Dhana ya njama (Conspiracy theory) na mauaji ya Polisi wanne

Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
1,143
Nadharia ya njama (Conspiracy theory) ni nadharia inayotumika kuelezea hasa hasa matukio mabaya yaliyopangwa.

1. Conspiracy theory: a belief that some covert but influential organization is responsible for a circumstance or event (Oxford Dictionaries).

2. Conspiracy a theory: Explains an event or set of circumstances as the result of a secret plot by usually powerful conspirators (Dictionary and Thesaurus | Merriam-Webster)

Mara nyingi dhana hii inatumika katika siasa na inahusisha matukio makubwa makubwa. Kwa mfano kupigwa na kuangushwa kwa Word Trade Center, Marekani huelezewa na baadhi ya watu kwa dhana hii ya Conspiracy. Inatumika katika matukio ambayo yanatia shaka na kuna-lead fulani ya mashaka hayo. Hapa Tanzania kuna vifo vya wanasiasa ambavyo vimehusishwa na dhana hii. Mfano ni mauaji ya Soweto Arusha, Mauaji ya Igunga na kifo Cha Wangwe aliyekuwa Chadema.

Mauaji ya polisi wanne yanakidhi kuelezezwa kwa dhana ya njama kwa sababu ya uharaka wa Polisi kusema kuwa yanauhusiano na UKUTA, bila hata kujipa muda wa kutosha kuchunguza. Vilevile kuna mwanasiasa ambaye mara nyingi amekuwa akihusishwa na matukio ya Conspiracy. Na kwa kweli huwezi kuzuia watu kuwa na dhana hii kwa sababu Mungu amempatia mwanadamu akili ya utashi ikiwemo kufikiri kwa uhuru. Hivyo hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kuzuia alichokianzisha Muumba wetu.
 
Mhhhh!!

Ina maana wametolewa kafara ama .....................!!? Sometimes ni coincidence tu!! Sasa wanatake advantage!!
Ni vigumu kutake advantage kwa mauaji mabaya hivyo. Mtu au taasisi inayo-take advantage tukio kama hilo hapana shaka wanakidhi kuelezwa kwa dhana hii. Unawezaje haraka haraka hujafanya uchunguzi unakimbilia kusema kuwa sababu ya mauaji ni UKUTA, kama hukupanga njama kufanya tukio? Wamefanya uchunguzi lini hadi kuhitimisha kwamba sababu ni UKUTA?
 
Incidence za matukio ya polisi kuuawa zilikua even more during the 4th presidential session. Ku blame ukuta kwenye tukio hili inaweza ni wrong diagnosis na kuchanganyikiwa kwa polisi Kumbuka wrong diagnosis leads to progression of the problem. Hata kama polis wanachukia upinzani ningewasihi kwenye ili suala wa avoid kuingiza siasa kwani hawatofikia kiini cha tatizo
 
Naomba tujadili kwa uhuru bila mihemko
Hayo mauaji naona yamefanywa na kile kikundi kilichovamia tena kituo cha polisi. Hawa sio majambazi bali ni kikundi cha watu wenye mlengo fulani wa dini. Tatizo ni kwamba polisi walijisahau wakaona kama wameshakimaliza hiki kikundi na nguvu zao wakaelekeza kwenye siasa badala ya kufanya kazi yao. Na mwisho ni ujinga uliotukuka polisi kutumia mauaji kama haya kulaumu watu ambao hawahusiki. Je, wanakumbuka yule mtoto aliyekuwa anapiga uongo kelele kama amevamiwa na chui? Hao waliyotoa wazo la kuwaunganisha UKUTA kweli wana akili ndogo!
 
Ni vigumu kutake advantage kwa mauaji mabaya hivyo. Mtu au taasisi inayo-take advantage tukio kama hilo hapana shaka wanakidhi kuelezwa kwa dhana hii. Unawezaje haraka haraka hujafanya uchunguzi unakimbilia kusema kuwa sababu ya mauaji ni UKUTA, kama hukupanga njama kufanya tukio? Wamefanya uchunguzi lini hadi kuhitimisha kwamba sababu ni UKUTA?
Huyo aliyetamka kusingizia UKUTA Uongo inabidi ashitakiwe kwa sababu anafanya kazi kwa kutaka kumfurahisha Mkuu wake hafanyi kazi Kama mtaalam wa uchunguzi .
 
Unakumbuka Mhe Mbowe aliporushiwa bomu kule Arusha na baadaye risasi kumiminwa katikati ya watu hadi watano wakapoteza maisha, harakaharaka Polisi walisema ni Chadema wenyewe waliuana. Hawakujali kuwa siku moja nyuma mkubwa mmoja kwenye Kampeni za CCM aliwatahadharisha watu wasiende kwenye mkutano wa Chadema.
 
Back
Top Bottom