Dhana ya CCM washamba na masalia, kamwe hatutapiga hatua.

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
CCM Masalia.
Kilichobaki kwenye CCM ni wale masalia wa upinzani ambao kwenda kwao CCM ni kutaka kupata maslahi tu. Hakuna kipya ndani ya CCM ile ile ambayo miaka yote wametawala wao na uhalisia uliopo kwenye jamii ni kivuli chao halafu utegemee mabadiliko.

Hawa ndugu zetu walikosa maslahi kwenye vyama vyao na kuamua kungatuka wakidhani wataweza kuleta mabadiliko huko CCM. CCM ni mfumo tena mkongwe hauwezi kubadilishwa kwa masalia. Mfumo huu umetengenezwa katika idara zote. Nadhani tumeona tatizo la rushwa na ufisadi lilivyo gumu kuondoka kwa sababu limezama kwenye mfumo. Hata kukosa uzalendo mfano wa rasilimali na uwekaji wa mikataba mibovu ni zao la CCM kongwe. Utawezaje kuleta mabadiliko kwa kutumia hawa masalia ? Never.

CCM Washamba.
Hawa ni malimbukeni wa utawala na wapenda sifa. Katika awamu hii kundi hili ndilo limechukuwa nafasi sana. Limbukeni atavunja sheria ili asifiwe, ataamuwa na kuvunjia staha wengine bila taratibu, atahonga ili asifiwe na atafanya kiburi sehemu ambayo haina ulazima. Kuwepo kwa asilimia kubwa ya washamba hawa wa CCM katika awamu ya tano ya uongozi wa nchi yetu kumekuwa janga kubwa. Desturi na hulka za ustaarabu wa watanzania unayoyoma kwa kasi na kupandikizwa fikra za ubabe na uvunjifu wa sheria bila kuchukuliwa hatua kwenye tabaka la watawala. Hii ni hatari ya washamba kwa nchi hii.

Mwisho
Katika hali zote mbili tusitarajie kupiga hatua yoyote mbele. Ilimradi CCM wastaarabu na wazalendo wako pembeni kwenye awamu hii, tusitarajie umoja wa kitaifa wala maridhiano, tutarajie mifarakano na chuki tu. Tusitarajie maendeleo ya kweli bali unafiki , ubabe na kupendeleana tu. Tusitarajie haki na wajibu lakini uzushi na misifa tu. Tusitarajie uzalendo na ujasiri lakini woga na kujipendekeza tu.

Ni maoni yangu, chini ya utawala huu wa CCM washamba na masalia hakuna hatua ya maana itakayopigwa hapa Tanzania.

Kishada.
 
Watakuja kutwambia tupambane na hali zetu. Huu msamiati unatumika kupoza stress za watawala.
 
Umelisahau kundi la CCM Waswahili, hawa ndio wanaowaita wenzao wanaokuja na gari moshi kuwa ni washamba!!
 
kila kitu shaghala bhaghara ukiona think tank wa chama ni bashite gambo na kibajaji mnyeti unategemea nini hatari
 
CCM Washamba.
Hawa ni malimbukeni wa utawala na wapenda sifa. Katika awamu hii kundi hili ndilo limechukuwa nafasi sana. Limbukeni atavunja sheria ili asifiwe, ataamuwa na kuvunjia staha wengine bila taratibu, atahonga ili asifiwe na atafanya kiburi sehemu ambayo haina ulazima. Kuwepo kwa asilimia kubwa ya washamba hawa wa CCM katika awamu ya tano ya uongozi wa nchi yetu kumekuwa janga kubwa. Desturi na hulka za ustaarabu wa watanzania unayoyoma kwa kasi na kupandikizwa fikra za ubabe na uvunjifu wa sheria bila kuchukuliwa hatua kwenye tabaka la watawala. Hii ni hatari ya washamba kwa nchi hii.
Hebu nitajie mifano 10 ya CCM Wajanja ambao kwa mtazamo wako unahisi ndio wenye haki ya kuwa viongozi
 
Watu wote wana haki ya kuwa viongozi. Ilimradi wawe na sifa za uongozi. Mimi sijazowea kutaja majina ya watu hapa JF.
 
Ushamba wakkati mwengine ni mzuri. Kwa mfano kuogopa kukatiza barabara kwa kujiamini kama watu wa mjini kwa kuogopa kugongwa gari
 
Unakuta kiongozi wa serikali anaamini katika kutoa lugha kali kuwa ndio zinajenga na kuogopwa kumbe ni ushamba tu.

Hata staha za maneno ni ustaarabu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom