Dhana ya Kuinuana Kiuchumi baina ya Wanafamilia; Kuna haja unapompa ndugu yako Mtaji wa biashara umtoze riba ili kuongeza uwajibikaji?

Haileti picha nzuri kupewa mtaji then uutumie ndivyo sivyo, tena unakuta anayekupa hata amekopa benki.

So ukibeba make sure unabebeka, lengo ni kupunguza umasikini level ya familia
Huyo mdogo wako anachukulia maisha kiutani utani sababu ndugu mpo wa kumsaidia ila mkimchinjia baharini atatia akili!
Akipoteza na hela mara 3 mfululizo mkatieni umeme achapwe na ukata ndio ataelewa somo!
 
Tusipobadirika na kuanza kuwa na family businesses then tutaishia kuona tu group of companies za wahindi, waarabu, wachina na nchi zingine then watoto wenu wawe tu waajiriwa kila leo
Very sure, tatizo wenzako kuona vile unaona wewe ndiyo shida, Wenzetu Wahindi wanaweza Sana.

Akina Dewij nimeanza kuwasikia kitambo Sana hadi leo hii wapo
 
Huyo mdogo wako anachukulia maisha kiutani utani sababu ndugu mpo wa kumsaidia ila mkimchinjia baharini atatia akili!
Akipoteza na hela mara 3 mfululizo mkatieni umeme achapwe na ukata ndio ataelewa somo!
Ni sahihi, pengine itakuwa nafasi yake kujifunza
 
Binafsi naamini kwenye familia, mmoja anaweza kuinuliwa ili aweze kuwainua wengine. Ndiyo maana kwenye maandiko Kitabu cha Mwanzo 42:25-28 unaona Yusufu alivyoinuliwa ili kuwasaidia ndugu zake. Kuna mtu anaweza kujiuliza kwani ni lazima kuwasaidia ndugu zako, Jibu sio lazima (Sijui kama kuna sheria inayolazimisha ndugu kusaidiwa hata Baba/Mama sio lazima) kuwasaidia lakini unajiuliza ni faida kiasi gani unapata kuona ndugu zako wakihangaika mitaani bila mafanikio wakati wewe ukiwa na nafuu?

Binafsi nimejaribu mara kadhaa kuwainua ndugu zangu (Tumbo moja) bila mafanikio mwisho wa siku najikuta napoteza mitaji tu. Natolea mfano, mwaka fulani nilimpa brother angu mtaji wa kumwezesha afanye biashara fulani iliyonigharimu kiasi. Bahati mbaya biashara akaiua/akala mtaji. Next time, nikampa mtaji mdogo wangu afanye biashara fulani aliyoitaka. Bahati mbaya naye akapoteza mtaji bila kufanikiwa. Simu za brother zikawa nyingi kuomba assistance huku akinishtakia kwa Wazee. Baada ya mivutano kidogo nikampa mtaji mwingine. Shida inakuja kwenye suala la kuikuza biashara na kuiendeleza, brother anafail, Kwahiyo baada ya muda mtaji huu pia ukafa.

Sasa nimempa mtaji wa mwisho wa biashara, akipoteza na huu Potelea mbali. Sitajali lawama za Walimwengu, hata Mungu anaona nilivyojitolea.

Swali, Je, kuna haja ya tunapowapa mitaji ndugu zetu(tuandikishiane) na tuanze kutoza riba ili kuongeza uwajibikaji (accountability)?? Jambo hili litakuwa na athari zozote kwa ustawi na mahusiano ya familia?
Jitahidi kuwapa Mawazo (elimu) kwanza kabla ya kuwapa mtaji. Ikibidi mpe ndoano akavue samaki kuliko kumleta Samaki aliyevuliwa tayari.
 
Kivipi Mkuu?
Yaani logic hapo ni kuinuana kwa lengo la kupunguza umasikini kwa level ya Familia
Nitakupa mfano. Nikitumia masaa kumi kusukuma zege ambalo haliwezi kuangushwa na greda utaniitaje?

Umaskini level ya familia unaondoka kwa wanafamilia kupambana kila mtu kwa njia yake. Unampa mtu support ambaye kaanzisha kitu na unaona anapambana. Ngoja nikupe huu mstari ukusaidie. Ukipata nafasi soma tu sura nzima utapata somo la mtu gana anapaswa kusaidiwa.

Mathayo 25
24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;

25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.

26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;

27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

28 Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.

29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.

