Dhana ya kubemenda mtoto: Mitazamo, Ufafanuzi na Ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhana ya kubemenda mtoto: Mitazamo, Ufafanuzi na Ushauri

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NGULI, Dec 7, 2009.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Dhana nzima ya kubemenda mtoto

  Kuna hili suala linaloitwa 'kubemenda' mtoto. Watu wanadai kuwa sperms huwa zinaleta madhara kwenye maziwa ya mama na kumdhoofisha mtoto kiafya na wengine wanasema ukimshika mtoto baada ya sex pia ina madhara. kiukweli suala la Kubemenda ni imani potofu (myth) na hakuna uhusiano wa sperms na maziwa ya mama katika kudhoofisha afya ya mtoto; iwe kwa kushirikiana tendo la ndoa au kumshika mtoto baada ya sex.

  Je, nini maana ya kubemenda mtoto?

  Kwanza hii imani potofu inaeleza kwamba kubemenda mtoto ni pale wanandoa wanapojihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa (pale mke anapokuwa tayari kiafya kwa tendo la ndoa baada ya kujifungua) kwa maana kwamba sperms huharibu maziwa ambayo mtoto ananyonya, si kweli hakuna uhusiano wowote kati ya maziwa ya mama na sperms katika kuathiri afya ya mtoto.
  Pili kubemenda mtoto ni kitendo cha wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa na mke kushika mimba miezi mwili tu au mitatu tu baada ya kujifungua na kupelekea kuzaa mtoto mwingine baada ya mwaka na matokeo yake mtoto aliyetangulia Kuzaliwa huwa dhaifu kiafya (huchelewa kutembea) na huitwa ni mtoto ambaye amebemendwa, kitu ambacho ni imani potofu kwani kuna wanandoa wengi tu wamezaa watoto waliopishana mwaka na wote wana afya njema kabisa.

  Tatu kubemenda ni kitendo cha mwanandoa mmoja kutoka nje ya ndoa (sex) na akirudi ndani huendelea na tendo la ndoa na matokeo yake mtoto wa ndani ya ndoa huwa dhaifu, pia ni imani potofu hakuna kitu kama hicho. Jambo la msingi ni kufuata ushauri wa kitaalamu ambao ni wiki sita baada ya kujifungua. Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hii imani potofu Iwe wanandoa kujihusisha na tendo la ndoa baada ya mtoto Kuzaliwa au kuzaa mwingine baada ya mwaka au hata kutoka nje hakuna uhusiano na mtoto aliyezaliwa kama suala la usafi na lishe bora litazingatiwa kwa mtoto anayehusika.

  Je, kulikoni mababu zetu wakaweka imani kama hiyo kwa wanandoa?

  Kama zilivyo imani zingine potofu kama vile mwanamke mjamzito kutokula mayai mababu zetu walikuwa na somo ndani yake, inawezekana walitaka kuhakikisha wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea mtoto kwa pamoja bila kupendekeza tabia za uchafu na kujirusha nje na ndani ya ndoa bila utaratibu. Pia labda mababu zetu walihofia kitendo cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika) wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika kileleni (tangu akifungue hadi miezi 8 hivi) na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba mtoto ataathirika kwa mke na mume kushiriki tendo la ndoa.

  Je, ili mtoto asionekane amebemendwa wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani?

  Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya mama wakati wa kumnyonyesha mtoto hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea. Mtoto anahitaji watoto chakula bora chenye viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua vizuri pia mama anahitaji kujiweka mazingira safi (kuwa msafi) wakati ananyonyesha, ahakikishe anasafisha chuchu zake na mikono yake au kuzingatia usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto iwe baada ya sex au muda wowote.

  Je, kulikoni mababu zetu wakaweka imani kama hiyo kwa wanandoa?

  Kama zilivyo imani zingine potofu kama vile mwanamke mjamzito kutokula mayai mababu zetu walikuwa na somo ndani yake, inawezekana walitaka kuhakikisha wanandoa wanashiriki vizuri katika kulea mtoto kwa pamoja bila kupendekeza tabia za uchafu na kujirusha nje na ndani ya ndoa bila utaratibu. Pia labda mababu zetu walihofia kitendo cha mwanamke kutoa maziwa (chuluzika) wakati wa tendo la ndoa hasa anapofika kileleni (tangu akifungue hadi miezi 8 hivi) na wakawa wanahofia kinaweza kuathiri kiwango cha chakula cha mtoto hivyo ili kuzuia ni kutunga imani (potofu) kwamba mtoto ataathirika kwa mke na mume kushiriki tendo la ndoa.

  Je, ili mtoto asionekane amebemendwa wanandoa wanahitaji kufanya kitu gani?

