Uchaguzi 2020 Dhana ya "mkono mtupu haulambwi" yaendelea kuonekana katika kura za maoni

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
DHANA YA "MKONO MTUPU HAULAMBWI" YAENDELEA KUONEKANA KATIKA KURA ZA MAONI.

Leo 20:45pm 21/07/2020

Nimeamini aliyevaa kiatu ndie mwenye kujua kiatu kinabana wapi,nimeshiriki katika kura za maoni juzi nikiwa na mapenzi tu ya Jimbo langu la Morogoro kichwani nikijua sasa naenda kuwaeleza wana Morogoro kinachowasibu hadi Mkoa wa Morogoro unadumaa kiuchumi,na wakinielewa basi wanipe kura,cha ajabu nimepata kura 1.

Nilianza kujinadi kwa kuwashukuru wajumbe wote wa mkutano kwa kunilea nikiwa mdogo,sisi tuliozaliwa miaka ya 1980 tulilelewa na kila mtu mtaani enzi za Ujamaa,ni fahari na heshima kuwashukuru,nimesoma na kukulia Morogoro niliwaambia sasa nina kazi na nitawalea,

Licha ya kuwashukuru nikawaambia matatizo ya Morogoro ni Ajira na mzunguko duni wa fedha,Ndio maana hivi leo watoto wote wa Morogoro wanafanya kazi Dar es Salaam na wamelowea uko tatizo likiwa Viwanda vinavyotoa ajira Morogoro vimekufa,vilibinafsishwa na aliyenunua kaviua ndiye Mbunge wa mioyo yao.

Nikawaambia kura yenu ni hatma ya watoto na wajukuu zenu,kesho watamaliza Shule watakosa ajira,ni vyema wakaonyesha kwa vitendo kumkataa aliyeua Viwanda na kumchagua mtu mwingine Mzalendo ili ajenge msingi wa kuanzisha Viwanda vipya,kwa ajili ya ajira kwa watoto,wajukuu na kizazi kijacho,

Niliwaambia kwa miaka mingi Morogoro ni kama kidonda kilichokosa dawa,naomba mnipe kura nikawe dawa,kweli niliongea kwa uchungu na watu walinyamaza na kuniangalia tu,sikujua walikuwa wanawaza nini,hadi mwisho nilipopata kura moja ndio nilijua kuwa wajumbe walikuwa wananionea huruma tu wao tayari walikuwa wakijua nini wanakwenda kufanya,

Asikwambie mtu wajumbe wanaopiga kura wenyewe hawajui cha huyu ni Mzalendo anatuambia kitu cha maana tumpe kura atusaidie kuiponya Morogoro ndipo nilipojua mkono mtupu haulambwi,uwezi amini kuna wajumbe wengine hawajui kama kuna mtu anaitwa Magufuli wala Majaliwa nikimaanisha zama za Wito na Uzalendo na si pesa ndio uwe kiongozi katika hii nchi,wao wapo kulamba mkono wako tu.

Niliulizwa na baadhi ya wajumbe "Mjomba mbona hujatutembelea" nikawaambia nilijua tunakutana hapa ukumbini na kufahamiana wakati wa kujieleza,cv yangu ipo kwenye form,mnanifahamu mimi kijana wenu nimekulia kichangani,na screening nimefanyiwa,wakaniambia Mjomba ungezungukia wajumbe wote,nikagundua ili ushinde kura za maoni lazima uzunguke wakulambe mkono,ni lazima uwe na hela na uwape wale viongozi wao kisha wao ndio watawapa hela watu wao,

-Tathmini yangu,live kabisa.

Matokeo ya kura za maoni maeneo mengi hasa Morogoro yameonyesha kuwa harakati za Rais Magufuli za Chama kuwa cha Wakulima na Wafanyakazi bado hazijafika wilayani,kata na matawini,ndio maana Katibu Mwenezi atapanda Jukwaani na kusema "mnaniona Mimi,Mimi nalelewa na Wazee wa Morogoro,mimi nakula vizuri,

Hili ni gamba la ile CCM ya zamani kwa maana ya mkono mtupu haulambwi,mwenye pesa ndio atawatunza na kuwalea kwa hiyo Wazalendo wa kweli hatuna nafasi kuleta mabadiliko na mawazo mbadala kwa ajili ya kuleta chachu ya Maendeleo Mkoani Morogoro,naungana na Mwenyekiti kukata kila aliyepata kura nyingi kwa pesa na bahati nzuri wanajulikana hata kwa historia zao za nyuma,japo historia za nyuma haziwezi kumfunga mtu.

Matumaini pekee ya kuibadilisha CCM ya Wilayani,Kata na tawi na kuwa ccm mpya itakayoendelea kujali maslahi ya nchi kama enzi za Mwalimu Julius Nyerere na Wakati huu wa Rais John Magufuli yamebakia mikononi mwake Rais na Mwenyekiti John Magufuli mwenyewe.

