Dhana ya CCM ina wenyewe imetimia tarehe 08.12.2022 kupitia kwa Rais Samia

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,614
3,903
Ni aibu kwa taifa na kwa Serikali Rais kutoa maneno ya kijembe hadharani ya kusema kwamba anayekijua chama hawezi kuwa na Nongwanongwa kwa kusema hadharani hii maana yake ni kwamba maovu yote kwa vile yapo nadani ya CCM yanatakiwa kufumbiwa macho kazi kubwa ni kusifia tu.

Kwa kauli ya Mzee Kikwete, Mzee Makamba na Mzee Kinana imeonesha dhahiri kwamba CCM pamoja na maovu yake hawataki kusikia inakosolewa wala mtu wao kukosolewa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kimantiki wanajua kwa sasa wao ndio wa kutoa hukumu na kufokea baadhi ya wana CCM ambao wanaweza kukosoa utendaji wa Samia

Napojiuliza kama Hayati JPM angestaafu namuona JK na Kinana wangezimwa kisiasa walio wengi hakuna ambaye angeenda kupata ushauri wa kisiasa kwani wao wanaamini katika siasa maslahi siyo kwa ajiri ya kutumikia Watanzania.

Imefikia hatua kwenye media wanasema watu wazuri hawafi maana yake ni kwamba Nyerere, Mkapa na JPM hawa watu walikuwa wabaya kwenye Taifa hili lakini kwa kuangalia kauli hii ililenga kusema kwamba JPM alikuwa mbaya ndiyo maana alikufa.

Watanzania tuwe macho na kundi hili ambalo lipo tayari kwa kila kitu watoto na jamaa zao ndiyo waongoze nchi wanavyotaka , hili kundi lisipoangaliwa litaifilisi nchi na siyo tu kufilisi nchi litafukarisha watu kwani hakuna miradi yao itakayolipa kodi zaidi ya watu masikini tu ndio wataendelea kunyonywa kwa tozo na mengineyo.
 
CCM nzima ni wafu na mashetani, kuanzia top down! Hakun aliyesema la maana , wote ni maneno ya mdundiko!
 
Back
Top Bottom