Dhana ya kutii sheria bila kushrutishwa: mna mawazo gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhana ya kutii sheria bila kushrutishwa: mna mawazo gani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, Mar 21, 2012.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  1. Dhana ya kutii sheria kwa hiari ni nzuri sana. Inafaa liwe somo la kufundishwa mashuleni kuanzia chekechekea hadi chuo kikuu.
  2. Nasema hivi kwa sababu matukio mengi mabaya yanayotendeka hapa nchini yanaonesha ni kwa jinsi gani Watz bado hatujui sheria na wala hatutaki kutimiza wajibu wetu.
  3. Kuonesha kuwa Watz wengi wanatii sheria kwa kushrutishwa angalia siku ambazo askari wa barabarani hawapo barabarani kuongoza magari kwa sababu ama wameenda kula au mvua inanyesha au hawapo tu kwa sababu nyingine yoyote, halafu uone madereva walivyo na akili mbovu - maana kila mmoja anataka kuwahi na matokeo yake wanachelewa wote.
  4. Pamoja na kuona umuhimu wa kutii sheria kwa uhuru, inanitia uchungu sana ninapoona askari polisi ndio wa kwanza kutotii sheria kwa hiari: nina mifano kadhaa: ndio wa kwanza kutanua kwenye traffic jam, ndio wa kwanza siyo tu kuendesha pikipiki bila helmet hata kupakia abiria bila helmet na wale wanaoendesha magari wanapiga maji tena wakiwa kwenye uniform, wanajichukulia sheria mkononi kupiga watuhumiwa wa uhalifu hata kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo na pia kuua raia kwa risasi za moto kuonesha wao wako juu ya sheria.
  5. Katika mazingira kama haya, polisi kusema "tutii sheria kwa hiari" wanakuwa wanafanya mzaha kabisa!
   
Loading...