Mhe. Rais amesisitiza sana kuwa kila mtu anyenunua huduma ADAI RISITI.
Kwa utamaduni wetu wa Kitanzania nadhani ni 2% tu ya wafanyabiashara ndio wanaotoa risiti na hivyo mpaka sasa 98% hawatoi risiti kwa sababu watanzania hatuna utamaduni wa kudai risiti.
Nitoe mfano mdogo tu. Kwenye bucha zetu nani anatoa risiti ii hali kwa siku muuza bucha kwa kiwango kidogo wanauza si chini ya Tshs.800,000 kwa siku.
Pili, twende kwenye vituo vya Mafuta, hapa unapewa risiti ukichachamaa. Kwanza EFD mashine wanaificha ili usiione.
Tatu,lini hoteli zetu za kawaida wakatoa risiti lakini kwa siku wanauza si chini ya Tshs.300,000.
Natoa ushauri, kwa wenye bucha watoe risiti kule machinjioni mfano vingunguti kwa kilo zote za nyama alizonunua kabla hajaifikisha kwenye bucha.
Pili kwa wenye vituo vya mafuta, mashine za EFD zifungwe kwenye kila pampu ya mafuta ili mteja anapowekewa mafuta basi risiti itoke pale pale kwa idadi ya mafuta aliyowekewa. Kwa wenye mahoteli, TRA iwakadirie mapato yao kwa siku, ili kila mwisho wa mauzo ya siku basi atoe risiti. Mfano amekadiriwa Tshs.300,000 akimaliza kazi ya siku hiyo atoe risiti.
Hivi sasa sehemu nyingi hawatoi risiti na Serikali inapoteza mapato kweli kweli hasa kwenye vituo vya mafuta.
Mwisho, elimu iendelee kutolewa ili Watanzania wafahamu maana ya risiti inavyochangia mapato ya nchi na hatimaye kupelekea uboreshaji wa huduma za kijamii.