Dhana ya "kujenga uchumi"

nmkenda

Member
Mar 6, 2006
12
60
Eti mwenzenu mimi sioni kama tunaweza kujenga uchumi imara bila kuwa wazalishaji. Biashara sioni kama ni muhimili wa jishikilia.

Mimi nikiangalia nchi nilizochagua (sijui zingine) zimepanda kwa kusimamia vizuri rasilimali zake. Baada ya hapo biashara inakuja tu bila kupenda.

Mfano China ni mkakati mkubwa sana wa kilimo, viwanda vikubwa na migodi.

Urusi wali identify resources zao kama madini nk.
Marekani Waarabu, South Africa etc.

Kwa kweli tusipokuwa wakweli kwa nafsi zetu tutaumbuliwa hadharani vibaya sana kama huu mradi wa TANESCO ambao hata hauvutii kujadili.

Wafanya biashara watakuja tu, serikali iweke mkazo kwenye uzalishaji.

Resources zetu ni ardhi kwa kilimo madini na mifugo pia utalii.
viwanda vitokane na hayo na visimamiwe na waadilifu wakijua hapo ndio pa kujengea nchi au pa kuiulia.

Ningependekeza jina la nchi yetu lijulikane kwa umaarufu wa hayo yote. Kila moja na uzito wa kutosha.

Mfano wasiwepo watu wasio na uwezo katika hizo sekta, kwa sasa panatakiwa uwajibikaji wa haraka na ufanisi wa hali ya juu kujitoa shimoni zilipo na kuanza kupanda.

Chonde chonde wanasiasa sikilizeni wataalamu,
 
Heshima yako NMKENDA,

Kusema kweli hili swala zito sana!...nakubaliana na wewe kwa mapana kama alivyochangia ndugu yetu Poloz huko kwenye siasa. Kusema kweli nashindwa kabisa kuelewa elimu ya kitabu yaani economics inahusishwa vipi na mazingira yetu.

Mfano wako hapo juu tosha kabisa kutufahamisha kwamba, wasomi wetu sijui niseme viongozi maanake TZ viongozi wenyewe ndio haohao wasomi wanaotoa maamuzi ya ujenzi wa taifa hili. Kiutawala tu tayari tumekwisha changanya mchuzi na ndio maana viongozi wetu wana kiburi hawaambiliki.

Ni kweli kabisa maneno yako ukiangalia tunakokwenda kiuchumi inaonyesha wazi bishara imepewa kipaumbele mbele ya Uzalishaji.. sasa sijui hiyo biashara ni ya kudumu ama tunaweka mkazo pale kwenye mirathi tuliyoachiwa na Mungu....mali asili tu.

Ebu tazama toka uhuru, miundombinu kama reli ya kati na hiyo ya kaskazini imeshukashuka chini mwaka hadi mwaka haina ukarabati. na ukitazama kwa undani utakuta pato la mashirika haya yameshuka mwaka hadi kwaka na sababu kubwa ni ukosefu wa bidhaa!... yaani uzalishaji umepungua. Cha ajabu ni kwamba kila mwaka hata kama hizo statistics zinaonyesha kupungua kwa uzalishaji bado serikali yetu imefunga mkanda ktk sera ambazo zinazidi kupotosha kabisa malengo.

Hatuwezi kufikia kujitegemea ikiwa Watanzania hatutaweza kuzalisha wenyewe mazao, mali ghafi za viwanda na hata finished product nchini. Na wala sijui nani wa kulaumu kwani wakulima na wenye viwanda pia madai yao nchi yetu haina maji wala umeme kuendesha shughuli zao. hawana budi kufunga virago na kutafuta riziki sehemu nyinginezo zisizotegemea maji wala umeme kwa wingi....

Hivi kweli tutafika?
 
...wind energy ndio itatuondolea matatizo yetu ya umeme sio vinginevyo..Germany sasa wamefikia 110,000 MW from wind energy,Tanzania nchi nzima hata hatuhitaji 1000MW na approx. cost za kujenga 100MW hazifiki hata 100m$,huku Richmond na IPTL tuliwapa 100's of millions kwa umeme ambao unatucost milele...

Wind technology imemprove sana miaka ya karibuni,jamani we need that kama kuna mhusika humu afanye kazi yake...information zote zipo kwenye internet,hope tutaweza kuwa exporter wakubwa wa UMEME na viwanda vyetu tukaweza kuzalisha kwa bei rahisi,kwa ufupi tutawasha engine yetu ya maendeleo maana umeme ni kila kitu(ENERGY)
 
Koba,
1. Wind poa- naunga mnoko!
2. Serikali yenyewe itengenge fungu la pesa pia kuwasaidi wawekezaji wazawa wakubwa kufungua viwanda vikubwa. Au watoe guarantee-manake vingi vilivyopo sii vya wazawa! sisi ni vibarua tu! Mimi bado sijaona juhudi ya makusudi -ZA wana Black Empowerment Scheme! Sisi hapa tunaongea tu kuwaleta wawekezaji wa nje!
3. At the same time kuimarisha miundo mbinu
 
Hali yako muheshimiwa NMKENDA,tatizo ni kwamba nani atamfunga paka kengele ikiwa viongozi wote wa bongo ni wababaishaji??
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom