Dhana ya elimu kwa mujibu wa wasomi na wanasiasa wetu Tanzania

Fredwash

JF-Expert Member
Oct 27, 2009
1,032
1,372
Watanzania wengi hasa hawa wanasiasa na wasomi wetu ni watu wa ajabu sana.. hivi ni nani aliewaambia ukiwa na phd ama degree basi ni lazima kila unachokifanya kiwe kwenye mstari automaticaly

wamesahahu kuwa elimu haina uhusiano na mtu kuwa na moral authority.. bali elimu ni nyenzo tu inamsaidia mtu katika kunyambulisha mambo na decion making.

Lakini bila mtu kuwa na maarifa kwanza, basi hawez kuitumia hiyo nyenzo inayooitwa elimu.

bahat mbaya hili jambo halimo vichwan mwa wanasiasa na wasomi wetu.. maana yake pia wamekosa MAARIFA.

mfano:

Watu wawili tofauti wenye elimu na uzoefu sawa watapishana kiutendaj ikiwa tu mmoja kati ya hao kakosa maarifa katika utendaji wake

Maana yake uwezo wake wa kufanya "decision making" hayongozwi na maarifa.. maarifa ndo yanakuongoza nini kifanyike wapi na kwa wakat gani.

Baada ya maarifa kukuongoza ndo unatumia nyenzo zako katika utekelezaji.. ikiwemo ujuzi na elimu yako uliopata .. hapa namaanisha kuanzia elimu ya darasan hadi elimu ya nje ya darasa kwa lugha rahis elimu ya mtaani.

Ambayo kujifunza kwake ni kutokana na kuona kusikia ama kukosea kwako mara kwa mara au mara ya kwanza ulipokuwa unafanya kitu fulani mwishowe utakuwa bora kwenye hicho kitu

Au unaweza ukawapa 100m watu waili, mwenye elimu na hana maarifa na asiye na elimu ila ana maarifa. mwisho wa siku mwenye maarifa atazalisha maradufu kuliko mwenye elimu na pengine akamtumia huyo huyo mwenye elimu

Elimu ya darasan ina umuhimu sana sababu ndio nyenzo itakayokufanya ufike malengo kwa wepes ama kwa mda mfupi na itakupunguzia zile trial and errors sababu utakuwa unajua FACT.. ila bila maarifa ni bure.

Wasichokijua watu ni kuwa wengi waliofanikiwa kwenye maisha waliosoma na wasiosoma ni kuwa wana karama ya maarifa ambayo walitumia kupata mafanikio tena wengine kwa kutumia wasomi wenye elimu zao..

Na wengine kwa kutumia makosa ya wengine au tunaita wajanja wa kusoma mazingira. kwa maana ya watumia fursa..

Wanasema elimu haina mwisho ila ukomo wake utategema na maarifa uliyonayo. Maarifa hayana limit ni karma ambayo kila mmoja anayo ila tuna tofautiana katika kuitumia na kuiboresha

Kuna watu hawakusoma na waliweza ku invet vitu kurahisisha maisha yao. maarifa yanazalisha skills

Ukifatilia utaona kuwa walichukua mda kuweza kutimiza hizo invention zao na zilijaa trial and erros nying sababu hawakujua in advance zile do's and dont's za walichokuwa wanafanya

Ili uwe bora sana kwenye kila unalolifanya basi wekeza kwenye elimu ila ili ufanikiwe kwenye kila unalolifanya basi ishi kwenye maarifa.

Mifano hainya maarifa

Mzee Mengi

Msomi alieacha kazi akaenda kuanzisha biashara zake zikastawi hadi leo hayupo na bado zipo

Mzee Bakhera
Tunaambiwa hajasoma ila ndo siku haitapita hujatumia bidhaa yake

Hata hao wanasiasa waliofanikiwa na hawajasoma ni sababu ya maarifa. aidha wametumia vibaya kwa kutapeli ama kwa njia sahihi hilo haijalishi. ila jambo moja ni kuwa ukifatilia utaona mafanikio yao yamechukua mda sababu hawana elimu

Vitabu vya dini vinasema WATU WANGU WANAPOTEA KWA KUKOSA MAARIFA.. na wala sio elimu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom