Dhana ya usajili wa wanasiasa katika siasa za nchi yetu

neno1

Senior Member
Oct 9, 2013
196
141
Kuna dhana iliyojengeka katika siasa zetu za kusajili wanachama hasa wenye majina toka chama kingine. Kibaya zaidi huwa haijalishi taswira aliyokuwa nayo huyo mwanachama kwa jamii alipokuwa upande mwingine.

Tuliona Nape alipokuwa CCM kama katibu mwenezi na baadaye waziri, tulimlalamikia sana kwa kauli zake za kuminya demokrasia. Alienda mbali hadi kujipatia umaarufu kwa kauli yake ya 'bao la mkono'. Na karibuni sheria ya vyombo vya habari. Lakini alipotolewa wale wale wapinzani ndo wakawa sympathisers wake na wengi wakiwa na nia ya kumvuta kuja kwao.

Leo hii Mwigilu ametolewa pamoja na matamko yake yaliyolenga kumlinda kisiasa bila kujali haki za raia, naye wameanza kumfariji na kumtaka upande wao. Hivyo hivyo ilitokea kwa Lowasa wakampa na nafasi mwisho wake tunajua ilivyoishia. Mbaya zaidi sioni vyama hivi vikijifinza

Najiuliza badala ya kusubiri wenzenu waangushe ili nyie muokote, kweli mmeshindwa kuendeleza wanasiasa wenu. Hizi ni siasa mfu ambazo zitawafanya kuendelea kuwa back benchers. Lakini pia kama yale mnalaumu wafanyayo wakiwa upande wa pili ila wakiachwa mnawataka, inaashiria hata nyie mnaunga mkono hayo mambo yao ila tatizo lenu ni kufanyia upande gani.
 
Back
Top Bottom