Criss
JF-Expert Member
- Mar 19, 2011
- 858
- 252
Naogopa kusema kuwa kama siyo wewe ni wakufaa kulaumiwa kwenye mkwamo wake basi wewe haukuwa msaada sahihi wa tatizo lake .Binafsi naamini kwenye familia, mmoja anaweza kuinuliwa ili aweze kuwainua wengine. Ndiyo maana kwenye maandiko Kitabu cha Mwanzo 42:25-28 unaona Yusufu alivyoinuliwa ili kuwasaidia ndugu zake. Kuna mtu anaweza kujiuliza kwani ni lazima kuwasaidia ndugu zako, Jibu sio lazima (Sijui kama kuna sheria inayolazimisha ndugu kusaidiwa hata Baba/Mama sio lazima) kuwasaidia lakini unajiuliza ni faida kiasi gani unapata kuona ndugu zako wakihangaika mitaani bila mafanikio wakati wewe ukiwa na nafuu?
Binafsi nimejaribu mara kadhaa kuwainua ndugu zangu (Tumbo moja) bila mafanikio mwisho wa siku najikuta napoteza mitaji tu. Natolea mfano, mwaka fulani nilimpa brother angu mtaji wa kumwezesha afanye biashara fulani iliyonigharimu kiasi. Bahati mbaya biashara akaiua/akala mtaji. Next time, nikampa mtaji mdogo wangu afanye biashara fulani aliyoitaka. Bahati mbaya naye akapoteza mtaji bila kufanikiwa. Simu za brother zikawa nyingi kuomba assistance huku akinishtakia kwa Wazee. Baada ya mivutano kidogo nikampa mtaji mwingine. Shida inakuja kwenye suala la kuikuza biashara na kuiendeleza, brother anafail, Kwahiyo baada ya muda mtaji huu pia ukafa.
Sasa nimempa mtaji wa mwisho wa biashara, akipoteza na huu Potelea mbali. Sitajali lawama za Walimwengu, hata Mungu anaona nilivyojitolea.
Swali, Je, kuna haja ya tunapowapa mitaji ndugu zetu(tuandikishiane) na tuanze kutoza riba ili kuongeza uwajibikaji (accountability)?? Jambo hili litakuwa na athari zozote kwa ustawi na mahusiano ya familia?
Nikama natamani kukuuliza maswali matatu madogo yahusuyo chanzo cha mafanikio yako na weredi wa uliyemsaidia :-
1.
(a) Mafanikio yako yametokana na (ELIMU) bila kujali ukubwa wa mshahara wako (ninachotaka kusema hapa nikuwa ,wenda uwelimu yako imekusaidia kujitambua na kukuongezea umakini .
(b) Au ulifanikiwa tu kwa kudra za Mwenyezi Mungu plus ujanja ujanja?
2.
(a) Msaidiwa anakiwango gani cha elimu ,anaujuzi wowote?
(b) Ulimsaidia kwa kumuwekezea kwenye kile alicho na ujuzi nacho , wewe ndiye uliyempangia chakufanya au ulimsaidia fedha kisha yeye asonge zake tu kwa kudra za Mungu?
3.
(a) Baada ya kumsaidia fedha /mali ulimsaidia ,pia kumpa usimamizi wa karibu juu ya kumfanikishia kuzifikia ndoto zake ? Au ulimpa ili tu uondoe lawama kwa family ?
Sitaki kusema watu wengi hasa tunaojiita watoa msaada wa family zetu ndiyo haswa huwa vyanzo vikuu vya kudumaza ndoto na ustawi wa family zetu .
Wengi wetu hasa waafrika tunahulka za UBINAFSI ,wengi huwa tunataka kuonekana miungu watu kwenye family zetu kutokana na aidha vyeo au mali tulizonazo na hata pale tunapotakiwa au tunapowasaidia wengine huwa tunafanya hivyo lakini siyo kwa dhamira zetu za ndani ,lengo kubwa ni washindwe ili tujidhihirishe kwao na kwakuokoo kuwa Mafanikio siyo lelemama
NAOGOPA KUHITIMISHA KWA KUSEMA MTOA MADA HUWA HAITOI MISAADA YAKE KWA LENGO LA DHATI LA KUMSAIDIA MWWNAFAMILY WAKE AFANIKIWE BALI NI KWA LENGO LA KUTAKA KUJIONDOA KWENYE KUNDI LA LAWAMA .
Binafsi ninamfano wangu kwa mdogo wangu wa kike aliyekuwa ameishia form four wakati ule , na kupachikwa mimba ,kwababhati mbaya aliyempa mimba alipoteza mvuto nae ndani ya muda mfupi Baada ya kujifungia na akahamishia mahaba kwa mschana mwingine ,kwetu halikuwa kosa , tatizo lilianzia pale mdogo wetu alipoomba apewe mtaji , sisi tukamwambia kwa sasa hana sifa ya kupewa mtaji hadi hapo atakapotimiza vigezo , na kigezo No 1 akubali kuendelea na shule au arudi nyumbani na kukaa miaka miwili ili achunguzwe ili tuone kama atakuwa na sifa zitakazomfanya apewe msaada .
Alikubali kurudi shule na kuendelea na form five na six na hata chuo .
Wakati yupo chuo alichagua kuwa mtabibu ,hii ilimfanya boom lake la kwanza aliwekeze kwenye duka la madawa baridi na Baada ya muda kidogo akatushawishi tumuongezee nguvu kwenye biashara yake hiyo ,Baada ya maswali mawili matatu tulijiridhisha nakumsaidia kutimiza hitaji lake huku tukimsaidia kumpa mbinu kadhaa za kiushindani zikiwemo kuweka record za wagonjwa anaowahudumia ,anuani za wanakotoka pamoja na history za magonjwa yanayowasumbua .
Pia tulimsaidia gari ndogo ili awe anawatembelea kwenye makazi yao walau maramoja kwa wiki sambamba na kuwapelekea walau dawa za kupunguza maumivu na juice za na maji madogo sambamba na kuwapa ushauri wa kitaalamu uhusuyo matatizo yanayowahusu .
Hii ilimjengea jina sana kiasi cha kuongeza idadi ya wateja (wagonjwa) hivyo kulazimika kuongeza eneo la kuwapokea sambamba na kuandaa eneo la kuwapumzisha kwa muda wale ambao wanakuna wakiwa hawako kwenye hali ya kuweza kukaa na sasa anamiliki hospital Arusha na hajawahi kuhangaikia ajira tena serikalini na tatizo lake KIUCHUMI nikama limekwisha kusovika kwa zaidi ya 85% .
Mtoa mada wenda ukawa na chakujifunza , samahanini kwa maelezo MAREFU