  Ni vizuri kufahamu kwamba hakuna uhusiano wa sperms kuharibu maziwa ya mama wakati wa kumnyonyesha mtoto hivyo wanandoa kushiriki tendo la ndoa halina uhusiano wowote na mtoto kuwa na afya mbaya kiasi cha kuchelewa kutembea. Mtoto anahitaji watoto chakula bora chenye viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua vizuri pia mama anahitaji kujiweka mazingira safi (kuwa msafi) wakati ananyonyesha, ahakikishe anasafisha chuchu zake na mikono yake au kuzingatia usafi kimwili kabla ya kumnyonyesha mtoto iwe baada ya sex au muda wowote. Huwezi kusikia takataka za neno kubemenda katika nchi zilizoendelea kama Canada, Sweden, Australia, Ujerumani nk why? Ni traditions (Myth).

  Chanzo: sayi manyanda

   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Imani zetu za kienyeji, mzazi wa kike au wakiume harusiwi kumshika mtoto wake mdogo(aliyezaliwa chini ya miezi 9) bila ya kujisafisha/kuoga iwapo atakuwa ametoka kufanya matusi nje ya ndoa.Akifanya hivyo mtoto huwa mzaifu na huandamwa na magonjwa.
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,990
  Likes Received: 23,886
  Trophy Points: 280
  Sure! Imagine wife ametoka kuliwa denda na jitu linalipiga mswaki mara moja kwa wiki. Akanyonywa maziwa na jitu lililotoka kunywa mnazi. Chuchu zimetomaswa na mikono yenye aleji na maji + sabuni. Midume mingine ikipiga bao inaenda kumwagia sh.ahawa zao kwenye chuchu za wanawake.Afu mama arudi home hajaoga anyonyeshe kabinti kake! Unategemea nini hapo kwenye makuzi!

  Nadhani kubemenda kwenyewe kunakuja kihivyo!
   
 4. c

  compressor Member

  #4
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa mfano mke ametoka kuliwa denda na mtu anaepiga mswaki kila siku katika siku zote za wiki. Akanyonywa maziwa na mtu ambae hanywi pombe ya aina yoyote. Chuchu zikatomaswa na mikono isiyona aleji na maji + sabuni. akapigwa bao ndani na si kwenye chuchu.Afu mama arudi home hajaoga anyonyeshe kabinti kake! JE kubemenda kutakuja?,Je kubemenda ni swala la uchafu tu?,naomba unielimishe mkuu
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  wengine wanasema "kukira"....hata mwanaume nae anaweza kubemenda mtoto, pale anapotoka kufanya matuc huko nje akija home anamparamia mama bila kujiweka safi, lakini kwa mwanamke ndio sana..na watoto wanaobemendwa huwa wanachelewa kutembea, unakuta mtoto anakuwa mzito sana kwenye mambo ya kawaida, na kuumwa umwa etc.
   
 6. Lisa

  Lisa JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 1,568
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Burn si Imani za kienyeji hilo swala ni kweli kabisa kama baba au mama anatoka nje ya ndoa, halafu unamshika mtoto wakati hujawa safi ni lazima mtoto awe Dhaifu. na si hilo tu hata kama ni baba na mama wamekula SAKALAMENT TAKATIFU. halafu wakamshika mtoto bila ya kuwa safi ni lazima mtoto awe dhaifu na anakuwa na afya mbaya sana.

  SO THAT zingatia kuwa msafi ndipo umshika MTOTO kuepusha ukuaji/Afya mbaya kwa MTOTO.
   
 7. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimefuatilia vizuri mjadala wote
  ni hivi:

  hakuna kitu hapa duniani kinachofanana na hicho mnachoita kubemenda.

  kuna watu wawili wenye watototo wenye afya nzuri na ambao niliwashauri (kila mmoja kwa wakati wake) "kuwarudia" wake zao mara tu anapokuwa tayari kimwili na kiakili baada ya kujifungua, ni takribani siku 100 hivi (ingawa si kanuni). nilishauri hivi kwani ilikuwa ndio njia pekee kumaliza tatizo la mmoja wa watu alilokuwa nalo na mkewe, wale, na kweli tatizo liliisha na mtoto hakuathirika kiafya!

  watoto wanahitaji chakula bora chenye viini-lishe vyote vinavyohitajika ili kukua vizuri na hata ukimnyoyesha sijui baada ya kulala na nani haitasumbua kama hakipata viini vya kumletea maradhi mfano ya kuhara.

  hakuna madhara yoyote yanayoweza kumpata mtoto kupitia maziwa ya mama endapo mama na baba au hata mama au baba atatembea nje ya ndoa. yote hayo ni imani potofu.

