Dhana potofu na propaganda za uvunjifu wa amani-ni dhambi kumpumbaza mtanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dhana potofu na propaganda za uvunjifu wa amani-ni dhambi kumpumbaza mtanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by luckman, Nov 23, 2011.

 1. l

  luckman JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Nimekua nikisiliza baadhi ya wanasiasa na wanaandishi wa habari wakipotosha umma na kuzusha taharuki kinyume na hali halisi ili kukidhi matakwa na haja zao, ieleweke kwamba, mambo yote yanayoendelea ndani ya nchi ni propaganda za kisiasa na janja ya walanguzi wa nchi wakitumia mgongo wa waandishi wa habari wasio na haiba ya undishi, ni dhahiri kuwa kila mtanzania ana uelewa wa mambo mengi ingawa tunazidiana kwa viwango katika kuelewa mambo,

  ni ukweli uliotukuka kuwa, tumeambiwa na kutishia sana ikiwa ni pamoja na polisi kuvunja katiba ya nchi kukataza maandamano kwa propaganda za alshabab, hizi ni siasa za maji taka ambazo lazima zikemewe kwa nguvu ya uma katika kupigania ukombozi wa kweli wa mtanzania, kumekuwepo na vitendo kwa njia isiyo sahihi katika kutumia vyombo mbalimbali kueneza habari zisizokuwa kweli hasa pale wananchi wanapodai haki na kuhoji mambo mengi yenye majibu hatarishi kwa nchi juu ya mwenendo wa viongozi na utawala wao wa kiimla!

  ni dhahiri kuwa, kwa kila nchi yoyote ambayo ishaonja utamu wa madaraka, huwa inatumia janja nyingi na wakati mwingine huwa iko tayari hata kutoa roho za watu pindi wanahisi tonge linataka kupokwa na wenye uchungu na cnhi, kizazi chetu cha sasa, kilichoshuhudia karne mbili yani 20 na 21, tumeona mengi na bado tuanshuhudia mengi, tunahoji na kuwaza mwisho tunapata majibu yenye kutia hasira, tahamaki na uchungu juu ya yale tunayoyaona, tunayoyasoma na kuyasikia, viongozi wamejitokeza sana bila woga na kudani sera mfu na propaganda za siasa kwenye mambo ya msingi na uhai wa taifa, ustawi wa taifa hauwezi kuwepo kama maslahi ya watanzania yatapuuzwa kama kinachooneka katika kipindi hiki!


  tumeona propaganda za katiba na hotuba za vijembe lenye lengo la kuudhoofisha na kuposha ukweli, lazima watanzania waelewe kuwa kosa linalotaka kufanywa na ccm ni kosa kubwa litakalotaka maelezo ya kina hapo baadae kwa kutaka kutumia kodi za wanachi kutengeza katiba feki ili ikataliwe tuingie uchaguzi na katiba ya sasa, hizi janja tushazishutukia na kamwe hatutakubali, delaying tacs zinazofanya ni siasa za kizamani na watanazania watambue kuwa, iwapo kura ya no itazidi ya ndiyo juu ya katiba mpya ni makubaliano yaliyowazi kwamba tutatumia katiba ya zamani, huu ni mtego wa kisiasa ambao ushashutukiwa na lazima tuukemee na walio nyuma yao tuwalaani na kamwe hatutaishia hapa!
  Mwisho nitoe rai kwa wananchi tujitahidi kuelimisha umma, tusimame na kujitokeza kupinga kwa nguvu kubwa juu ya uonevu wa makusudi unaofanya na chama ikiwa ni pamoja na kutumia rasilimali vibaya!
   
 2. N

  NIPENDEMIMI Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  well said brother, umeongea ukweli mtupu! mwisho upo na ole wao, no stone will be left unturned!
   
 3. babad

  babad Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SURE naungana na wewe katika yote uliyosema na inabidi kweli tuelimishane kwani Maandamano haimaanishi ni fujo au kuhatarisha amani ya nchi.Hata watu wasipoandamana wakabakia kulalamika ina maanisha hakuna amani zaidi ya utulivu wa uoga.Ni wakati wa watanzania kubadillika ili tuwe na amani ya ukweli si ya unafiki au uoga
   
 4. e

  emalau JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Nafurahi sana kupata mtu aliyetoa na maoni yanayofanana na ya kwangu, kinachonikera zaidi ni pale watu wanapojifanya kuubiri kuhusu amani wakati hawatoi core reason ya kwa nini baadhi ya nchi zilikosa amani. mfano ni jana wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari waliishia kutoa upupu juu ya amani kuvunjika bila kutoa sababu zenye kusababisha kuvunjika amani. Sababu kuu ya kuvunjika amani katika nchi yoyote ni kukosa HAKI, ili neno lina herufi nne tu lakini maana yake ni pana sana.

  CCM wanatumia umbumbumbu wa watanzania kutopata elimu ya development studies kuwapumbaza watanzania. Waliopata nafasi ya kusoma somo hilo historia inatufundisha kwamba ili maendeleo yaje lazima conflict ziwepo, na hapa conflict si lazima iwe ya kupigana ingawa hilo linaweza likawa mojawapo kama uburuzaji utatokea. maana halisi ya awali ya conflict ni mgonagano wa mawazo. Katika hili kundi moja huwa halitaki mabadiliko ili liendelee kufaidika na udhaifu uliopo na kundi jingine likitaka kuweka mambo sawa. Kwa hiyo yanapotokea makundi yakitaka kuweka mambo sawa usishangae CCM na vikaragosi vyake kama kakundi kanakojiita "vijana wapenda amani" watakuja na propaganda ili kuwanyamazisha.

  Nawaambia kabisa watanzania wenzangu bila kuuma maneno kwamba CCM wakiendelea na mtindo wao wa uburuzaji kama uliotokea juzi bungeni nchi yetu lazima itaenda katika hatua ya pili ya conflict amabayo ni mapigano, na hivyo ndo historia inavyosema !!!!!
   
 5. l

  luckman JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Lazima tushirikiane kwa hali na mali, tulipofikia hali ni mbaya, kwa mtanzania wa kawaida siongopi, anaweza akawa haelewi ni nini kinachoendelea hapa nchini lakini mambo ni mabaya sana tena sana!kuna baadhi ya vishria vingi sana kuonesha uhalali wa ibaya ninaoungelea na kwa juu juu tu ebu fikiria kwa sasa chakula kwa ujumla tunanunua shilingi ngapi?thamani ya pesa ikowapi?tuna wahujum uchumi wangapi na kesi ziko wazi ila viongozi husika nikimaanisha dpp, igp, dci,rais mwenyewe, maadili kwenye vyombo vya uma vinavyoendeshwa kwa kodi za wananchi?nenda tra uone kazi, nenda jeshi la polisi hadi uhonge,

  nenda hospitali uone kasheshe, nenda wilayani huko chini uone vurugu kila mtu ni rais kwenye kitengo chake, yani hakuna kinachoeleweka hapa mjini, angalia elimu, angalia viwanda na mfumo mzima wa uwekezaji, angali ukwepaji mkubwa wa kulipa kodi, angalia tenda zinavyogawiwa kwa sura na undugu, angalia utendaji wa serikali, angalia rais anavyoteua watu bila kufuata vigezo vya kitaaluma bali namjuaje yule, hatuwezi kufika na sema hatutafika, haya ni baadhi tu.
   
Loading...