Hii ni kanuni ya maisha. Mpambanaji anaongezewa. Mzembe, hata alicho nacho kinachukuliwa anapewa mpambanaji
 
Kuna ndugu wengine ukimpiga tafu mtaji anaenda fanyia starehe pombe..au mwingine ananunua furniture zA gharama anashop mlimani city hata mchele au maharage ananunua mlimani city ..hawa tunawaweka kundi lipi?
Kutoa msaada pasipo kuangalia vigezo na masharti nalo ni tatizo mkuu .

Binafsi nimekutolea mfano hai uliyonihusu mwaka 2006 na leo tunajivunia kwa kuwekeza kwake kiasi nae kumfanya awekeze kwa wenzake 3 kwa mtindo ule ule huku akiboresha baadhi ya maeneo .

WAKUU kunatofauti mbili kuu Kati ya KUMSAIDIA mtu ili ujiondoe na lawama kwa family na KUMSAIDIA mtu ili upunguze utegemezi kwenye family .

Nimeeleza pale juu kuwa aina ya kwanza ni kumtatulia mwanafamily hitaji lake pasipo kumfanyia uchunguzi wa kina juu ya MSINGI WA HITAJI LAKE SAMBAMBA NA CHANZO KILICHOMPELEKEA YEYE KUWA ALIVYO NA AINA YA PILI NI KUANGALIA HITAJI LAKE NA UHALISIA WA SABABU HALISI YA MKWAMO WAKE .

Wakuu.

Siyo kila tatizo linalopelekea mtu kuwa na mkwamo wa KIUCHUMI huwa linaweza kutatuliwa na pesa ,sasa unapompa mtu pesa pasipokuangalia chanzo cha mkwamo wake hii tunaita nikutakatu kujiondoa kwenye lawama za kifamily otherwise you won't do that na badala yake utamsogeza karibu na kumpa ushirikiano sambamba na kumuonyesha njia sahihi ambazo unadhani hasa ndizo zilizompelekea awe alivyo na mwisho kumpa ufumbuzi wa tatizo lake .

Msaada wa pesa huwa na maana zaidi kwa mtu aliye na utayari wa ndani sambamba na kuwa na wazo imara linalousukuma moyo wake juu ya hitaji lake la kujikwamua KIUCHUMI .

Hitimisho
Kabla hujaamua kumsaidia mtu kujinasua na tatizo lake (bila kujali aina ya tatizo lake) yafaa kwanza ukajitahidi ukifahamu chanzo cha tatizo lililompelekea awe alivyo sambamba na kumtafutia njia mujarabu za kujikwamua nalo and not otherwise .
 
Mada nzuli sn wenzetu warabu na waindi wanafanya sn hii njia na inawatoa sn nzuli zaidi hasa hasa kwa warabu mtu anapewa mtaji na biashara idia yani anapewa cash pesa na conection ya biashara aise wakikutana ndugu kma familia wote madone
 
Sisi kwetu tunasaidiana kwa kukomoana tu ,ufell ili wakucheke na mwisho uendelee kumuabudia aliyekusaidia huku akiendelea kukudumaza kiakili kuwa wewe siyo kitu ,huwezi ,wewe silolote which is very bad .

Licha ya kuuwa ndoto za wanafamilia wetu pia tunaongeza sana idadi ya wategemezi kwenye family zetu kitu ambacho mwisho wa siku hugeuka kuwa mzigo kwenye maisha yetu .
 
Tukubaliane kitu kimoja

Kuna watu hapo juu wametoa michango ya kwamba unamsaidia mtu kwa lengo la kupata ukuu au Umungu mtu, na lengo sio afanikiwe bali aendelee kuwa shidani, hili napingana nalo.

Nadhani ni rahisi zaidi kumnyima mtu msaada kuliko kumpa ule wa kusudio la yeye asifanikiwe.

Tunachopaswa kufahamu familia zetu ni kama darasa lenye wanafunzi wengi, kila mnoja atakua na akili yake na uwezo wake, utapata characters aina tofauti tofauti.

Wote hawatakua na uwezo sawa wala tabia.

Tukubali tukatae kuna watu hawasaidiki, kuna watu utawasaidia watajipinda kwelikweli kuhakikisha msaada ule unamfikisha sehemu fulani nzuri.

Hawa wasiosaidika sio kwamba hawafahamu, bali hawajali, uoga wa kwanza mtu unatakiwa kuwa nao ni kuogopa utegemezi, ukiona mpaka leo hii huoni tabu kutembeza bakuli na utu uzima wako jitafakari mara mbilimbili.
 
Sasa mtu mlevi kweli kabisa unampa mtaji na unajipa moyo kabisa nimemsaidia kaka, mdogo wangu😂😂.