  tuzingatie chakula bora kwa watoto na tusinyimane tendo la ngono ndani ya ndoa kwa sababu kama hizi,

  ni upuuzi mtupu
   
 8. K

  Kilambi Member

  #8
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona wasiwasi wa wengi hapa ni nje ya...

  okkeeey!! hivi kwenye hii imani potofu itakuwaje kama ba/ma kajivinjari nje then akaoga huko huko!? kanuni za imani potofu zinasemaje hapa, au mpake aoge nyumbani?!
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  nijuavyo mimi kumbemenda mtoto maana yake ni kwamba wakatii mama amejifungua, na ndani ya mwezi mmoja au miwili mpaka mitatu akawa ameanza tena kufanya mapenzi, na mara akabeba mimba tena wakati ana mtoto mwingine tena bado mchanga ananyonyesha basi mtoto huyu anakuwa amebemendwa, maana yake ni kwamba mama hatamjali sana huyu mchanga ila aitaanza kulea mimba yake.hivyo katoto kachanga kanakuwa na afya mbovu kupita maelezo, kanaweza kakaanza kutembea kakiwa na miaka mitatu.

  umeelewa?
   
 10. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  narudia ni imani potofu,

  hayo "aliyooga" hata wakimnywesha mtoto kama hayana viini vya maradhi na mtoto akapata afya chakula kilichokamilika kwa viini-lishe, atakuwa kwa afya timamu bila wasiwasi!

  jamani na elimu yote hii iliyotuzunguka kuna watu JF wanaamini upuuzi huu!
  tusiwe wavivu, tuamke, tuelimike tujikomboe
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hili swala limeshawahi kujadiliwa sana siyo hapa tu bali kwenye forums mbalimbali..

  Cha kujiuliza kwanini haya mambo ya kubemenda utayasikia kwa watu fulani tu wa social status fulaini mfano uswazi zaidi( kunradhi ni katika kujaribu kuweka point ieleweke na siyo kudharau mtu yeyote)

  Kama walivyosema wengine waliotangulia.... kubemenda hakuna tofauti na kusema utapia mlo/ unyafuzi..ambapo afya ya mtoto hudhoofu kutokana na maradhi au lishe duni.Udhofu huu kama utatokana na magonjwa ya kuharisha mara nyingi tunajua kuharisha kunasababishwa na nini- kula uchafu na maradhi mengine.Afya ikitetereka maendeleo ya mtoto lazima yatarudi nyuma.

  Ukiangalia haya mambo ya kubemenda yanahusishwa sana na hii imani potofu kwa sababu ya mazingira ya wahusika wanamoishi - utaona kuna wanawake hawajali kuangalia watoto - wako kutwa wanazurura hata kama siyo kufanya kitu kibaya.

  Kumbe wangetulia nakutunza watoto wao, afya zisingetetereka namna hii.

  Imani hii pia imejitokeza kama social control mechanism kuwazuia watu wenye watoto wadogo kutokujihusisha na mambo ya zinaa maana huweza kusababisha mimba nyingine na pia magonjwa na hivyo kuingilia utaratibu wa kulea mtoto.

  Labda tujiulize ni maeneo gani zaidi utayasikia yakizungumzia kubemenda na kwa sababu gani.
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Vera, hebu kwanza cheki hiyo senks niliyokuchapa kwa maelezo mazuri sana! Kubemenda na miiko mingine iko zaidi uswazi na hakuna mtoto wa Masaki, Mikocheni au Oysterbay ambaye amebendwa ingawa huko nako ngono zinatembea kama kawa!

  Kwa wazee wetu wa enzi hizo, hii ilikuwa ni control mechanism kupunguza ngono za hovyo hovyo na kumfanya mtu atumie muda wake kumlea mtoto. Ni sawa na imani kuwa ukichezea kisu au kukata kucha usiku kwa kutumia wembe baba yako atakufa! Kumbe hawataki kuhangaika na majeruhi usiku! Au ukinyonyesha mtoto baada ya tendo la ndo ataharisha! Yapo mengi sana ya namna hiyo kwenye jamii zetu. Ila baada ya kuelimika inabidi tuweze kutafuta maelezo na chanzo cha imani hizo.
   
 13. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  Naomba scientific expalianation ya kile kinachofahamika kwa kiswahili 'kubemenda mtoto'. Kwa wasio fahamu hii kitu ni pale unakuta mtoto ana miaka hata mitatu au zaidi hata kusimama au kutemebea hawezi.

  Ni suala linalohusishwa na zinaa kwa mzazi au wazazi wa mtoto huyo during his/her very early stages of growth mfano first 5 months of age. Awali nilifikiri ni myth lakini nimekutana na hizo case sehemu kadhaa.

