Dhana ya Wananchi wengi kujua Serikali ni kampuni binafsi inayotoa msaada

wazanaki

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
1,092
804
Wakuu kuna haka kadhana. Kuwa watanzania wengi bado wako kwenye ujinga wa kutoelewa serikali.

Nilikuwa kwenye kijiwe kimoja nasikiliza maongezi nikaona kuna group kubwa la watanzania hawafahamu Serikali na majukumu yake.

Ndio maana mtu ukimuelezea kuhusu kudai katiba anaona kama unagombana na kampuni.

Kwa uelewa huo wa wananchi, inamaanisha sasa kwamba wananchi wanahalalisha kila kitu ambacho kinafanywa na serikali. Na wanajua Serikali hata kama ikikufinya, ina haki kwa sababu inakusaidia.

Kama ukionekana unaipinga wananchi hawa hawa wanaona kama unaikosea Serikali, kwa sababu Serikali inatoa msaada
Mwananchi anashindwa kuelewa kuwa, Serikali ikiwa onezi ni kwamba yeye ndio anayeisaidia
Elimu ya uelewa wa Serikali ni muhimu na inapaswa itolewe katika vipindi vya redio na televisheni ili watu wawe na uelewa.

Otherwise watu wasipoelewa inakuwa ngumu kufikiria suala kwa pamoja

Asante. Narejesha kwa wadau
 
Back
Top Bottom