Dharau ya serikali kwa walimu ni kichocheo cha wao kugoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dharau ya serikali kwa walimu ni kichocheo cha wao kugoma

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by simaye, Jun 26, 2012.

 1. simaye

  simaye JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Walimu wa Tanzania wanaweza kuwa ni watumishi pekee duniani kupewa nafasi ya mwisho katika malipo. Wapo baadhi ya watu wanajiaminisha kwamba mgomo wa mwalimu hauna athari yoyote kwa nchi. Nafikiri wenye mawazo ya aina hii wamepotoka sana kwa sababu utendaji usiokidhi viwango wa mwalimu una athari kubwa kwa Taifa kwa vizazi vingi vijavyo. Mwalimu asipotulia na kufanya kazi ya kufundisha kwa kufuata maadili mazuri na hasa anapoonekana kudharauliwa na serikali kwa kupewa mshahara mdogo kama ilivyo sasa atapata muda wapi wa kujianda kwa ajili ya kuandaa watumishi bora wa Taifa hili? Ndio maana leo hii watumishi wengi wanazalishwa na walimu hawana maadili kwa sababu walimu hawana muda wa kuwapika vyema bali wamebaki kufanya kazi kama kutimiza wajibu tu na watanzania tunachekelea na kuwakejeli kwa kila namna.Kwa nini wadau tusiwaunge mkono walimu ili waweze kulipwa vizuri sawa na kada nyingine za utumishi ili kuwapa morali nzuri ya kufanya kazi?
   
Loading...