tayari mashamba yapo na miundo mbinu imeshatayarishwa kwa nguvu za serikali yetu, nchi rafiki ya China na wananchi wetu? Ni wawekezaji gani hawa wanaokuja kuvuna kilichopandwa?
Nchi hii ina mabonde ya maji makubwa tisa. Kwa nini wasiende kuwekeza kwenye mabonde ambayo hayajaendelezwa kama lile bonde la Ziwa Rukwa? Wanananchi wa Mbarali bado wana imani ya kilio chao kusikilizwa. Kwamba dhuluma hii wanayofanyiwa ikomeshwe, sasa.
 
Aisee wewe ndio ulisema Lipumba atashika nafasi ya pili ya urais? Mbona umehamia huku kwenye kilimo, au kwa kuwa utabiri ulienda mrama?
 
Hii ndo kazi nzuri inafanywa na serikali ya CCM na bado watajuuta kuijua na kuichagua CCM

Watu wanapigania HAKI lakini wapo wachache kwa masrahi yao binafsi wanadai kupigania HAKI ni uvunjifu wa amani
 
( Makala Hii Imechapwa Kwenye Raia Mwema juma hili)

Na Maggid Mjengwa,

KAMWE huwezi kuyazuia maji yatokanayo na chemchemi kwa kumwagia mchanga. Na kuna namna mbili za mwanadamu kuula mkate: Ama aukate slesi (slices) kwa maana ya vipande vipande, au aufakamie. Hilo la mwisho hufanywa na mtu mlafi, mtu mchoyo. Mtu mbinafsi.Watanzania tuna bahati mbaya ya kuwa na baadhi ya viongozi wenye hulka za kibepari miongoni mwa jamii ya watu wengi wanaoishi maisha ya kijamaa. Viongozi wenye kuendekeza tamaa ya mali na hata kufikia kuwatelekeza wananchi wanaowaongoza.
Naam. Kwa Serikali kubinafsisha yaliyokuwa mashamba ya taifa ya mpunga; Kapunga na Mbarali, kisha waziri mhusika, mwaka 2006 kujibu manung'uniko ya wananchi kwa kuwaambia "Serikali imeuza chake", ni sawa kabisa na kujaribu kuzuia maji ya chemchemi kwa kumwagia mchanga. Manung'uniko ya wananchi hayakupungua, yanaendelea kutolewa. Ni chemchemi ya ukweli, haikaushwi kwa kumwagia mchanga.
Juzi hapa nilikuwa Mbarali. Nilifika hadi kijijini Nyeregete. Pale nikutana na kuzungumza na wananchi wenye kusikitishwa na namna Serikali inavyoshindwa kuwaelewa. Inahusu ardhi ya mashamba yao. Serikali imeyauza mashamba ya mpunga ya Kapunga na Mbarali kwa wafanyabishara wawili kupitia makampuni yao; yaani Highlands Estates Limited kwa shamba la Mbarali, na Export Trading Company Limited, kwa shamba la Kapunga.
Kilimo kina falsafa yake. Mkulima ni shamba lake. Pale kijijini Nyeregete nilielewa zaidi kuwa hakuna faraja na heshima kubwa kwa mkulima kama kurudi nyumbani akiwa ametoka shambani kwake. Na hakuna fedheha kubwa kwa mkulima kama kurudi kutoka kwenye kibarua cha shamba la mtu mwingine. Kwamba hana shamba. Kwa mkulima kutokuwa na shamba analolimiliki, hata kwa kukodi ni sawa na kupoteza sehemu ya uhai wake.
Kule Mbarali wananchi wana kilio cha haki. Wamebaini dhuluma waliyofanyiwa na Serikali yao kwa kushirikiana na wanaoitwa wawekezaji. Pamoja na kuwa zaidi ya ekari elfu saba (7000) za mashamba ya mpunga ya iliyokuwa NAFCO kubinafsishwa, wawekezaji ama wachukuaji hao wa mali ya umma wamefikia hatua ya kuchukua maeneo nje ya mipaka ya yaliyokuwa mashamba ya NAFCO.
Wameingia kwenye maeneo ambayo wananchi wamekuwa wakijilimia mashamba yao ya mpunga. Wakulima wa kata za Songwe, Rujewa na Ubaruku leo ni mfano wa wanaoishi kwa mashaka kwenye bonde la Usangu. Walichofanyiwa ni dhuluma kubwa. Ni uonevu mkubwa. Umefanywa mchana wa jua kali.
Wananchi wa Mbarali wanajiuliza: Wameikosea nini serikali yao? Miaka ya sitini wazazi na babu zao waliambiwa waondoke kwenye maeneo ya makazi na mashamba yao ili wapishe mradi mkubwa wa taifa wa kilimo cha mpunga. Walikubali. Sio tu kukubali na kukaa kando, walishiriki kwa hali na mali kufanikisha mradi huo.
Serikali ilipoamua kubinafsisha mashamba hayo, walitegemea nao wangepewa nafasi ya kuingia ubia na wawezekaji kupitia vyama vyao ya ushirika. Hilo halikutokea. Mawaziri wale wawili wakishirikiana na viongozi wa wilaya walikuwa mstari wa mbele kufanikisha zoezi lililowanyima haki wananchi.
Ninavyoandika hii leo, mawaziri wale wawili hawapo bungeni. Mkuu yule wa wilaya naye hayupo kwenye utumishi wa serikali. Lakini, watatu wale wamewaachia wana Mbarali dhahma kubwa na majonzi makubwa.
Kimsingi, uamuzi wa kubinafsisha mashamba ya Kapunga na Mbarali ulikuwa ni uamuzi wa makosa na ulioharakishwa kwa sababu za kutanguliza maslahi binafsi ya viongozi walioongoza zoezi hilo. Na historia itawahukumu wote walioshiriki na wanaondelea kushiriki kuitenda dhuluma hii kwa wananchi.
