wimbi la mbele
JF-Expert Member
- Jan 4, 2011
- 647
- 266
GREAT THINKERS. Naamimi sisi ni watu ambao tunaupeo mkubwa kuliko vyombo vya habari vilivyojaa proganda na waandishi uchwara ambao hawapendi kuuliza maswali wala kuwa na ma critical thinkers.
Nadhani siko peke yangu ninaliyechoshwa na upuuzi na propaganda toka wa wanasiasa wetu wa CC, CHADEMA na vyama vyote vya siasa kuwa serikali haina dini lakini raia wake wanazo dini.
Dhana hiyo ni maarufu Tanzania. Mara nyingi katika masuala yahusuyo dini, viongozi wa serikali husikika wakisema «serikali haina dini, ila wananchi wake wana dini zao
Hoja ya usekula wa serikali ni ya kihistoria. Ilijengwa kiasi cha miaka miambili iliyopita ikitaka serikali ijiepushe na shughuli za kidini hususan katika masuala ya elimu, mafundisho ya maadili na na ibada.
Japokuwa Tanzania imekuwa ikidai kwamba serikali yake ni ya kisekula, hali halisi haioneshi hivyo. Pamoja na madai hayo, serikali ya Tanzania imewahi kuingia katika msuguano na Waislamu na baadhi ya wasiokuwa waislamu pale Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipotaka kuanzisha somo la dini au maadili ya nchi. Kadhia hii ni maarufu kwa jina la dini mseto. serikali ya kisekula haiwezi ikaja na mipango ya kusomesha dini kwa jina lolote lile liwe la maadili au vyovyote vile.
Mifano mingine inayotia wasiwasi usekula wa serikali ya Tanzania ni hii ifuatayo:
1. Wimbo wa Taifa unaomba mungu aibariki nchi
2. Dua ya Bungeni ina muomba mungu
3. Idara za serikali kutenga mabilionioni kwa ajili ya sherehe za kidini
3. Kuapishwa kwa wanaochukua nafasi za uongozi. Japo wanaoapa huapa kwa dini zao, aneapisha si kiongozi wa dini husika bali wa serikali au wa bunge.
Utaratibu huo hauendani na madai kuwa nchi au serikali ya Tanzania haina dini, bali wananchi wake ndiyo wenye dini.
Swali ni je, tunapomtaja Mungu katika wimbo wa taifa
au katika dua ya bungeni, na kadhalika, tunamkusudia mungu yupi?
1.Mungu wa Waislamu?
2.Wa Wakristo?
3.Wa dini za asili?
Je, kuna mungu wa kitaifa? Mungu huyo wa kitaifa ni yupi na ni wa dini gani?
Je, katika hali hiyo, ni kweli serikali haina dini?
Hivi kwa nini hawa wanasiasa wa CCM, CHADEMA na vyama vingine wanapenda kutufanya sisi wajinga?