Dhana ya uhaba wa wanaume: huwaweka baadhi ya wanawake katika mahusiano magumu…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhana ya uhaba wa wanaume: huwaweka baadhi ya wanawake katika mahusiano magumu…!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jul 23, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kuna wakati hutokea wanawake wakateswa sana kwenye uhusiano wao wa kindoa au kimapenzi na bado wakaendelea kukaa tu kwenye uhusiano huo. Inafikia hadi mtu anakufa huku akiona kabisa. Watu wengine huiita hali hii kuwa ni ujinga na wengine huita kulogwa au huelezea hali hii kwa njia ambayo haiwapi haki wanawake hao. Zipo sababu nyingi ambazo zinawafanya wanawake kuendelea kukaa kwenye mahusiano magumu au ndoa ngumu, bila hata kufikiria kuondoka. Sababu nyingine zinaweza kuonekana kama kituko, lakini ndizo zinazowafanya wang'ang'anie uhusiano huo au wafie kwenye uhusiano au ndoa hiyo.
  [​IMG]
  Kuna dhana imejengeke kwa baadhi ya wanawake kwamba wanaume ni wachache au hakuna wanaume wa kuoa. Dhana hii ambayo haina ukweli wowote, imewafanya baadhi ya wanawake kuishi katika mahusiano magumu na wenzi wao wakihofia kutoka au kuachana nao kwa sababu hawatapata mwanaume mwingine. Kuna wanawake wengi sana ambao wanagombea kupendwa, au wanajipendekeza ili wapendwe. Hawa ni wanawake ambao wana kasoro kubwa kwenye mifumo yao ya kufikiri au ufahamu. Unaweza kukuta mwanamke anadhalilishwa, anaoneshwa kwamba hatakiwi, amechokwa, ameshachezewa lakini amemng'ang'ania mwanaume huyo kama luba.

  Wanawake wanaoteswa kwenye uhusiano au ndoa, huwa wanajidanganya kwamba, watamudu siku moja kubadili tabia hiyo a waume zao kuwafuja. Wanajiambia kwamba, kutukanwa, kupigwa, kudhalilishwa, na matendo mengine, kuna siku watamudu kuwasaidia wanaume hao watoke kwenye tabia hizo. Lakini wakati mwingine wanaume hawa watesaji, huwa wanajidai kusema kwamba, wanafanya mambo hayo bila kujua sababu na kuna wakati wanasema wamelogwa.
  [​IMG]

  Hujawahi kuwaona wanawake wanaokwenda kwa waganga kutafuta dawa ili waume zao wasiwapige, ati kwa sababu vipigo vyao vinatokana na kuchanganywa na uchawi wanaofanyiwa na wanawake zao wa nje? Mwanamke anaamini kabisa kwamba, mumewe hamjali na anamdhalilisha kwa sababu ya kulogwa! Mwanamke anaweza kujiambia kwamba, kwa sababu mume wake kuna wakati anamtendea wema, hata kama ni mara moja, basi anampenda na hayo mengine mabaya, yatakwisha au ni bahati mbaya. Mwanamke pia anaweza kufikiri kwamba, akijitahidi sana kumfurahisha mumewe, mume huyo atabadilka na kuwa na tabia nzuri. Hivyo hujipendekeza na mwanaume habadiliki na mateso yanaongezeka.
  [​IMG]
  Kuna wanaomudu kutoka kwenye uhusiano wa aina hiyo, hawa ni wale ambao wanajua nini maana ya kupenda wao hawasukumwi na mihemko, bali husukumwa na kupenda. Kwao msamiati kwamba wanaume ni wachache au hakuna wanaume wa kuoa haupo kabisa akilini mwao..............

   
 2. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nadhani wanawake wengi pia wanalazimika kubaki kwenye mahusiano kwa sababu ya neno..'watu au jamii itanionaje'
  Wakati mwingine makosa yaleyale ambayo yanavunja ndoa endapo yangefanywa na mwanamke yakitendwa na mwanaume jamii inachukulia poa..so, wanawake always wanajikuta wapo kwenye disadvantaged position!
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Najua wanaume wataukimbia huu uzi kwa sababu nimewashika wanawake masikio....................LO

  [​IMG]
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Jul 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  SnowBall nimetafuta kitufe cha LIKE sikioni...................
  Pokea LIKE yangu mkuu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi bana!..hapa napo hukioni?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  mkuu Mtambuzi pia inaonyesha wanaume ndo hasa tunachangia kuvunjika kwa mahusiano.
   