Ndio, kule Mbarali mwaka 2006 walifika mawaziri wawili; mmoja mwenye dhamana ya uwekezaji na mwingine wa kilimo. Waliwapa wananchi majibu ya kukatisha tamaa juu ya madai yao ya haki. Na mawaziri hao wawili wote wametupwa chini kwenye kura za maoni ndani ya CCM kuwania ubunge kwa mwaka huu. Leo hawakubaliki hata na wananchi huko walikotoka.
Wananchi wa Mbarali hawakukosea, miaka minne iliyopita, kutilia shaka dhamira mbaya za mawaziri wale wawili. Na hata aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali naye, hadharani alitiliwa shaka dhamira yake mbaya. Naye alitupwa chini kwenye kura za maoni jimboni Ubungo. Hakubaliki hata huko alikotoka.
Uamuzi wa makosa wa kuyabinafsisha mashamba ya mpunga ya Kapunga na Mbarali umesababisha kuporomoka kwa uchumi wa Mbarali. Mathalan; mji mdogo wa Rujewa uliokuwa ukikua kwa kasi sasa umeanza kusinyaa. Shughuli za kiuchumi zimepungua. Hakuna mzungunguko wa fedha kama zamani.
Umasikini wa kipato umeongezeka.
Na si tu uchumi wa watu wa Mbarali unaporomoka kutokana na ubinafsishaji huu kipofu, bali hata umaarufu wa chama tawala CCM nao unaporomoka miongoni mwa Wana-Mbarali.
Matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yametuma ujumbe mkubwa kwa CCM kutoka kwa watu wa Mbarali. Wakati mwaka 2006 Mwenyekiti wa CCM, Mbarali alitamba sera za ubinaifshaji za CCM zinakubalika maana CCM ilipata ushindi jimboni humo kwa asilimia 85, mwaka huu CCM imeambulia nusu ya asilimia ya mwaka 2006.
Kisiasa, unapoona mgombea wa chama cha upinzani asiye na jina kubwa, mwananfunzi wa Chuo Kikuu, anaingia ulingoni bila fedha nyingi za kampeni, na bado anapata kura zaidi ya elfu kumi na tano, basi, ujue kuna jambo hapo.
Leo kule Mbarali tumeambiwa na Waziri mwenye dhamana kuwa "serikali imeuza chake". Ni kweli, kama mwenye basi ameamua kuuza basi lake, kondakta hana kauli. Lakini, hapa kuna tofauti kubwa, tunazungumzia ardhi ya kilimo, uhai wa mtu. Anayeupigania uhai wake huwezi kumfananisha na kondakta wa basi.
Aliyesema serikali "imeuza chake" alipaswa kutafakari kabla ya kusema na si kinyume chake. Ni kauli ya dhihaka, imejaa kejeli kwa mwananchi mnyonge. Wananchi hawakutarajia kauli kama hiyo itolewe kwao na waziri mwandamizi wa serikali waliyoiingiza wenyewe madarakani.
Bila shaka Watanzania ni wapenda amani sana. Katika nchi za wenzetu kiongozi anayetoa kauli ya namna hii kwa wananchi wenye matatizo na wenye njaa, basi, angekuwa na wakati mgumu sana. Mdomo wenye njaa ni mdomo wenye hasira. Tukubali, kuwa uvumilivu una kikomo hata kwa Watanzania. Busara si kusubiri kuona ukomo wa uvumilivu huo.
Katika nchi zetu hizi, ufisadi hujificha katika zinazoitwa sera za serikali kama hii sera ya ubinafsishaji. Ndani ya ubinafsishaji huu kuna ufisadi uliojificha. Akili ya kawaida inatuambia kuwa hakuna mantiki ya kuwanyima haki ya kumiliki mashamba wazawa walioonyesha uwezo mkubwa wa kuendesha kilimo endelevu na kutoa mazao mengi yenye kuyajaza maghala ya vyakula.
Tangu mwaka 2001 wananchi wa Mbarali wameomba kutaka kuyamiliki mashamba ya iliyokuwa NAFCO. Sababu ya kuyamiliki mashamba wanazo, nia ya kufanya hivyo wanayo na uwezo wa kuyamiliki mashamba hayo wanao. Kinachokesekana ni dhamira ya kweli kutoka kwa wanasiasa na watendaji wengine ya kuwamilikisha mashamba hayo wananchi.
Kwa kiasi fulani, hii inachangiwa na ufisadi. Na tujiulize: wakati wananchi wa Mbarali hawajaonyesha kushindwa kuyamiliki na kuyaendesha mashamba hayo, iweje leo waje kumilikishwa wengine kirahisi tu?
Tufanye nini?
Kama Serikali inavyofanya katika maamuzi mengine yaliyofanyika nyuma na yaliyo na mapungufu, serikali hiyo hiyo haina budi kupitia upya uamuzi huu wa kuyabinaifsisha mashamba ya Mbarali.
Tujiulize; hivi ni wawekezaji gani hawa wanaokuja kuwekeza wakati tayari mashamba yapo na miundo mbinu imeshatayarishwa kwa nguvu za serikali yetu, nchi rafiki ya China na wananchi wetu? Ni wawekezaji gani hawa wanaokuja kuvuna kilichopandwa?
Nchi hii ina mabonde ya maji makubwa tisa. Kwa nini wasiende kuwekeza kwenye mabonde ambayo hayajaendelezwa kama lile bonde la Ziwa Rukwa? Wanananchi wa Mbarali bado wana imani ya kilio chao kusikilizwa. Kwamba dhuluma hii wanayofanyiwa ikomeshwe, sasa.
Tukisema mnadhani tunatania jamani kunawatu wanaumia watanzania tunaumia jk please wake up mkuuu utalala mpaka lini!??
 