Akifika kona ya kichochoro anasema hiiiiiiii bangosha, anakuteta kabisa huyu mwamba hajui utamu wa pombe.
 
Binafsi naamini kwenye familia, mmoja anaweza kuinuliwa ili aweze kuwainua wengine. Ndiyo maana kwenye maandiko Kitabu cha Mwanzo 42:25-28 unaona Yusufu alivyoinuliwa ili kuwasaidia ndugu zake. Kuna mtu anaweza kujiuliza kwani ni lazima kuwasaidia ndugu zako, Jibu sio lazima (Sijui kama kuna sheria inayolazimisha ndugu kusaidiwa hata Baba/Mama sio lazima) kuwasaidia lakini unajiuliza ni faida kiasi gani unapata kuona ndugu zako wakihangaika mitaani bila mafanikio wakati wewe ukiwa na nafuu?

Binafsi nimejaribu mara kadhaa kuwainua ndugu zangu (Tumbo moja) bila mafanikio mwisho wa siku najikuta napoteza mitaji tu. Natolea mfano, mwaka fulani nilimpa brother angu mtaji wa kumwezesha afanye biashara fulani iliyonigharimu kiasi. Bahati mbaya biashara akaiua/akala mtaji. Next time, nikampa mtaji mdogo wangu afanye biashara fulani aliyoitaka. Bahati mbaya naye akapoteza mtaji bila kufanikiwa. Simu za brother zikawa nyingi kuomba assistance huku akinishtakia kwa Wazee. Baada ya mivutano kidogo nikampa mtaji mwingine. Shida inakuja kwenye suala la kuikuza biashara na kuiendeleza, brother anafail, Kwahiyo baada ya muda mtaji huu pia ukafa.

Sasa nimempa mtaji wa mwisho wa biashara, akipoteza na huu Potelea mbali. Sitajali lawama za Walimwengu, hata Mungu anaona nilivyojitolea.

Swali, Je, kuna haja ya tunapowapa mitaji ndugu zetu(tuandikishiane) na tuanze kutoza riba ili kuongeza uwajibikaji (accountability)?? Jambo hili litakuwa na athari zozote kwa ustawi na mahusiano ya familia?
Katika kila familia mara nying hutokea mtu mmoja kwa ajili ya kubreak "a chain of poverty" ya ukoo/familia, huwa ni mpango wa Mungu kabisa.Tatizo kubwa ya familia hizo huwa ndugu/jamaa wengi wa mhusika huwa na uelewa mdogo na elimu hamna! Unaptia hali sawa na yangu, mimi wa mwisho kwetu, mabro wote chenga ukiwapa hela wanatumia then lawama zinabaki palepale! Kwa vile bro mmoja alinipambania hadi nikafika nilipo, siwapi pesa kamwe, natunza wazazi na kusomesha madogo wote wa home mpaka pale ambapo mtu atashindwa mwenyew ila sio kukosa ada/mahitaji! Tunza wazazi, somesha ndugu zako. Ukiendelea kuwapa pesa utapoteza! Wape pale kwenye tatzo
 
Tukubaliane kitu kimoja

Kuna watu hapo juu wametoa michango ya kwamba unamsaidia mtu kwa lengo la kupata ukuu au Umungu mtu, na lengo sio afanikiwe bali aendelee kuwa shidani, hili napingana nalo.

Nadhani ni rahisi zaidi kumnyima mtu msaada kuliko kumpa ule wa kusudio la yeye asifanikiwe.

Tunachopaswa kufahamu familia zetu ni kama darasa lenye wanafunzi wengi, kila mnoja atakua na akili yake na uwezo wake, utapata characters aina tofauti tofauti.

Wote hawatakua na uwezo sawa wala tabia.

Tukubali tukatae kuna watu hawasaidiki, kuna watu utawasaidia watajipinda kwelikweli kuhakikisha msaada ule unamfikisha sehemu fulani nzuri.

Hawa wasiosaidika sio kwamba hawafahamu, bali hawajali, uoga wa kwanza mtu unatakiwa kuwa nao ni kuogopa utegemezi, ukiona mpaka leo hii huoni tabu kutembeza bakuli na utu uzima wako jitafakari mara mbilimbili.
Nimeeleze misaada ile inayotolewa ilimradi imetolewa kwa muhusika pasipo kufanya deep analysis juu ya chanzo cha mkwamo wake mkuu wangu .

