Dhana ya Mokrie Dela 'wet affairs' na yanayoendelea nchini

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
kwa mara ya kwanza nilitambua uwepo wa dhana hii baada ya kusoma riwaya mbalimbali zinazohusu mambo ya kijasusi yaliyorandana na vita baridi kati ya mataifa ya magharibi na dola ya USSR.mimi nilichukulia ni riwaya kama zilivyo riwaya nyingine mpaka hivi majuzi nilipoamua kufuatilia zaidi.
Dhana hii ilikuwa ikitumiwa na shirika la ujasusi la KGB Chini ya kitengo maalumu ndani ya KGB.
Inasemekana hiki kitengo maalum kilichojulikana kama kitengo V kilihusika na utekaji,utesaji na hatimaye mauaji ya kikatili dhidi ya wote walioonekana kwenda kinyume na Dola la ussr.pia KGB ilitumia kitengo hiki kuharibu miradi au majengo mbalimbali ya maadui wao.

Inasemekana kitengo hiki kiliwatumia watu waliokosa maadili katika jamii kama vile majambazi sugu,mafirauni,wabakaji n.k ambao vinginevyo wangekua wako vifungoni au wamenyongwa.
Haya yalitokea kati ya miaka ya 60 na 70.

Leo hii hapa nchini kuna visa kadhaa vimewahi kutokea na kuhusishwa na mkono wa serikali au TISS.
Nimeshindwa kujiunga na kundi linaloamini kuwa mauaji,utekaji,kuchoma moto makanisa ni kazi ya TISS ndio maana naleta hoja hii tuijadili kwa kina.

Mifano ya matukio tata yanavyoweza kuhusishwa na dhana hii ya 'wet affairs'

kifo cha sokoine
kifo cha kombe
kifo cha kolimba
kifo cha chifupa
kifo cha wangwe
kifo cha mwaikusa
kifo cha balali
kifo cha mwenyekiti chadema USA RIVER
kifo cha mkuu wa wilaya(sikumbiki jina la wilaya)
ugonjwa wa mwandosya
ugonjwa wa mwakyembe
Kuchomwa moto makanisa
kuteswa kwa Dr ulimboka
vitisho kwa mnyika,slaa,lema.

Je ni kweli Nchi yetu imerudi miaka hiyo ya sitini?kwa nini wanaoathirika ni watanzania wenyewe?je inawezekana ni mkono wa nchi jirani ?
Maswali ni mengi,tuanze kujadili kwanza.

Naomba kuwasilisha...
 
Ni dhana ya kufikirika imeijengwa kwenye malalamiko ya kisiasa kuliko kazi ya mikono ya vyombo vya dola
 
Ni ushushushu wa kizamaani waliotumia mashushushu mbumbumbu! You cant groom a div 0 tobe an intelligency ofc!
ni kweli kuwa huu ni ushushu wa kizamani ,je Tanzania imeamua kutumia mbinu hizi za kizamani?kuna wataalamu wa mambo ya kijasusi wanaamini unaweza kufanikiwa sana utakapotumia old school techniques katika kipindi hiki cha technology ya hali ya juu kwa sababu watu wamesahau.
 
Baba akiwa zuzu, lazima azae mitoto mizuzu, na akiwepo mwenye akili ujue ni bahati mbaya.
Tumuombee Ulimboka apone haraka. Baba yetu atatumaliza wanawe kwa mateso ya Sobibo
 
Dr ulimboka atapona lakini kama ilivyotokea kwa mwakyembe na mwandosya atakaa kimya!lakini kama watanzania ni lazima tujiulize je serokali yetu inatumia dhana hii?
 
kwa mara ya kwanza nilitambua uwepo wa dhana hii baada ya kusoma riwaya mbalimbali zinazohusu mambo ya kijasusi yaliyorandana na vita baridi kati ya mataifa ya magharibi na dola ya USSR.mimi nilichukulia ni riwaya kama zilivyo riwaya nyingine mpaka hivi majuzi nilipoamua kufuatilia zaidi.
Dhana hii ilikuwa ikitumiwa na shirika la ujasusi la KGB Chini ya kitengo maalumu ndani ya KGB.
Inasemekana hiki kitengo maalum kilichojulikana kama kitengo V kilihusika na utekaji,utesaji na hatimaye mauaji ya kikatili dhidi ya wote walioonekana kwenda kinyume na Dola la ussr.pia KGB ilitumia kitengo hiki kuharibu miradi au majengo mbalimbali ya maadui wao.

Inasemekana kitengo hiki kiliwatumia watu waliokosa maadili katika jamii kama vile majambazi sugu,mafirauni,wabakaji n.k ambao vinginevyo wangekua wako vifungoni au wamenyongwa.
Haya yalitokea kati ya miaka ya 60 na 70.

Leo hii hapa nchini kuna visa kadhaa vimewahi kutokea na kuhusishwa na mkono wa serikali au TISS.
Nimeshindwa kujiunga na kundi linaloamini kuwa mauaji,utekaji,kuchoma moto makanisa ni kazi ya TISS ndio maana naleta hoja hii tuijadili kwa kina.

Mifano ya matukio tata yanavyoweza kuhusishwa na dhana hii ya 'wet affairs'

kifo cha sokoine
kifo cha kombe
kifo cha kolimba
kifo cha chifupa
kifo cha wangwe
kifo cha mwaikusa
kifo cha balali
kifo cha mwenyekiti chadema USA RIVER
kifo cha mkuu wa wilaya(sikumbiki jina la wilaya)
ugonjwa wa mwandosya
ugonjwa wa mwakyembe
Kuchomwa moto makanisa
kuteswa kwa Dr ulimboka
vitisho kwa mnyika,slaa,lema.

Je ni kweli Nchi yetu imerudi miaka hiyo ya sitini?kwa nini wanaoathirika ni watanzania wenyewe?je inawezekana ni mkono wa nchi jirani ?
Maswali ni mengi,tuanze kujadili kwanza.

Naomba kuwasilisha...
Ulichokileta hapa ni "hearsay" na mbaya zaidi hakuna ukweli wowote. KGB siyo hiyo ulvyoifafanua na hata " mokrie dela" siyo namba V.
 
Back
Top Bottom