Unavyo tetea HAKI za wanyonge hawa hawa watakwambia wewe mdini, mkabila, unahatarisha amani wkt ndugu zake yaani wajomba zake, mashemeji zake, dada zake, binamu zake, mama zake wanaumia sana kwa kukosa HAKI zao za msingi
 
Mbarali wametaka wenyewe waache waumie tu. Tangu mwanzo wameelezwa jinsi ufisadi wa ardhi etc unavyoendeshwa wilayani mwao na wakapewa somo kamili jinsi ya kuuondosha lakini wakajifanya ndiyo JK na CCM basi mtaipata faida yake. Wajue kwanza CCM haina huruma nao. Na ikumbukwe kuwa Rostam nimemwona Mbarali mara nyingi kuna nini na tunamjua yeye na jamaa zake ni wezi wa mchana wa mali zetu hana huruma kabisa
 
Aisee wewe ndio ulisema Lipumba atashika nafasi ya pili ya urais? Mbona umehamia huku kwenye kilimo, au kwa kuwa utabiri ulienda mrama?
I think Maggid alikua na haki ya kusema alichosema... tuache kumnanga tuangalie mbele

we like sticking in the back sio?
 
Sawa sawa mzee wa Let us call spade and not big spoon

Mambano yanaendelea kuwanyima watu HAKI zao za msingi kwa mgongo wa kuhatarisha amani hii haiingii akilini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom