Dhana ya kutochanganya siasa na kanisa na madai ya Askofu Emmaus Mwamakula juu ya mchakato wa Katiba Mpya

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za wakati huu JamiiForums.

Kwanza kabisa ninaomba ieleweke kwa kila mmoja wetu ya kwamba, Tanzania ililazimika kupigana vita ya Kagera mwaka 1978 kwa lengo la kuikomboa ardhi yetu na kumtoa nduli Idd Amin Dada na genge la wahuni wenzie.

Vita ile haikuwa na maana tulikuwa tunawachukia sana raia wa Uganda ama mfumo wao wa maisha, la hasha, Waganda walikuwa ni ndugu na rafiki zetu kwa miaka mingi sana hata kabla Amini na wapuuzi wenzake hawajaingia madarakani.

Uamuzi wa kuivamia ardhi ya mkoa wa ziwa Magharibi (Kagera) haukuwa na ridhaa ya waganda hata kidogo bali ni maamuzi ya kipuuzi na kichokozi yaliyofanywa utawala wa kidhalimu wa dikteta Amini dada.

Nimejaribu kuanza mbali kwa kukumbushia vita ya Kagera na hivyo ndivyo inavyopaswa kueleweka kwa jamii ya watanzania kwamba, yule aliyekamatwa na Polisi ni "Emmaus Mwamakula" na hakukamatwa kwa sababu ya "uaskofu wake" au Jeshi la Polisi linalichukia sana kanisa la "Moravian Uamsho" ila alikamatwa kwa maana kuhamasiaha maandamano na kudai katiba mpya ni uamuzi wake binafsi na sio msimamo wa kanisa kama taasisi inayojitegemea.

Hili la huyu baba askofu limekaa hivi, hizi itikadi za kisiasa za mtu mmoja anayejulikana kama askofu kamwe haziwezi kuwa itikadi za wafuasi wote wa kanisa.

Serikali, kwa umoja wake, ina jukumu la kuunda taratibu za msingi pamoja na sheria zinazohitajika katika jamii ili kuweza kuruhusu watu wote kuishi maisha yao kama watakavyo pasipo kila mmoja kuleta bughudha kwa mwingine.

Ikiwa mtu anataka kuongeza itikadi zake binafsi za kisiasa katika sheria/misingi ya kanisa ambayo kila mtu anapaswa kufuata, swali la kwanza litakaloibuka ni "Je! Ni itikadi ipi/mlengo upi wa kisiasa ni sahihi utakaofaa?"

Itakuwa ni bahati nzuri sana kama kutapatikana kiwango chochote cha makubaliano/ maridhiano juu ya swali hilo muhimu na la msingi sana. Vile vile inaweza ikawa ni bahati mbaya sana, kwa maana vita nyingine ya wenyewe kwa wenyewe (ndani ya kanisa) inaweza kuibuka juu ya suala hilo hilo la kisiasa (katiba mpya kwenye muktadha ya kesi ya baba askofu)

Kama ambavyo mtu huchagua taaluma anayopenda kuisomea ama kiwango cha elimu anachopenda kuishia, ndivyo ilivyo hata katika siasa. Misimamo ya kisiasa ni chaguo.

Hakuna mtu anayepaswa kulazimishwa kufuata itikadi za mtu mwingine eti kwa kuwa ni kiongozi katika ngazi fulani ya kanisa. Hapana. Kanisa halifanyi kazi hivyo hata kidogo ndugu zangu kwa maana hakuna mtu anayeweza kulazimishwa kuamini kwamba katiba ya sasa ni sahihi ama sio sahihi.

Kama hiyo ndio hali halisi, sasa kwa nini umshawishi mtu yeyote afuate kitu ambacho haamini? Dini nyingi hutoa kanuni na miongozo ya kimaadili kwa washiriki wao kufuata.

Watu wengine, kwa makusudi kabisa, wanataka kuchanganya dini na siasa ili kila mtu alazimike kufuata itikadi sawa na zao kwa malengo wayajuayo wao wenyewe jambo ambalo sio sahihi hata kidogo.

Kwa mfano, Mimi binafsi sinywi pombe. Sikuwahi kujifunza kunywa kwa sababu dini yangu inafundisha kujiepusha na pombe. Inawezekana kabisa kwamba mtu mwingine anaweza kuwa alianza kunywa alipotimiza umri wa miaka 21, lakini baadaye aliamua kuacha na hakunywa tena kwa sababu aligundua alikuwa anaenenda kinyume na dini yake. Kwa mfano huo mdogo, je jamii nzima ikatazwe kunywa beer kwa staha eti kwa kuwa imani yangu mimi mtu mmoja inakataza? Jibu ni rahisi tu kuwa "HAPANA".

Je! sehemu iliyobaki ya waumini wote wa Kanisa ilazimishwe kuingia katika makatazo fulani fulani kwa sababu ya misimamo ya kisiasa ya mtu mmoja ama kikundi cha watu wachache wanaotaka kuingiza kanisa katika siasa? La hasha!

Ninaomba kumalizia kwa kusema, hoja za kisiasa zinazolenga kulazimisha itikadi za mtu mmoja au kikundi cha watu wachache ndani ya hizi dini/imani zetu juu ya wengine zinapaswa kukemewa na kuwekwa nje kabisa ya kanisa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Hii katiba ya mwaka 1977 wewe unaamini ni kamilifu? Nani hasa walikaa chini na kuiandika na kuipitisha? Je kwa hapa nchi ilipofikia, na ukitilia maanani mabilioni ya umma yaliyoliwa bure kwenye mchakato wa rasimu ya katiba ya mzee Warioba, hatuhitaji katiba mpya?

Kama sasa ni wakati muafaka kwa akili yako nani hasa alianzishe hili jambo? Kwa akili yako unadhani watawala wanaona umuhimu na haja ya kuwa na katiba mpya?

Nani hasa atanufaika ikiwa ile rasimu ya katiba ya mzee Warioba ingepita na kuwa katiba yetu mpya? Kwa akili yako, na kwa kuzingatia katiba na mifumo imara ya kuongoza nchi, umejifunza nini kutokana na uchaguzi wa Marekani?

Kwenye gazeti la Mwananchi la jana au leo, aliyewahi kuwa Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Tendwa amenukuliwa akisema wakati sasa umefika katiba kubadilishwa ili matokeo ya uchaguzi yaweze kupingwa mahakamani kama tunavyoona Kenya, Uganda na kwingineko what is your take on this?

Mfano wako wa mnywaji wa bia na ambaye hanywi ni irrelevant kwa sababu issue ya katiba inagusa walevi, wasio walevi, wacha Mungu, wapagani etc.
 
Askofu kamlazimisha nani kufuata Imani yake? Kama kaamua kufanya maandamano ya amani shida ipo wake? Kama wasingemfuata au wangemfuata si ni suala binafsi.

Kama Dini na Siasa havichangamani basi huifahamu Dini na Hufahamu Siasa. Askofu angesema maandamano ya kuunga Mkono utendaji wa Rais angekamatwa?

Wewe bado hujakua ukaelewa mambo. Endelea kuwa unasoma mambo unayatafsiri unaweka humu. Yale hayahitaji kutumia akili kuyaelewa.
 
Hii katiba ya mwaka 1977 wewe unaamini ni kamilifu? Nani hasa walikaa chini na kuiandika na kuipitisha? Je kwa hapa nchi ilipofikia, na ukitilia maanani mabilioni ya umma yaliyoliwa bure kwenye mchakato wa rasimu ya katiba ya mzee Warioba, hatuhitaji katiba mpya?
Issue ya katiba inagusa kila Mtanzania lakini wanasiasa wabaki na siasa na maaskofi waendelee na utumishi wao kwa kanisa.
 
Habari za wakati huu JamiiForums.

Kwanza kabisa ninaomba ieleweke kwa kila mmoja kwamba, Tanzania ililazimika kupigana vita ya Kagera mwaka 1977 kwa lengo la kumtoa nduli Idd Amin Dada na genge la wahuni wenzie.
Umejikakamua sana. Ungekunya tu kifupi askofu hana tatizo. Vipi kuhusu yule kiongozi wa dini ambaye ni mbunge anayesifia kila kitu kwa watawala?
 
Hoja yako Haina mashiko,

Kamwe
Huwezi kutenganisha kanisa (Dini) na SIASA.

Hata yesu mwenyewe aliwekwa msalabani na wanasiasa.

Na manabii wote tangu dunia iumbwe wamekufa vifo vya Mateso sana kwa kuingia kwenye 18 za wanasiasa.
CHADEMA kama kawaida yenu
 
Sawa mkuu ila mimi binafsi sio mwanasiasa
Angekuja kumsifia magufuli, wewe na mwenzako mambo sasa mngepiga mpaka vigelegele! Ila kwa sababu amekuja na hoja ya msingi ya kupigania haki, unakuja na mada yako ya kujichanganya!

Mbona wakati wa kampeni walijitokeza hadharani baadhi ya Masheikh Ubwabwa na Maaskofu Wanafiki kumuunga mkono magufuli, lakini hukuja na bandiko la kuwakemea kutenganisha siasa na dini?
 
Issue ya katiba inagusa kila mtanzania lakini wanasiasa wabaki na siasa na maaskofi waendelee na utumishi wao kwa kanisa.
Wewe kweli kilaza. Wapi katiba imetenganisha hao watu uliowataja na haki zao? Kuwa mtanzania atapata moja mbili tatu isipokuwa askofu au sheikh? Unaifahamu katiba? Soma katiba dogo ili upate uelewa. Katiba ni HAKI YA MTANZANIA.
 
Issue ya katiba inagusa kila mtanzania lakini wanasiasa wabaki na siasa na maaskofi waendelee na utumishi wao kwa kanisa.
Mwanasiasa ni mtanzania na askofu ni Mtanzania.

Ndani ya jamii kuna watu wa aina tofauti ambao wanaopaza sauti zisizosikika zilizomo ndani ya jamii ili kilio cha wahusika kisikike. Hao watu wamo wasanii wa uimbaji na waigizaji, wana michezo, wamo wanasiasa wenyewe, wamo viongozi wa dini n.k

Hao wote ni wanajamii ambao ni Watanzania. Utumishi wa Mungu haumvui mtu utanzania, uwanamuziki haumvui mtu utanzania n.k

Mtumishi wa Mungu anapoona mambo hayapo sawa ana jukumu la kupaza sauti kwa sababu yeye ni mtanzania. Halikadhalika anapoona mambo safi anapongeza kwa sababu yeye bado ni mtanzania.

Ukumbuke pia hao wote wanamuongoza binadamu. Siasa ni mwili na dini ni roho. Siasa imebeba itikadi ambayo inayoweza kuichafua roho. Kiongozi wa dini hatokustahi ukiichafua roho.
 
Back
Top Bottom