Kinyume na hapo matokeo ya ubunge na udiwani maeneo mengi yakibakia kama yalivyotoka kwenye kura za maoni kwa maana ya wa kwanza ndio wa kwanza kweli hadi wakati wa uchaguzi mkuu basi CCM itabakia na sura ileile na matendo yaleyale hatari kwa uhai wa CCM ya baada ya Mwalimu Julius Nyerere na kabla ya Rais John Magufuli.

-Hatma ya CCM

Kama ccm itarudi kulekule kwenye Azimio la Zanzibar yaani CCM ya wafanyabiashara baada ya Rais John Magufuli kuondoka,hali hii itasababisha kuibuka kwa makundi makubwa mawili ndani ya CCM kwa maana ya CCM mpya safi ya watu wenye mtazamo wa Mwalimu Julius Nyerere na Rais John Magufuli,

Kundi lingine likiwa la ile CCM chukua chako mapema iliyokuja baada ya Mwalimu Julius Nyerere na kabla ya Rais John Magufuli na kudumu kwa miaka 30 ikitapanya rasilimali za nchi yetu hadi ikawaudhi wananchi kiasi cha kuwa tayari hata kuchagua jiwe badala ya CCM,tujihadhari na kurudi huku.

Matendo yale baada ya Azimio la Zanzibar ya Wafanyabiashara kuhodhi Madaraka ndani ya CCM na Serikali ni hatari kwa uhai wa chama na Taifa.

Nimalizie kwa kijembe iki nilichopigwa na mjumbe mmoja pengine ndiye aliyenipa kura moja,"Umeifanyia nini Morogoro wewe,

Sikutegemea mtu kama wewe unaejitambua kwa kiasi kikubwa kujipeleka tu hujawahi hata kukutana na wajumbe wa mkutano mkuu wa kata unaenda tu kwa vile unafikiri ukiongea kwa dakika moja utaweza kupindua meza ya mbunge mwenye mabus anayetoaga kwenda kuzikia,uwaconvince watu wakuchague"

Tatizo wengi mliokuja kuchukua fomu mnawaza kama wagombea na sio kama wapiga kura,wapiga kura ni wajumbe,wengi la saba,hawana mshahara wao uchaguzi ndio mavuno yao,wewe unakuja,umeongea kitu kimewachoma hadi ukumbi ukanyamaza lakini mwisho ukaambulia kura 1"

Kwa maisha hayo ya kutaka kula bila kuliwa uliyochagua uwezi kushinda kura za maoni ila endelea kuishi maisha ya furaha sana,usiwe kinyongo aisee,Hongera pia huna hasira ni mtu wa kucheka na kuchukulia powa kila jambo, wenye kuyaweza maisha hayo Ni wale tu wanaoamwamini Mungu,Mungu akubariki na karibu Morogoro.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Pole Sana mkuu, sizani Kama hao wajumbe Kama watakua wamelilipwa na chama kwa ajili ya kuja kupiga kura. Kama walilipwa halafu wanampigia mtu aliyewahonga pesa nyingine hiyo sio poa kabisa, Ila Kama hawakulipwa na chama kwa ajili ya kuhudhulia hapo wapo sahihi kumpigia aliyewapa pesa.

Maana hata mimi siwezi kuacha shughuli zangu za kuniingizia kipato kisha nije kupiga kupiga kura bure bure hapana aisee.
Maana hata nyie mkipata uongozi huwa mnatabia ya kusahau mlioyosema .

Bora tu hako kautaratibu kaendelee aisee.

Hayo ni maoni yangu mkuu

Pole sana
 
Pole sana mkuu,

Ila ujifunze kitu kimoja, será zako ni kama vile kumtongoza Wema Sepetu kwa kumwambia nakupenda, hilo neno keshatamkiwa mara milioni na vudúme mbalimbali so halitokuwa na mtikisiko wala mshtuko ktk masikio yake!!

Será zako tamu tamu hawajaanza kuzisikia kwako zishatamkwa mara mía na wagombea mbalimbali waliopita miaka dahali so ulipaswa ujiongeze baba
 
Morogoro sio wajinga wanathamini vya kwao na wapo tayari kuvilind vilivyo vyao...Abood kazaliwa Morogoro na still bado anaishi Morogoro kwahyo anazijua shida za Moro nje ndani..wewe umeukimbia mji ajabu zaidi hata tawi lako LA ccm lipo kimara baruti(Dar).. umeshindwa kusoma alama za nyakati na nahisi huwajui watu wa Morogoro...Morogoro sio kama maeneo mengine huwezi kuwa mbunge wa Moro kama hujawahi kuishi hapo Mbunge lazima uwe mkazi wa Morogoro ndio watakuchagua.. vinginevyo ukiwaletea historian ulizokalilishwa km ww ukivyokuwa watakubwaga tu
 
