singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
DHANA ya kubana matumizi iliyokuwa inapigiwa makelele muda mrefu, iliwavutia Watanzania na wananchi wengi, hususan wa Afrika Mashariki baada ya Rais John Magufuli kuitekeleza kwa vitendo.
Mtindo wake alioanza nao wa kupiga vita rushwa na kubana matumizi, ulisababisha Waafrika wengi, hususan watumiaji wa mitandao ya kijamii kuja na kile kisemacho: “What Would Magufuli Do” ambayo kimsingi ni dhana ya kubana matumizi. Siku ya kwanza kuingia ofisini Rais alipiga marufuku safari holela za kwenda nje, akapeleka pesa zilizotakiwa kutumika kwenye sherehe za uhuru kujenga barabara, akapunguza pesa zilizotakiwa kutumika kwenye sherehe za uzinduzi wa Bunge kwenda kununulia vitanda na vitu vingine.
Hatua hiyo ya Rais imeshaanza kuzaa matunda ambapo katika tukio linalokumbukwa zaidi ni pale Rais Magufuli alipokea hundi ya Sh bilioni 6 kutoka kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila, fedha ambazo ziliokolewa na Bunge baada ya kubana matumizi. Ilielezwa kwamba matumizi hayo yalibanwa katika kipindi cha miezi minne na kwamba ni kati ya kiasi cha Sh bilioni 127.3 ambazo Bunge lilitengewa mwaka 2015/16.
Akipokea hundi hiyo, Rais alisisitiza umuhimu wa taasisi mbalimbali za Serikali na umma kujenga utamaduni wa kuokoa fedha na matumizi mengine yasiyo ya lazima. Rais alieleza kufurahishwa na hatua hiyo ya Bunge ya kubana matumizi na kurudisha fedha serikalini ambazo kwa sasa zitatumika kununua madawati ili yapelekwe mashuleni.
Rais alienda mbali na kuwataka makatibu wakuu wa wizara kuiga mfano huo wa Bunge, huku akiwalaumu kuwa haijawahi kutokea Katibu Mkuu ambaye amerudisha fedha zilizobaki katika wizara yake serikalini kwa ajili ya matumizi mengine. Wapo baadhi ya watendaji serikalini ambao wameanza kutekeleza kwa vitendo dhana ya Rais John Magufuli ya kubana matumizi na mmoja wa watendaji hao ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela.
Mkuu huyo wa Mkoa hivi karibuni alifanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Ukerewe, ambapo aliagiza viongozi alioongozana nao kwenda wilayani Ukerewe kuacha magari yao jijini Mwanza na badala yake wakapanda meli ya MV Nyehunge. Baada ya kuwasili wilayani Ukerewe viongozi hao walipokelewa na viongozi wa Ukerewe kwa kutumia magari yao.
Viongozi waliongozana na Mkuu wa Mkoa kwenye ziara yake hiyo ni pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Clodwing Mtweve, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mwanza Ernest Makale, Mrakibu wa Polisi, Shedrack Kigobanya ambaye alimwakilisha Kamanda wa Polisi wa Mkoa na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zima Moto Andrew Mbate.
Wengine ni Kaimu Mshauri wa Mgambo wa Mkoa, Kepteni Abinel Ndetwa, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Uhamiaji, Moses Mtashi ambaye alimwakilisha Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Mwanza, Ofisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Atley Kuni na Katibu wa Mkuu wa Mkoa, Matia Levi. Kwa kawaida viongozi wa mkoa wa Mwanza walizoea kupitia wilayani Bunda mkoani Mara walipokuwa wakifanya ziara kwenda wilayani Ukerewe, umbali wa kilomita 250.
Mongela anasema aliamua kufanya ziara hiyo kwa kutumia usafiri wa meli na kuacha magari ili kuanza kuwajenga kisaikolojia watendaji wake utamaduni wa kubana matumizi. “Sikuona sababu ya kuzunguka kupitia Bunda hadi Kisorya kwenda kwenye ziara yangu wilayani Ukerewe na maofisa nilioongozana nao. “Usafiri wa meli ni rahisi na unabana matumizi. Nilijiuliza kwa nini kwenda Ukerewe tutumie magari ya Serikali. Kwa kutumia magari fedha nyingi zingeteketea lakini pia kutupotezea muda kuzunguka wilayani Bunda,” anasema.
Anasema anawataka watumishi wenzake wajiandae kufanya ziara hizo na yeye kwa kutumia usafiri wa boti za halmashauri ili kuendelea kuunga mkono ubanaji matumizi. Anasema katika ziara hiyo pekee kama msafara wake ungetumia magari saba, kiasi cha Sh milioni 3 zingetumika kwa ajili ya mafuta, fedha ambazo Mongela anasema zitatumika kufanya matumizi mengine muhimu ya serikali.
“Wewe umeona tulipofika Ukerewe, mimi na Katibu Tawala tulipanda gari la Mkuu wa Wilaya. Mkuu wa Usalama akapanda gari la Mkuu wa Usalama wa Wilaya, na maofisa wengine walibadilishiwa magari na hakuna aliyepata shida,” anasema na kuongeza kwamba kwa sasa anataka msafara katika ziara zake usizidi magari manne. Anataja magari hayo kuwa ni la kwake, la Katibu Tawala wa Mkoa ambaye naye atakuwa anabeba watumishi wengine, gari la Kamanda wa Polisi wa Mkoa kwa ajili ya usalama na gari moja kwa ajili ya wataalamu wake kutoka Sekretarieti ya Mkoa.
Hatua hii ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ni ya kupongezwa na kuigwa na watendaji wengine wa sekta ya umma na hata binafsi. Endapo watendaji hawatajenga tabia ya kuokoa fedha kidogo walizo nazo kwa kujitenga na matumizi yasiyo ya lazima ni dhahiri dhana hii itakuwa ya mtu mmoja na hivyo juhudi anazofanya Rais Magufuli katika kubana matumizi hazitakuwa na tija kubwa.