Dhana nzima ya neno Uzalendo

Gpaghy

Member
Sep 25, 2021
47
138
Habari wakuu !!!leo nimetafakari sana dhana nzima ya uzalendo! Hizi ndo Tabia za mtu mzalendo
1: Ni mwaminifu na mwadilifu kwenye kazi yake na majukumu yake

Mithali 14:5
Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.
2: Ni kiongozi ambaye hana upendeleo kwa anaowaongoza

Mithali 29:26
Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa BWANA

3: Ni kiongozi ambaye anapotawala au kuongoza anaowaongoza hufurahi

Mithali 29:2
Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua.

4: Hutenda kwa haki anapofanya maamuzi

Mithali 3:27
Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, kiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.
Nimemtumia Suleman kwenye quotation zangu, Huyu ndiye aliyekuwa mzalendo wa kweli, lakini huu uzalendo wa kisasa tunaoambiwa wakati

1; Kuna upendeleo kwenye vyama vya siasa
2: Kuna wizi, viongozi wanajilimbikizia mali na kujilipa posho za ajabu wakati mwananchi wa kawaida anaumia
3: Watu wanateswa na kulazimishwa kukiri makosa ambayo hawakufanya na hata wengi kuuliwa
4: Wongo hupindishwa kuwa ukweli.
5: Katiba walioapa kuilinda lakini wanajitungia sheria zao wenywe

Huu sio uzalendo mbali ni kinyume cha uzalendo!
 
Siasa, Dini na Uchumi ni mambo yanayotofautiana sana kimsingi.

Una point nzuri ila siasa itabaki kuwa siasa.

Uzalendo na uadilifu upo kwenye moyo wa mtu na unaweza badilika kutegemeana na hali na mazingira.

Tanzania hakuna uzalendo, tumetawaliwa na nidhamu ya uoga na siasa za kimaslahi.
 
Uzalendo kwa wengine tu huku wao wakijilipa 3M - 30M per month.

Uzalendo kwa wengine huku wao wakiwa ndani ya Ma V8.

Uzalendo kwa wengine huku wao wakivaa suti.

Uzalendo kwa wengine tu huku wao wakiishi kwenye majumba ya kifahari.

Nk.

NENO UZALENDO NI PANA SANA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom