Dharura ni kipimo cha uongozi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,780
Na Askofu Bagonza
-------
DHARURA NI KIPIMO CHA UONGOZI

Dunia ina dharura. Taifa letu lina dharura. Tusiulizane nani kasababisha. Haisaidii sasa. Nyumba yetu inawaka moto. Tusihangaike na kuua panya, nyoka, mende na mijusi inayokimbia moto.

Kushughulikia dharura ni kipimo halisi cha uongozi. Kutawala ni kitu kingine. Dharura inataka uongozi. Uwezo wa kumshawishi hata adui wako aamini yuko salama mikononi mwako. Wakati wa raha, viongozi waweza kuwa wengi. Kwenye dharura ndipo tunagundua viongozi halisi hawajai kiganjani.

Haya ni baadhi ya maadili ya kiongozi wakati wa dharura:

1. Asijifanye anajua kila kitu.

2. Aruhusu wataalam wafanye kazi zao. Askofu asisimamie kujenga daraja na Afisa mtendaji Kata asimuagize Askofu namna ya kugawa sakramenti!

3. Asigeuke kuwa dharura kuliko dharura yenyewe.

4. Awe tayari kuongoza kutokea nyuma, mbele, katikati na hata juu. Asigeuke kuwa jiwe la mlango wa kaburi.

5. Atofautishe mambo ya lazima na mambo muhimu.

6. Asubirishe adhabu na zawadi mpaka mwisho wa dharura.

7. Achochee matumaini kuliko hofu. Kama ipo haja ya kuogopa, iwe hofu ya kuogopa dharura kuliko kumwogopa kiongozi.

8. Akikosa busara, awe makini. Akikosa nguvu, awe na akili.

9. Awe tayari kuwa wa kwanza kulaumiwa na wa mwisho kupongezwa.

10. Awe karibu zaidi na wanaopinga mkakati wake kuliko wanaouunga mkono.

Daima kiongozi wakati wa dharura akubali kuwa gunia la kufanyia mazoezi (punching bag), lakini alijaze gunia hilo kwa pamba kuliko mawe. Akilijaza mawe, atatumia raslimali nyingi kutibu majeraha ya wanaompiga.

Mungu wetu ni mkubwa kuliko CORONA VIRUS, tutashinda tukijificha ndani yake.

Jr
 
Kwahiyo unampangia cha kufanya? Unajuaje kuwa hajatoa? Jo si kila mtu anapenda kupayuka majukwaani ili naye aonekane kasema.. Kuna njia nyingi za kufanya mambo
Kama KUB anapaswa kuonyesha uongozi hata kwa kutoa elimu au maono yake kwenye hili janga tunalopambana nalo.

Jr
 
mkuu Mshana Jr huwa nakuelewa sama hoja zako.
bahati mbaya ni kwamba haya ulioandika hapa yana baki hapa hapa,wanopaswa kukuupokea ujumbe huu hawaupokei wala wale waliowazaidizi wao hawawafikishii :mad::mad:
 
Back
Top Bottom