Dhihaka ya Barabara ya IKULU...

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,545
29,617
Wanabodi, kwa wanaoishi ama kuelekea maeneo ya kigamboni mtakubaliana nami ktk hoja yangu hii.

Awali ile kona ya Ocean Rd Hospitali kuliwekwa bango (la majaribio) kuzuia magari kupita nyuma ya ikulu kuanzia saa 12 jioni hadi saa 12 ahsubuhi, hali hii imesababisha usumbufu kwa magari yanayokwenda feri hasa yanayovuka kwani ile junction ya soko la samaki kuna kuwa na vurugu kubwa ya magari nyakati hizo za kuanzia saa 10 hadi saa 3 usiku. Mantiki ya katazo hilo haikuwekwa wazi ambapo labda nikahisi ni masuala ya kiusalama (ingawa eneo lenyewe la ikulu limezungukwa na vibaka wenye njaa kali)

Hivi ninavyoandika hapa leo, ile barabara ya Ikulu imefungwa kabisa kwa magari kutopita muda wowote. Cha ajabu ni kwamba haijulikani amri ya kuifunga ile njia imetoka kwa nani na kwa sababu zipi.. Kuna mambo kadhaa niliyawaza hapa
  • Labda eneo la mbele/nyuma ya Ikulu ni eneo hatari ama hatarishi kwa usalama wa mkuu wa nchi hivyo imetangazwa hali ya hatari kwa kipande hicho...
  • Labda kwa sababu kuna uwezekano wa mambo ya kizani kuendelea kutamalaki hivyo kuzuia magari ni njia muafaka ya kufanikisha hayo
  • Labda mamlaka ya Jiji inajipendekeza kwa mkulu
Kwa maoni yangu ni kwamba huu ni uonevu mkubwa kuifunga hiyo barabara kwani kero za foleni ya kusubiria pantoni inakera mno. Ile hali ya kupitia njia ya Waziri mkuu inasababisha ajali zinazoweka kuzuilika...

nani nyuma ya hii dhihaka?
 
wewe...!
 
Damu ya wakala wa CDM Igunga imeanza kumuandama Mkulu, anahofia maisha yake kuwa hatarini...

Upande mwingine watu wanataka kutenganisha urais na uenyekiti wa chama. Bora kuziba njia ili kuimarisha usalama, haya mambo ni magumu...

Upande mwingine tena wanataka kurudia kuanza kuleta maandamano yao ili nchi isitawalike, kisa Dowans, barabara zaidi zitafungwa...
 
It is the public who owns the state house. I see the begining of privatization of a public house. It is utterly nonsense.
 
Huu ndio ufisadi wenyewe...kwanini Mwalimu JK Mwinyi hata Mkapa hawakufunga barabara....Watu tunahaha na mahali pa kupita wao wanafanya barabara kama mali binafsi.... Mie naomba huu mjadala usogezwe mbele wahusika waeleze kwanini maana sasa hivi kwa wingi wa magari nadhani kufunga barabara kwa matumizi binafsi ni kuwatesa wananchi
 
Wanabodi, kwa wanaoishi ama kuelekea maeneo ya kigamboni mtakubaliana nami ktk hoja yangu hii.

Awali ile kona ya Ocean Rd Hospitali kuliwekwa bango (la majaribio) kuzuia magari kupita nyuma ya ikulu kuanzia saa 12 jioni hadi saa 12 ahsubuhi, hali hii imesababisha usumbufu kwa magari yanayokwenda feri hasa yanayovuka kwani ile junction ya soko la samaki kuna kuwa na vurugu kubwa ya magari nyakati hizo za kuanzia saa 10 hadi saa 3 usiku. Mantiki ya katazo hilo haikuwekwa wazi ambapo labda nikahisi ni masuala ya kiusalama (ingawa eneo lenyewe la ikulu limezungukwa na vibaka wenye njaa kali)

Hivi ninavyoandika hapa leo, ile barabara ya Ikulu imefungwa kabisa kwa magari kutopita muda wowote. Cha ajabu ni kwamba haijulikani amri ya kuifunga ile njia imetoka kwa nani na kwa sababu zipi.. Kuna mambo kadhaa niliyawaza hapa
  • Labda eneo la mbele/nyuma ya Ikulu ni eneo hatari ama hatarishi kwa usalama wa mkuu wa nchi hivyo imetangazwa hali ya hatari kwa kipande hicho...
  • Labda kwa sababu kuna uwezekano wa mambo ya kizani kuendelea kutamalaki hivyo kuzuia magari ni njia muafaka ya kufanikisha hayo
  • Labda mamlaka ya Jiji inajipendekeza kwa mkulu
Kwa maoni yangu ni kwamba huu ni uonevu mkubwa kuifunga hiyo barabara kwani kero za foleni ya kusubiria pantoni inakera mno. Ile hali ya kupitia njia ya Waziri mkuu inasababisha ajali zinazoweka kuzuilika...

nani nyuma ya hii dhihaka?
Ikulu ihamie Bunju mbali na kadhia za mji, na rahisi kudhibiti kiusalama!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Acheni jazba ni sula la USALAMA tu
Si nimesema Ikulu ihamie mbali na mji kama vile Bunju ili kudhibiti usalama, hata hivyo mambo yakichacha atafuatwa tuu mbona Ghadafi anatafutwa kwao Sirte!!!!!!!!!!!! Hilo la kufunga barabara sio jibu la usalama wake!!!!!!!!!!!!
 
Huu ndio ufisadi wenyewe...kwanini Mwalimu JK Mwinyi hata Mkapa hawakufunga barabara....Watu tunahaha na mahali pa kupita wao wanafanya barabara kama mali binafsi.... Mie naomba huu mjadala usogezwe mbele wahusika waeleze kwanini maana sasa hivi kwa wingi wa magari nadhani kufunga barabara kwa matumizi binafsi ni kuwatesa wananchi
Mwalimu Nyerere jioni alikuwa anatembelea majirani zake Wamakonde wa Msasani, hakuwa na sababu za kuogopa watu!!!!!!!!!
 
Ukiishi vizuri na watu unaowaongoza amani itadumu sana,lakini kama kiongozi anakuwa kama huyu itabidi waweke na waya za shoti kbs sababu maadui watamzunguka kila pahala.Nnasema hakuna aliejuu ya binaadamu mwenzie,wakiamua kukutafuna utafunwa tu hakuna cha jeshi wala kitu gani
 
hii ni kwl kabsa,hvi kwli kwa mwendo huuu atatufikisha kweli?
 
UJIRANI MWEMA WA MIAKA NENDA RUDI NI SIRI YA ULINZI IMARA WA IKULU YETU MAGOGONI KUPITIA ULINZI JAMII KWA HIARI TU

Nakumbuka miaka ileeeee Ikulu yetu hii hii hapa Magogoni ilikua ikilindwa tu na akina yahkhe tu bila hata kubeba kisu mkononi.

... nasema miaka ileee ambapo Ikulu yetu ilikua na heshima kweli kweli na kuonekana jumbani kwa Wa-Tanzania wote, ulinzi wake wala haukua swala la kupangiwa bajeti kamwe. Nasema ile miaka ambayo Ikulu yetu haikuwahi kuhusishwa n tuhuma zozote za mtu yeyote kutumia wadhifa wake biashara zozote zile mle, usalama wa eneo hilo zima ulikua ni jukumu la hiari ya ulinzi toka kwa akina mama wauza samaki ferry, wavuvi, wachoma mahindi na mihogo na kadhalika.

Ndio, kumbukumbu zote zinaonyesha wakazi wote eneo zima lile la Kata ya Kigamboni kwa ujumla na wapangaji wetu hasa wa kwenye jengo letu Magogoni mle waliishi bila tukio lolote la ajabu kwa mtaji huo wa Ulinzi Jamii tena bila gharama kwa miaka hiyo yote.

Lakini miaka hii ya hivi karibuni ambapo nako ningependa niamini kwamba wapangaji wetu wapya wote pale Magogoni nao pia ni watu waadilifu sana tu kama watangulizi wao, kwamba hata siku moja hawahusiki na biashara yoyote inayoendelea kufnyika au kuwahi kufanyika mle, hivi leo wanazidi kutushangaza kadiri siku zinvyoendelea kwamba sasa wanageuka kero za kila aina kwa wakazi wa Kata ya Kigamboni kuibuka na amri hii leo na ile kesho.

Kwanza walianza taratibu tu kwamba hakuna kupaki gari eneo la chuo cha wananchi Magogoni ingawaje watu ni wengi sana pale na vyombo vyao vya moto.

Wakaja na suala la barabara gani kusikatishwe mida gani vile na hivi leo ndio hivo tunasikia hilo la kutolewa amri kwa Waheshimiwa Walipakodi walioijenga ikulu yao na kuendelea kuihudumia kifedha, waliojenga barabara mbalimbali katika eneo hilo kwamba sasa wasipite pale mara wapite kule basi kero tupu!!!!!!!!!!

