Dhana ya mwendokasi kama sababu ya ajali hasa za barabarani inafaa ibadilike

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,700
1,721
Wakati fulani nilikuwa semina Morogoro na pana mtoa mada mmoja toka India akasema mwendokasi sio sababu ya chombo cha usafiri kupata ajali. Huwa pana sababu nyingine tuu inayosababisha kupata ajali.

Wakuu, nimetafakari mno baada ya kutokea ajali ya barabarani hivi majuzi mkoani Singida ya mabasi mawili ya kampuni moja ya City Boy. Pana wengine walisikika wakisema ni mwendo kasi ilihali ni uzembe dhahili wa madereva katika kuoneshana mbwembwe.

Tukubali tusikubali spidi ya chombo cha usafiri iliyowekwa ni salama hasa kwa wanaokitumia kama wanakuwa makini. Mfano, tabia tuliyokuwa nayo ya kukata alama za barabarani makusudi hii ni ishara dhahiri ya kupata ajali.

Tujiulize angani ni nadra sana ndege kugongana na ndo hakuna ishara yoyote kule lakini ndege hupata ajali na hawakimbii kwenye mwendo kasi kama sie tunavofanya.

CmkdoV3UIAEQREp.jpg

IMG_20160709_074057_0.jpg IMG_20160623_083244_0.jpg IMG_20160708_075004_0.jpg IMG_20160708_075153_0.jpg
 
Uko sahihi sana. Hii nina ushahidi nayo. Kuna mtu kaendesha gari for more than 30 years lakini hajawahi kupata ajali aina yoyote. Hapa tunatakiwa tuwe wakweli tu. Chanzo cha ajali kikubwa ni uangalifu. Si miundo mbinu kama tunavyosingizia. Ni uzembe kwa asilimia mia. Kama mtu anaweza kulazimisha kulipita gari lingine kwenye kona huo ni uzembe. Kama mtu anaendesha gari lenye matairi hafifu huo ni uzembe nk. Hapa kwetu tumeenda mbele zaidi. Watu wanaambiwa long trip wawe madereva wawili lakini halifanyiki. Wanawadanganya matrafiki wakitoka stand na wakifika hapo mbele mmoja anashuka. Kingine, hata asiposhuka bado hapumziki. Huyo wa pili alitakiwa akae sehemu kwa mabasi ya Dar Mwanza awe Singida na basi limkute hapo. Mbeya akae hata Iringa au popote halfway basi limkute hapo. Ukichukulia ajali zote za basi hapa majuzi ni uzembe plus kwa kweli. Huyu anaendeaha usiku akiwa mbio bila kujali anaona umbali gani na kama kungekuwa na kitu mbele angeweza kusimama au la. Huo ni uchovu. Dereva akichoka huwa anawaza deatination zaidi so uangalifu hupungua sana au hata kuisha. Hawa wengine wanabadilishana lane wakati wa kupishana. Hata hawa ukichunguza zaidi unaweza kukuta ni fatigue kwa mmoja wao yaani siku hiyo alichoka na hakutaka tena huo mchezo. Hapa cha kulaumu ni waendeshaji zaidi.
 
Mkuu, kwa kweli inakera kusikia pengine abiria aliyekuwa ndani ya chombo kilichopata ajali akipayuka eti dereva alikuwa mwendo kasi!!!!!! Angalia barabara zetu jinsi zinavohujumiwa na wafanyibiashara wa vyuma chakavu, hili halisemwi asilan! Tubadilike tumuone atakae sema mwendo kasi basi tumuone kama anaota vile.
 
Barabara zetu nyingi nyembamba. Pia nje ya barabara kuna mitaro ya ajabuajabu au korongo. Ukitoka tu nje kwa bahati mbaya hurudi tena barabarani au haupati nafasi ya kusimamisha gari. Yaani unapinduka kutokana na korongo lililopo ukingoni mwa barabara.
Pamoja na wembamba wa hizo barabara mkuu, wataalamu wametuwekea ishara za mwendo 'spead limit' ila ishara hizo zinakatwa bila hatua stahiki kuchukuliwa dhidi ya wahujumu maisha ya watumiaji wa barabara, sikiliza inapotokea ajali, wanakimbilia MWENDO KASI tu!
 
Kuna gari Tanzania hii zinakimbia 160+ KPH kwenye barabara hizo?

Labda gari za magazeti!
Mkuu, bado nasisitiza 'speed meter' kwenye chombo cha usafiri kilichowekwa ni salama kabisa. Sasa kumbe barabara zetu ndio tatizo kwanini hatulitatui?
 
Back
Top Bottom