Kuna mkuu hapo juu amesema "UNAKUTA MTU ANAMPATIA MTAJI MLEVI THEN ANA EXPECT MATOKEO CHANYA" hebu tuuchukulie mfano huu as a case study , umeona kabisa mwanafamilia wako ako na shida ya "ULEVI" tena ULEVI ndiyo umekuwa chanzo cha mkwamo wake na badala yake hujali hilo unampatia tena mtaji , hebu hapa napo tusemeje?

Binafsi naamini hakuna kinachoshindikana kwenye UPENDO NA DHAMIRA YA DHATI AS LONG AS UMEAMUA KUPAMBANA NA UTEGEMEZI NYUMBANI huyu nirahisi aidha kumchukua au kumuandalia program maalumu ya kuhakikisha u amuondoa kwenye tatizo lake la awali kabla hujaanza kummilikisha mali au kumpa jukumu la kujisimamia.

Iwe kwa kumpeleka kwenye vituo maalumu vya watu wenye shida hiyo au kuutumiae mwamvuli wa DINI kumrejesha kwenye misingi na kisha ndiyo umuwezeshe , kinyume na hapo MSAADA UTAKAOMPATIA KABLA HUJAMTOA KWENYE SHIDA MSINGI HUO TUTUITA MSAADA WA KUJIONDOA KWENYE LAWAMA Mkuu wangu .
 
Katika kila familia mara nying hutokea mtu mmoja kwa ajili ya kubreak "a chain of poverty" ya ukoo/familia. Tatizo kubwa ya familia hizo huwa ndugu/jamaa wengi wa mhusika huwa na uelewa mdogo na elimu hamna! Unaptia hali sawa na yangu, mimi wa mwisho kwetu, mabro wote chenga ukiwapa hela wanatumia then lawama zinabaki palepale! Kwa vile bro mmoja alinipambania hadi nikafika nilipo, siwapi pesa kamwe, natunza wazazi na kusomesha madogo wote wa home mpaka pale ambapo mtu atashindwa mwenyew ila sio kukosa ada/mahitaji! Tunza wazazi, somesha ndugu zako. Ukiendelea kuwapa pesa utaoteza! Wape pale kwenye tatzo
I see! Kumbe ni mitihani ya wengi hili

Unajua ingekuwa wanaweza kuona vile unaona naamini hata issue ya poverty kwenye familia nyingi zingepungua kama sio kuisha kabisa.
Ni aibu miaka zaidi 59 bado tunaishi na umasikini
 
Jitahidi kuwapa Mawazo (elimu) kwanza kabla ya kuwapa mtaji. Ikibidi mpe ndoano akavue samaki kuliko kumleta Samaki aliyevuliwa tayari.
Kwa upande wangu ndoano niliyodhani nawapa ilikuwa Mtaji, najua ingekuwa wako serious enough tungekuwa tumeshashinda adui umasikini kwa sehemu.

Nimegundua suala la kuvunja mnyororo wa Umasikini kwenye level ya familia zetu si lelemala
 
Hawa wasiosaidika sio kwamba hawafahamu, bali hawajali, uoga wa kwanza mtu unatakiwa kuwa nao ni kuogopa utegemezi, ukiona mpaka leo hii huoni tabu kutembeza bakuli na utu uzima wako jitafakari mara mbilimbili.
Hakuna kitu naogopa kama kufika Uzee na kuendelea kutegemea kudra za watoto au ndugu kupata chakula cha kila siku kuishi.

Ndiyo maana nilidhani mkisaidiana kuushinda umasikini niliamini hata akiba ya kukuwezesha kuishi wakati wa Uzee wakati unasubiri kufa unakuwa nayo. Ni basi tu watu wanatofautiana ufahamu
 
Mada nzuli sn wenzetu warabu na waindi wanafanya sn hii njia na inawatoa sn nzuli zaidi hasa hasa kwa warabu mtu anapewa mtaji na biashara idia yani anapewa cash pesa na conection ya biashara aise wakikutana ndugu kma familia wote madone
Nadhani na huku Bongo wenzetu Wachagga hupigana tafu sana sijui kama miaka ya hivi karibuni wameacha.

Faida ya kuvunja umasikini kwenye level ya familia ni Kubwa kuliko kuendelea kuukumbatia.
Kama mtu anapewa mtaji wa kumkwamua kutoka kwenye umasikini basi tungeweka hata riba ili ajue kuwa kila wiki natakiwa kupeleka Rejesho. Tena ingekuwa vyema hilo rejesho awe anapeleka Kituo cha Polisi kilichokaribu yake.
 
Back
Top Bottom