  Ukweli na misconception yake...pia causes na treatment/management yake medically.
   
 14. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaweza ukaliweka swali lako vizuri..? sijakuelewa .. are you trying to ask kwanini baadhi ya watoto wanachelewa kutembea ..? alafu unaweza ukanijuza hiyo process ya kubemenda imekaaje..?! anafungwa kitu ama anapewa dawa ama.. etcl..?!

  shukran
   
 15. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  :shut-mouth:
  i doubt kama wewe ni mzoefu wa mambo ya watoto na kama unaishi Tanzania hii......hii kitu si ngeni ati!! yaani mtoto anaharibiwa na anakuwa hawezi kutembea unless afanyiwe utaalam. Nimejaribu kuuliza,exactly huwa anafanyiwa mtoto lakini sijapewa jibu. Kama wewe unaishi Tanzania,please jaribu kuuliza hii kitu.
   
 16. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hiyo issue ipo sana na ukiifuatilia kwa umakini unaweza kukubali kuwa ipo kisayansi zaidi. Madai kuwa endapo mzazi au wazazi wakati mtoto bado mchanga wakajihusisha na ngono nje ya mahusiano yao basi huyo mtoto atadhurika. Dhana hii imesimama kwa mtindo huu (especially kwa kina mama) kwa kuwa wakati huo kondom hazikuwa kitu cha kawaida kwahiyo ngono ilikuwa live. Kinachotokea ni kuwa mama atapokea mbegu za mwanamme ofcourse ni proteins ambazo kisayansi tunaamini kuwa baadhi yake huingi kwenye mzunguko wa damu na wakati atakapo mnyonyesha mtoto, yule mtoto atapata proteins za yule njemba aliyefanya ngono na mama yake. Matokeo yake yule mtoto atadhurika na hivyo kuishia kuwa legelege na kuchukua muda mtefu kuweza kutembea. Angalizo: Huenda ikawa ni njia moja wapo ya kuzui ngono nzembe wakati wa kulea watoto na pia kupunguza hatari za kupata watoto wanaoweza kukaribiana sana
   
 17. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  true siishi tnz na sijasoma medical uni ndani ya africa but i thought this little medical knowledge ya pediatric niliyosoma nilipokuwa 3rd year might help, my curiousity ilikuwa hapo kwenye RED "utaalam gani" ?
   
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  hii issue ni ya ki-sociolojia zaidi. kitu kinachotokea mwishoni ni malnutrition! mama anapobeba ujauzito mapema wakati ana mtoto mchanga (tunaita vodafasta), anakuwa anachoka na anashindwa kumnyonyesha mtoto. matokeo yake yule mtoto mchanga anapata lishe duni na hatunzwi vizuri (uwezo unachangia pia,manake kubemenda ipo uswazi zaidi ya masaki kwenye ma-housegal 2+). same for a woman having an affair nje ya ndoa, anakuwa busy na extra-curricular anajisahau kusimamia shughuli za mtoto.

  pia ilitumika kama mbinu ya kusaidia uzazi wa mpango hapo zamani, kuwa wazazi wasikutane kimwili hadi mtoto awe mkubwa. tunajua madhara yake, watoto wa nje ya ndoa na wa ndani wanapishana mwaka.

  HITMISHO: endapo mama atapata mimba mapema baada ya kujifungua,inashauriwa aendelee kumnyonyesha mtoto hadi dr atakapomkataza. lishe ya mtoto izingatiwe kwa ukaribu na baba ashiriki kumsaidia mama. ngono salama inaruhusiwa,na usafi uzingatiwe.
   
 19. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Haya mwalimu. Asante kwa "kunielewesha" kwamba kwa vile HIV (110-140 nanometers in size ) anaambukizwa through body fluids basi hata spermatozoa (diameter:0.042mm to 0.003mm, length: 25 ┬Ám) zitajipenyeza kuingia kwenye system ya mjamzito kwa njia hiyo hiyo.

  Take my comments very positively, although they are a bit embarrassing:
  Sayansi uliyonayo kwenye suala hili ni bomu. Bahati mbaya unajaribu kuitumia hiyo "junk science" kujaribu kuelezea folk myths.

  Usikasirike kwa hili. Kubali kwamba ulikuwa hujui au uliamini sana "myths" za kubemenda. Kwa majibu sahihi msome King'asti hapo juu.

  Wako,
  Mwanafunzi mtiifu.
   
 20. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hii ni "Sociological Myth", na pengine (?) inawahusu pia wanaume kwamba mke amejifungua, ana mtoto mchanga, na mwanaume anatoka nje ya ndoa, akirudi anambeba mtoto kabla ya kwanza kwenda kuoga. ???????/
   
Loading...