Dhana sahihi ya bodi ya wadhamini ya CUF

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Dhana sahihi ya bodi ya wadhamini - CUF (THE FACTUAL CONCEPT OF THE REGISTERED TRUSTEES AND BOARD OF TRUSTEES):

Bodi ya Wadhamini ya CUF “The Registered Trustees of The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi)” ilisajiliwa rasmi kwa Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali Mwezi May, 1993 mara baada ya Chama kupata Usajili wa kudumu. Bodi haijawahi kupoteza uhalali wake kwa kufutwa na RITA au vinginevyo. Mara ya mwisho kulipiwa RITA ni Mwezi May, 2016. Hii inaifanya Bodi ya Wadhamini kuwa ni halali na iliyo Hai. Bodi ya Wadhamani ya CUF haikuwasajiliwa kwa muda maalumu (Temporary Registration) uwepo wa Bodi ni wakudumu (Permanency), kusema bodi imekufa au si hai (Mfu) maana yake ni kusema kuwa mali za CUF hazina mwenyewe na kwamba CUF haiwezi kushtakiwa wala kushtaki? Huu ni mtazamo na tafsiri potofu ya kisheria (Misconception and erroneous interpretation of Laws) muda wa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini iliyopo sasa ulipaswa kumalizika Mwezi May, 2017. Kikao cha Baraza Kuu kilichofanyika tarehe 19/3/2017 kilifanya mabadiliko ili kukidhi haja ya matakwa ya katiba ya CUF ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2014.hii haimaanishi kuwa eti Bodi ya wadhamini iliyokuwepo awali imepoteza uhalali kwa mabadiliko ya Katiba ya CUF. Hapana, haiku hivyo. Bodi ya Wadhamini na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini kisheria ni mambo mawili tofauti.

BODI NI TAASISI, BODI SI WAJUMBE WAKE. Hata kama Bodi ya Wadhamini haitakuwa na mjumbe hata mmoja bado itakuwa hai na itakuwa na haki ya kumiliki na au kuendeleza mali, inaweza kushtaki na au kushtakiwa. Hivyo, kesi zote zinazoendelea Mahakamani ni kesi zilizofunguliwa kwa mujibu wa mamlaka ya Bodi ya Wadhamini ya CUF, mabadiliko ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya CUF hayafuti uhalali wa uwepo wa kesi Mahakamani. Mali zote za chama zipo chini ya Bodi ya Wadhamini ya CUF na usimamizi wa kila siku wa mali hizo upo chini ya Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad. Yeye ndiye kiunganishi kati ya Taasisi (CUF) na vyombo vyake ikiwemo Bodi ya Wadhamini, Jumuiya zake, Taasisi na watu mbalimbali hufanya mawasiliano na Taasisi kupitia Katibu Mkuu ambaye ndiye Muwajibikaji na Mtendaji Mkuu wa shughuli za Chama na mawasiliano yote ya Chama. ni kwa msingi huu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini anapotoa Ruzuku na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali-CAG anapotaka kufanya Ukaguzi uwasiliana na Katibu Mkuu.

Katika tafsiri na maana ya uwepo wa Bodi katika mashirika na taasisi mbalimbali juu ya Tafsiri na maana ya “PERPETUAL SUCCESSION” imeelzwa ifuatavyo katika vitabu vya sheria;

“Board of Trustees and Registered Trustees’ In company law, term

Perpetual Succession” defined very clear that is the continuation of a corporation's or other organization's existence despite the death, bankruptcy, insanity, change in membership or an exit from the business of any owner or member, or any transfer of stock, etc.

HII INA MAANA KUWA hata kama kuna wajumbe wengine wa bodi watapatwa na ugonjwa wa akili (wendawazimu) bodi inaendelea kuwa hai. Tunapenda kumuelimisha Magdalena Sakaya na wenzake wote wenye uelewa mdogo kama wake.

Nini kimefanyika hivi karibuni kuhusu Bodi ya Wadhamini?

Afisa Mtendaji Mkuu na Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Registration Insolvency and Trusteeship Agency–RITA) anawajibu wa kusimamia matakwa ya sheria za nchi na Vyama/taasisi husika kwa mujibu wa katiba zao. Amemuandikia barua Katibu Mkuu kumtaka kuboresha taarifa za Taasisi/wajumbe wa Bodi ya Wadhamini iliyopo katika ofisi yake. Katibu Mkuu amekamilisha kazi hiyo baada ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lililokutana katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika Tarehe 19/3/2017 Zanzibar, katika Agenda No.4A kilifanya uteuzi kwa mujibu wa Katiba Mpya ya CUF Toleo la mwaka 2014 Ibara ya 98(1-6), Liliwateua wafuatao kuwa wajumbe tisa (9) wa Bodi ya Wadhamini; Mhe. Abdallah Said Khatau- Kutoka Masasi, Mtwara. Mhe. Ali Mbarak Suleiman – Kutoka Unguja, Zanzibar. Mhe. Mohamed Nassor Mohamed- Kutoka Unguja, Zanzibar. Mhe. Dr. Juma Ameir Muchi- Kutoka Unguja, Zanzibar. Mhe. Mwanawetu Said Zarafi- Kutoka Kilwa, Lindi, Mhe. Brandina Obassy Mwasabwite, Kutoka Kindondoni, Dar es Salaam. Mhe. Yohana Mbelwa- Kutoka Handeni Tanga. Mhe. Mwana Masoud- Kutoka Pemba, Na Mhe. Zumba Shomari Kipanduka – Kutoka Mikumi, Morogoro. Kati ya wajumbe hawa Tisa (9) wajumbe watano(5) wamerejeshwa na Wajumbe wane(4) wamebadilishwa (wapya). CUF kupitia Katibu Mkuu, Maalim Seif imeuhisha (Update information) taarifa zake katika jalada (File) la CUF lililopo RITA. Bodi ya Wadhamini ya CUF ilishasajiliwa Rasmi tangu Mwaka 1993 baada ya kusajiliwa kwa CHAMA.

Viongozi wetu wamewasilisha RITA majina ya wajumbe wapya, wale wanaoendelea kuwa wajumbe wa Bodi, na sababu za kufanya hivyo na kuweka pamoja na taarifa zote za mikhtasari ya vikao vya Chama kwa mujibu wa Katiba ya CUF, kwa lengo la kubadilisha wajumbe wa Bodi na kuwarejesha wengine kuendelea na Bodi, mchakato huu unaitwa (RETURN OF TRUSTEES and NOTIFICATION FOR CHANGE). CUF haijasajili Bodi mpya RITA, kinachobadilishwa RITA ni Wajumbe wa Bodi na sio Bodi ya wadhamini ya CUF ambayo usajili wake upo tangu 1993, ili Bodi iwe mpya labda ingekuwa ndio tunaanza usajili rasmi au kama ingekuwa RITA imeifuta Bodi iliyokuwepo, jambo ambalo kwa yote mawili hayapo.

MBARALA MAHARAGANDE
 
Back
Top Bottom