Sasa mikanganyiko hii, kwa akili tu ya kawaida ya kuzaliwa nayo mtu, inakua vipi mpaka inatupeleka katika kujiuliza kwamba kuna ulazima gani uwepo tu wa jumba linaloitwa ikulu anamoishi Mtanzania mmoja tu kweli igeuke kero na kadhia kwa wananchi wakazi wa eneo la jimbo la Kigamboni ambao wanakaribia kufika idadi ya watu elfu 72??????

Kimsingi Tujuavyo sisi, siku zote ikulu kama taasisi yoyote ya umma inayo jukumu la kutekeleza miradi mbalimbali ya 'Ujirani Mwema' (Social Responsibility) kwa majirani zake wa eneo zima ya kata ya Kigamboni na kata nyinginezo za jirani mpaka watu wenyewe wa eneo hilo wakajihisi kubarikiwa kuwa mkazi jirani wa eneo hilo tofauti na sie wengine wa kule kwa Aziz Ali ambao hatupakani na eneo hilo. Ikulu isingependeza kuonekana laana na kero kwa wakazi wa eneo hilo na wapita njia tu.

Kuna taarifa kwamba miaka hiyo katika orodha ya maswali kwenye usaili Mwalimu Nyerere kukukabidhi uwaziri ni pamoja na kuulizwa jina lake yule kijana wako anayekulindia geti na nyumbani kwao anakotoka. Cha ajabu ni kwamba wengi sana walisikika kufeli mtihani huu na kukosa uwaziri.

Madai ya Mwalimu yasemekana kwamba aliamini kwamba kama mtu hujui hata jina la mtu anayelala nje kulindia usalama wako, mali na familia basi inamaana kwamba kwako wewe humthamini zaidi ya pochi tu unayomkatia kila mwezi hivyo kuna uwezekano pia usiwathamini wananchi wa kawaida pindi tunapokukabidhi jukumu la uwaziri.

Kwa tukio hili la uwepo wa ikulu mahali pale kuonekana kutoendana vema na mtiririko wa kawaida wa kila siku kwa jamii yetu pale, pengine wachambuzi wa mambo wakatamani kujua yafuatayo kuhusina na uwepo wa wapangaji mbalimbali wa jumba letu la Magogoni na tija ya uwepo wake kwa majirani zake; je ni kipindi cha mpangaji yupi (Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, BWM na leo hii Rais Kikwete) kati yao

(1) aliyesaidi kuleta ujirani mwema zaidi na vipi majirani zake wanamzungumzia vipi huko alikokua akiishi kabla ya kuhamia Magogoni?? Majirani wanasemaje juu yao katika vipindi mbali mbali pale Magogoni, kwa makazi ya awali na kule vijijini kwao kabisa??

(2) Ubora wa Elimu na matokeo ya shule za maeneo ya jirani na ikulu ikoje katika vipindi mbalimbali vya wapangaji hawa, je hali kama kama hiyo ikoje katika shule za maeneo ya makazi ya awali kabla ya kuhamia ikulu, na vipi kwa kule vijijini kwao kabisa kwa kila mmoja wao???

(3) Uhusiano binafsi ukoje kati ya waheshimiwa hawa na ujumla wa Wa-Tanzania wasiokua na vyeo, mali wala mjomba wa kumunganishia chochote huko Ikulu????????

(4) Tangu kila mmoja ya wapangaji wetu hao wanne hawa kuukwaa urais wa nchi yetu, hali ya uchumi ikoje eneo jirani na Magogoni, kwa makazi yake ya awali na vipi kijijini kwao kabisa.

Mpaka hapo nawapa changamoto kali Wanabodi JF mtoe jibu sahihi kwa kuleta PICHA HUMU itakayotubainisha kwamba kati ya Ikulu yetu Magogoni njia za kuingia na kutoka Kigamboni, ni ipi iliotangulia kwepo mahali hapo?

NB: Kama vipi Ikulu yetu itangulie kuhamia katika viwanja vyake stahiki Dodoma kama ilivyokwishapangwa viongozi wetu wa huko nyuma au ikishindikana basi bora wakazi wa Kigamboni ndio wahamie huku ili kadhia hako hapo ufukueni usiendelee kuonekana kero kwa Waheshimiwa Walipakodi wenzetu.
 
Watu wa barabara wapo wapi kwa kusababisha usumbufu huu, mhusika ni Magufuri au nani?
 
Labda interejensia wamegundua kuwa wanaharakati watakaoandamana kupinga dowans kulipwa wanataka kupita hapo
 
Back
Top Bottom