Kaka Umeongea kwa uchungu Mkubwa sana na Umewakilisha kilio cha Watu Wengi kwa tathmini ya haraka CCM ina wenyewe ndio Hao Wamerudi tena kwa kura nyingi Prof Kapuya,Magreth Sitta,Jerry Slaa,Mama Salma Kikwete,Ridhwan,Mtemvu nk Nilitegemea kuhesabu kura kwa uwazi ingewabeba Vijana lakini imekuwa tofauti nadhani hata Mwenyekiti hatapenda japo ndio Wameshinda wengi sana yaani Tumepatikana Watanzania Vijana Wameshinda wachache sana
 
Mtoa mada nmekusoma na nmekueleea zaidi kiundani, ila nmegundua nyie ndo wale vijana ambao mmekurupuka bila kuelewa aina ya Platform unayoipitia kugombea. Labda nkuulize tu kwanini wakati wa uchaguzi ndo money circulation inakua kubwa kitaani, ukijibu kwa uelewa utaelewa upo katika boti gani. Kwa ccm hakunaga uchaguzi uliofanyika ambao haukushirikisha rushwa kuanzia uchaguzi wa nyumba kumi hadi ule mkubwa. Ushauri wangu kwa vile umesema umesomea mambo ya research, jaribu kuchunguza kwann wananchi hawakipendi ccm na je mnafanyaje muwe mioyoni mwa watu
 
Mtoa mada japo unayo hoja, kwa elimu yako bado unao mchango wa kuwaendeleza watu wa Morogoro, hata bila kuwa mbunge, usishangae one day ubunge utakufuata hata bila ww kujua! Ebu tuacheni hii dhana kwamba ili kusaidia watu wa jimbo lako, ni lazima uwe mbunge?hii si kweli, timiza wajibu wako hapo ulipo bandugu
 
Asante kwa uchambuzi makini ni kweli mkono mtupu siku zote haulambwi CCM imekuwa chama cha matajiri kama huna nguvu ya fedha basi wewe piga debe kwa wengine wajumbe tatizo njaa ndio maana wakati unajinadi walikusikiliza tuu...i have confidence in you let this storm clear path for you...Godspeed comrade
 
Maelezo yanaonyesha kuwa ulienda kugombea lakini hata wapiga kura hawakujui. Yaani muda mwingi upo Dar na ishu zako ila umeenda siku ya uchaguzi wa kura za maoni. Sasa hapo wajumbe watakuchagua? Kama ishu ni rushwa na unadai kuna mazingira ya watu kutoa rushwa kwa nini hukutoa taarifa Pccb?
 
Morogoro sio wajinga wanathamini vya kwao na wapo tayari kuvilind vilivyo vyao...Abood kazaliwa Morogoro na still bado anaishi Morogoro kwahyo anazijua shida za Moro nje ndani..wewe umeukimbia mji ajabu zaidi hata tawi lako LA ccm lipo kimara baruti(Dar).. umeshindwa kusoma alama za nyakati na nahisi huwajui watu wa Morogoro...Morogoro sio kama maeneo mengine huwezi kuwa mbunge wa Moro kama hujawahi kuishi hapo Mbunge lazima uwe mkazi wa Morogoro ndio watakuchagua.. vinginevyo ukiwaletea historian ulizokalilishwa km ww ukivyokuwa watakubwaga tu
Kuna mtu aliwahi kusema " ujinga ni kurudia kile kile na kutegemea mabadiliko ".

Amandla...
 
Kuna rafiki yangu nae kapigwa chini na yeye anakuja na arguments kama zako. Sijui kwako ila kwa yeye siku ile ya mchujo ndio ilikua mara yake ya kwanza kukutana na wajumbe, imagine wajumbe hawakujui halafu una dakika 1 au 3 tu za kujitambulisha na kuongea na wapiga kura sidhani kama chance ya kumshinda mtu anaokutana nao kila siku unayo unless wawe wamechoka sana na sio lazima awe amewahonga they chose him/her sababu wanamjua.

Ambacho nilimshauri na wewe pia kinaweza kukufaa pia tengeneza mtaji wako wa kisiasa ndani ya chama na kijamii taratibu ila ukijitokeza siku ya kuchukua fomu tu utaonekana ni msaka tonge hata uwe na malengo mazuri kiasi gani.
 
Kwa taarifa yako Magu anachokitengeneza sasa kama hakitazuiwa kitakuja kuliingiza taifa kwenye giza la kuzimu.

Amewafundisha viongozi wa baadae kuwa ukitaka kula bila kupigiwa kelele na vyombo vya habari, wapinzani na wanaharakati basi zuia uhuru wao, wasiandike mabaya yako bali wakusifie mchana na usiku.

Ukitaka kuiba na watu wasijue lolote basi minya uhuru wao, usifanye kama akina Mkwere na mzee wa ukata ambapo ukila kidogo tu kelele zinatoka kila kona.

Wale hawakujua mbinu nzuri ya kupiga na bado ukasifiwa na kuonekana mkombozi wa nchi.

Huyu anatengeneza precedence ambayo tutakuja kujuta mbele ya safari.
 
Back
Top Bottom