Dhulma kwa wananchi katika kata ya Mkambarani mkoani Morogoro-chachu ya mageuzi ya kiutawala

CCM MKAMBARANI

JF-Expert Member
Mar 15, 2017
1,379
950
Habari zenu wanajukwaa?

Kutokana na kuwepo kwa wizi wa raslimali hasa ardhi katika mkoa wa Morogoro hasa ktk kata ya Mkambarani hatari iliyopo ni kutokea kwa mageuzi ya kiungozi hasa kwa ngazi ya U-bunge na U-diwani.

Katika kata ya Mkambarani maji imekuwa janga kubwa kutokana na wizi unaoendelea na kufumbiwa macho na mamlaka husika.

Takribani shilingi zaidi ya milioni 150 zimechotwa na viongozi waliokuwepo,jambo hili limelalamikiwa sana lakini hakuna mkuu wa wilaya wala mkoa aliyejishughulisha nalo kiutatuzi zaidi ya maneno ya hapa na pale.

Salamu hizi ni ndogo na ni ishara kuwa mageuzi wenda yakatokea.Nikitulia ntaandika na kuweka viambatanisho baadae.
Cc.Polepole na wanaCCM wote hadi Bashiru.

Professor Mshauri wa chama.
Safarini Matombo.
 
Back
Top Bottom