Dhana ya kujiepusha Mikusanyiko dhidi ya Coronavirus na Mashindano ya Draft Kitaifa yanayofanyika Moshi Mjini Majengo Mississippi

Fya-fyafya

Member
May 2, 2019
43
125
Serikali kupitia kwa viongozi wa juu akiwemo Mheshimiwa.Raisi, Waziri mkuu na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto wamekuwa wakituhadharisha na kutupa Elimu ya namna gani ya kujilinda na kujiepusha na Huu ugonjwa Hatari wa Korona ambao umeangamiza maelfu na maelfu nduniani.

Moja ya njia ya kujiepusha na kujilinda na Ugonjwa huu ni kujiepusha na Mikusanyiko. Mikusanyiko kwa haraka haraka mtu anaweza kutafsiri kama; hali ya uwepo na watu wengi, vitu vingi ama wanyama wengi. Na kama tujuavyo wingi huanzia mbili!

Sasa niende kwenye maada yenyewe isemayo :" Dhana ya kujiepusha Mikusanyiko dhidi ya Coronavirus na Mashindano ya Draft Kitaifa yanayofanyika Moshi Mjini Majengo Mississippi." Jana katika eneo la Majengo Mississippi mkoani Kilimanjaro ndani ya Moshi manispaa kuliaanza ligi ya Draft Kitaifa ambapo mabingwa kutoka mikoa yote Nchini wamekutana kumsaka Bingwa wa Taifa.

Jana ambapo ilikuwa siku ya Hatua ya Makundi, majira ya saa tisa hadi saa kumi na mbili jioni kuliuhudiwa Umati mkubwa wa watu [Tazama picha hapo chini] wakiwa wamefurika kushuhudia mashindano hayo.

Kwa ratiba ilivyokuwa inaonesha jana , leo ni nusu fainali na kumpata bingwa ambaye atajinyakulia kitita cha Shilingi laki tatu. [ Tshs 300,000]

Japo kuwa jana kulikuwa na tahadhari ya ugonjwa huu wa Korona kwa kuwepo na maji ya yanayotiririka ya kunawa mikono pamoja na Sanitizer zakutosha, je hii inatosha kuwapa uhalali wa kufanya mashindando hayo ambayo yanahusisha wachezaji na watazamaji wengi hasa ya kuleta dhana ya mkusanyiko?
IMG_20200406_153439_2.jpg
IMG_20200406_154747_7.jpg
 
Back
Top Bottom