 7. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Kuna swala la jamii itanionaje, lkn pia watoto wataishije na ile kitu famous ya 'mpaka kifo kiwatenganishe'.

  Mengine ni kuamini kuna siku atabadilika, nitaanzaje maisha (uoga na of course nitampata wapi mwingine) na ujinga au kutojithamini sisi wenyewe wanawake!

  Jamii has never been woman friendly hata siku moja. It is a big challenge to be a woman.
   
 8. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Hili ni tatizo la kutojitambua!
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hivi hao wanaosema wanaume wachache wanaishi wapi? Jangwani?
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,029
  Trophy Points: 280
  Tabia ya kutokumuamkua mumeo asubuhi umeianza lini.
   
 11. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Pole yao wenye upendo wa mshumaa kuwamulikia wenzao huku wenyewe unaungua na kuishilizia..personaly kwenye mapenzi hua sifanyi biashara isiyolipa(i mean kama nakupenda, kukujali,kukuheshimu you must do the same to me) unless otherwise kila mtu aende na njia yake hua sina muda wa kuvumilia mateso aisee..mapenzi sio mateso bali furaha na ukiona kwenye uhusiano wako karaha ni nyingi kuliko raha ujue unapoteza tu muda wako,huwezi kubadilisha tabia ya mtu ukubwani..
   
 12. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  akili ni nywele. kama unaishi na mwanaume kisa unahofia 'jamii na watu watakuchukuliaje' basi una matatizo makubwa zaidi ya hayo. badilisha mindset yako wadada mnafikiaje hatua hii??
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Jul 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Yote ya yote mke/mume mwema hutoka kwa MUNGU
   
 14. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  [MENTION]BADILI TABIA [/MENTION]nikweli wanaume ni wachache shauri yako!
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  oooh pole baby hubby wangu, umeamkaje? natamani game tena....nitapata cha chapchap?   
 16. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hili neno ndio mpango mzima kwa mwanamke. Only a woman can understand this! :A S-cry:
   
 17. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Uzi wako umenikumbusha sura za watu tofauti niliokutana nao katika maisha wengine ni wa karibu yangu kabisa. Wanaishi katika ndoa hizi wakitegemea kuwa kuna siku mwanaume huyo atabadilika and roughly is about 10 yrs and this person has never changed.

  Jamii ni mojawapo ya mwanamke kudhalilika, pili ni kufikiria watoto hasa wakiwa wadogo hakuna mama anayetaka watoto wake wabeheneke ndio maana utakuta mtu anavumilia mateso yake yote kwa ajili ya watoto. Mbaya zaidi ikiwa mama mwenyewe si mwajiriwa au hana namna ya kuwa independent.

  Mtambuzi , mimi naona kama tu umegusia hili tatizo lakini hebu tupe ushauri zaidi vipi mwanamke akabiliane na challenges kama hizi. Ikiwemo huo uhaba wa vidume....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh kwa kweli nawasikitikia sana wanawake wenye tabia za kuamnini kuwa wanaume ni wachache so lazima ang`ang`anie janaume hata kama ni likatiri, halimpendi na linamtesa.

  Heri wanawake wenye kuthubutu na kusema yatosha.lol!
   
 19. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe Kaunga kuwa jamii haiko woman friendly lakini specifically kwa mazingira ya Kiafrika. Kwa jamii ya wazungu suala la haki limesimama dede na ni jamii chache sana zenye mtazamo unaofanana na wa kwetu.

  Lakini hapa kunaishu ya dhana ya wanaume kuwa wachache ambayo Mtambuzi umeizungumza. Dhana hii ina ukweli kwa sehemu na imewatesa sana wadada hasa wale ambao hawajabahatika kupata exposure ya elimu na kutambua haki zao.
   
 20. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Sure na mfume baba ulioko kwenye jamii zetu basi mwanamke ni wakudharauliwa kuteswa, kupigwa na kuzingiziwa mabaya yote.lol!
   
Loading...