SoC01 Dhana kwamba huwezi kufanikiwa ulipozaliwa (kukulia) na msemo, ”Naenda kutafuta Maisha” ulivyojengeka kwa wanajamii

Stories of Change - 2021 Competition

ROJA MIRO

Member
Jul 19, 2021
52
56
Hali ilivyo:-

1.Watanzania waishio nje.


Kila mwaka mamia ya wanawaake wanaenda Uarabuni kusaka maisha ambapo baadhi hupata mazingira ya kazi yenye staha na mishara mizuri. Lakini wengine hufanya kazi kwa saa nyingi zaidi na kwa malipo madogo huku wakipata manyanyaso ya kimwili na kingono.Ripoti kutoka shirika la Human Rights Watch iliyotolewa November 14,2017.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari ulimwenguni la DW,takwimu zinaonesha kuwa kati ya vijana 100 wa Kiafrika wanaokimbilia barani Ulaya, ni asilimia 10 tu wanaofaidika kiuchumi na ukimbizi huo.

2.Hali ya ndani ipoje?

-Dar Es Salaam, kumejengeka na kuwa na miundombinu nyingi hususan barabara za kupendeza pia.Shughuli nyingi zinazopatikana jijini humo inapelekea idadi kubwa ya watu kutiririka kuelekea Dar es salaam kwa lengo la kutafuta maisha hasa vijana wengi hukimbilia huko. Hapo awali ofisi nyingi za serikali zilikuwa zikifanya kazi huko kabla ya mpango mkakati wa sasa wa kuhamishia ofisi hizo mjini Dodoma.


Nini kifanyike?

-Maendeleo yafuate watu badala ya watu kufuata maendeleo.
Hii nikimaanisha kile ambacho watu wanakifuata Dar Es Salaam au hata nje ya nchi kinaweza kufanywa hata hapa kwetu kwa kutengeneza fursa mbalimbali za ajira,mfano uvui,kilimo.Hii inaweza kufanywa kutokana na eneo husika mfano mikoa ya Tanga,DarEs Salaam,Pwani na mingine tunajua wanafanya uvuvi,kwengine kama Ruvuma,Mwanza,Singida,Dodoma nk hivyo kila mkoa watu wawezeshwe na kuboreshewa shughuli zao kutokana na fursa zilizopo kama nilivyoelezea.

Mtazamo wangu wa dhana hiyo kupitia ushairi:-


1.
Katika kuunga unga,sio unga wa ugali.
Ni maisha kukuzonga,kulala na njaa hali.
Mbona sana utaringa,siku utokula wali.
Maisha hayasogei,na mbali siyatafuti


2.Waweza kutangatanga,Zambia mpaka Mali.
Na ukashindwa kujenga,hata banda la kivuli.
Ni bora ukajipanga,sije tafuta muhali.
Maisha hayasogei,na mbali siyatafuti


3.Wapo walohama Tanga,na kwenda kuishi mbali.
Tena kuuza karanga,mashati na suruali.
Bado mambo yakagonga,wakose hata nauli.
Maisha hayasogei,na mbali siyatafuti


4.
Waweza ukajipanga,na badae ukafeli.
Kama ndege ni kipanga,waenda kila mahali.
Kashindwa balbu mwanga,taweza na kibatali?
Maisha hayasogei,na mbali siyatafuti


5.Kiukweli sitopinga,hata nirukwe akili.
Kwenda mbali,kujijenga,ni jambo la heri kweli.
Ila ukiyaboronga,itakuwa mushkeli.
Maisha hayasogei,na mbali siyatafuti


6
.Masiaha waweza panga,lile ukapata hili.
Kichwa uma hadi gonga,ukaumiza akili.
Ukamaliza waganga,Pangani hadi mbarali.
Maisha hayasogei,na mbali siyatafuti.


7.
Hapa ninachokilenga,sio usichume mali.
Bali dhana kuipinga,lazima uende mbali.
Wangapi wamejijenga? Nyumbani kwao asili?
Maisha hayasogei,na mbali siyatafuti.


8.
Nawaruhusu kupinga,kwa hizi zangu kauli.
Hili wazo kulijenga,tushauri serikali
Wenye ujuzi kutunga,lete muusta kabali.
Maisha hayasogei,na mbali siyatafuti


ROJAMIRO.

rajabumrope18@gmail.com

0626496734

Shairi ni mali ya mtunzi hairuhusiwi kuiga,kukopi au kunakili bila ruhusa ya mhusika.
 
Hii dhana ni kweli ila ukitaka kufanikiwa eneo ulilotoka,toka kwanza kisha Urudi hapo utakuwa umebadilika
 
Back
Top Bottom