Dharura; Kuna taasisi ya kupeleka wanafunzi chuo inanisumbua

drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
4,664
4,760
Naomba msaada wa haraka kuna taasisi ya kupeleka wanafunzi vyuo nje ya nchi nimempeleka mwanangu India nimelipa pesa yote lakini mwanangu india anasumbuliwa kuwa bado fee yake hajalipwa na ameambiwa hatufanya mtihani na tangu aende india ana wiki tatu.

Kila nikimwambia muhusika mbona fee hujalipa wanamsumbua kijana ananijibu achana nao nitaongea na director mpaka leo kimya hajalipa niende wapi kwa haraka nikapate msaada.
 
Sijui hizo taasisi zinafanyaje kazi. Ina maana hadi ulipaji wa ada unapitia kwao? Yaani haiwezekani kulipa ada chuoni moja kwa moja?
Nadhani kwa wazazi ambao hawafahamu namna ya kutafuta vyuo nje kwa ajili ya watoto wao wapendwa, ifike mahala wazitumie hizi taasisi kupata nafasi vyuoni tu na si zaidi ya hapo!
Anyway, ushauri wangu: Kama hiyo taasisi imefikia hatua ya kupokea ada ya chuo ina maana ina uhusiano wa karibu kabisa na chuo. Hapo mzazi fanya mawasiliano na chuo moja kwa moja na uwapatie uthibitisho wa malipo uliyoyafanya kupitia hiyo taasisi.
 
ada ya chuo india.. unailipia Tanzania kwa account ya wakala... huo ni ujinga..

why mtoto baada ya kufika india asijiridhishe na mfumo wa ada chuo.. kama wahindi wenyeji wanavyolipa.. wewe mzazi ukawa unafanya T T wire transfer direct kwenye account ya chuo
 
naomba msaada wa haraka kuna taasisi ya kupeleka wanafunzi vyuo nje ya nchi nimempeleka mwanangu india nimelipa pesa yote lakini mwanangu india anasumbuliwa kuwa bado fee yake hajalipwa na ameambiwa hatufanya mtihani. na tangu aende india ana wiki tatu. kila nikimwambia muhusika mbona fee hujalipa wanamsumbua kijana ananijibu achana nao nitaongea na director mpaka leo kimya hajalipa niende wapi kwa haraka nikapate msaada
Nakushauri ukae chini utulie na uandike vizuri tatizo lako kwa lugha inayoeleweka vizuri
 
naomba msaada wa haraka kuna taasisi ya kupeleka wanafunzi vyuo nje ya nchi nimempeleka mwanangu india nimelipa pesa yote lakini mwanangu india anasumbuliwa kuwa bado fee yake hajalipwa na ameambiwa hatufanya mtihani. na tangu aende india ana wiki tatu. kila nikimwambia muhusika mbona fee hujalipa wanamsumbua kijana ananijibu achana nao nitaongea na director mpaka leo kimya hajalipa niende wapi kwa haraka nikapate msaada

Waswahili sijui tupoje na ndiyo maana tunadharaulika na kusumbuliwa hivi na wenye Akili. Umeleta Suala hapa ili tukusaidie kukupa Ushauri na cha Kushangaza umeishutumu tu hiyo Taasisi lakini cha Kukera zaidi wala hujaitaja. Sasa unataka tukupa Mawazo yetu kwa Taasisi ambayo hata bado hatujaijua Ndugu? Umeambiwa Sisi ni Wafalme Njozi wa kuweza Kuijua?
 
Watanzania wengi wetu bado tupo kwenye usingizi wa pono, hadi Leo wewe na mwanao mmeshindwa kujua njia muafaka ya kulipia ada KWA chuo husika. Hapo ndipo CCM itaendelea kushinda chaguzi kwa watz wengi bado wapo gizani
 
Hata mimi nimeshindwa kushangaa. Leo 2020 bado tumelala hivi simuelewi mzazi unalipaje ada kwa agent. Dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hela ya manunuzi ya nyumba unamkabidhi dalali pasipo uwepo wa muuzaji halisi na hupewi documents yoyote kuthibitisha umenunua nyumba ila unatoka kwenda kujimwambafy kwa rafiki zako.

Hata Kama Mimi sio tapeli hapo ntakutapeli maana utakua umenishawishi kwa makusudi kabisa nikutapeli chanzo ni uzembe wako kutoa hela kizembe hivo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom