Dhana kuhusu kuchoma tunguli moto ni kichekesho

client

JF-Expert Member
Dec 13, 2015
661
847
Ni kichekesho kusema eti mchawi ajisalimishe na kukabidhi mikoba yake yenye matunguli ya kila aina, huyo hawezi kuwa na maisha tena! Asipouliwa na wenzake atakufa mwenyewe
Uchawi ni fani inayojitegemea yenye kanuni taratibu na masharti yake tena magumu, ndio maana si wengi wanaweza kuwa wachawi! Uchawi una mahusiano ya moja kwa moja na ulimwengu wa giza na mambo yasiyoonekana ulimwengu wa roho kuna viapo vyake huko! Tunguli na mapembe ni vibebeo tu vya nguvu isiyoonekana ni catalysts, kwahiyo mchawi wa kweli ana uwezo wa kuihamisha nguvu husika na kuacha mitunguli mitupu isiyo na nguvu yoyote kama mikasha tuu
Mchawi wa kweli hawindiki na wale wanaojifanya kutoa wachawi, mkikaribia nyumba yake msipokutana na bahari basi mtakutana na msitu au kiwanja kitupu... ..na huyo anayefanya hiyo kazi ni lazima awe amejizatiti kwa kinga za kila aina na zenye nguvu kubwa sana
Hii ni kwakuwa uchawi una wataalam na madaraja yake . kwahiyo kama daraja langu ni dogo na nikiona kuna mapambano yanakuja haraka sana hutafuta msaada kwa aliye juu yangu au aliyenifundisha kazi...lakini hapo hapo pia naweza kuwa ninamiliki silaha zangu za kinga za maangamizi kwa yeyote yule atakayejaribu kunichezea!
Tunguli halisi haiungui kwa moto wa kawaida..upo moto wa kichawi ambao ndio unaweza kufanya hiyo kazi au moto wenye nguvu ya kimungu na ni aina ya moto ambao hauunguzi kingine chochote zaidi ya kilichodhamiriwa
Wale wabebao matunguli na kuyapeleka kanisani kuombewa kisha kuchomwa moto wanakuwa tayari(hata kama ni wakweli)hawana nguvu tena na walishafukuzwa kilingeni na kupokonywa nguvu zote. Ni wachache mno wanaoamua kutoka wenyewe tena kwa kutoroka na kwenda kupata ulinzi wa Kimungu kabla wenzao hawajawastukia kwakuwa wakijua juu hufiki popote
Hizi operations nyingi vijijini za kutoa wachawi ni ujinga tu wa jamii yetu na kutoelimishwa dhana nzima ya uchawi na jinsi unavyofanya kazi
Kanda ya ziwa Kumekuwa na mauaji mengi ya kutisha ya vikongwe wakihisiwa ni wachawi....ujinga mkubwa huu!!! Tuache maskhara mchawi wa kweli hukuona na kukuwahi kabla hujamfikia
Jinsi tunavyozidi kulipuuzia suala zima la uchawi na ushirikina ndio jinsi tunavyozidi kuiumiza jamii
Wenzetu ulaya wanafundisha uchawi kama somo hii imesaidia kuepusha matatizo mengi sana...tusifungwe na nira za kiimani na kuonekana kuzungumzia uchawi na ushirikina ni jambo baya sana..tunapotoka na kukosea sana...kwakuwa hata katika hizo imani zetu zinaukubali na kuukiri uchawi kama nguvu hasi inayofanya kazi
 
Ila napenda kuwa mchawi sana...sema ndio hivyo tena...elimu hiyo adhimu sina mkuu

Thanks kwa bandiko zuri mkuu
 
Asante kwa kutupa changamoto, ngoja tuongeze utafiti zaidi na kujipanga.
 
hii thread ingeandikwa na mshana angeinogesha kwelikweli

tunakuita huku mshana utusaidie kuhusu kufafanua juu ya mada hii
 
Mbona wengine wakitolewa uchawi siku zao huwa xinahesabika, utasikia kafariki nini kilichopelekea kifo chake?
 
Ni kweli kwamba mtu anapopeleka tunguri na makorokoro yake ya uchawi vikachomwe moto, tayari nguvu zake za uchawi zimeshaisha. Ni kweli pia kwamba mikoba ya kichawi na tunguri zake ni kama 'vibebeo' ambavyo ni 'nyumba' za hizo roho za kichawi. Mchawi hataweza kusalimisha hivyo vifaa vyake kama hizo roho za kichawi zinazokaa kwenye hiyo mikoba hazijateketezwa. Hata hivyo, ni MUHIMU SANA hiyo mikoba na tunguri ziteketezwe kabisa. Hiyo mikoba isipoteketea, japo zile roho zilizokuwa zinatumia vitu hivyo hazipo tena, roho nyingine mpya za kichawi zinaweza kuja kutumia hiyo mikoba. Inatokea mara nyingi.
 
[QUOTE="client, post:

Allaah Anasema:

"Na (wakumbushe) siku atakapowakusanya wote (akawaambia): "Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu". Na marafiki wao katika wanaadamu (watagombania) waseme: "Mola wetu! Tulinufaishana sisi na wao na tumefikia muda wetu uliotuwekea". Basi (Allaah) atasema; "Moto ndio makazi yenu, mtakaa humo milele", ila apende Allaah (kuwarehemu), hakika Mola wako ndiye Mwenye hikima (na) ndiye ajuaye.”

Al-An'aam - 128
 
Ni kichekesho kusema eti mchawi ajisalimishe na kukabidhi mikoba yake yenye matunguli ya kila aina, huyo hawezi kuwa na maisha tena! Asipouliwa na wenzake atakufa mwenyewe
Uchawi ni fani inayojitegemea yenye kanuni taratibu na masharti yake tena magumu, ndio maana si wengi wanaweza kuwa wachawi! Uchawi una mahusiano ya moja kwa moja na ulimwengu wa giza na mambo yasiyoonekana ulimwengu wa roho kuna viapo vyake huko! Tunguli na mapembe ni vibebeo tu vya nguvu isiyoonekana ni catalysts, kwahiyo mchawi wa kweli ana uwezo wa kuihamisha nguvu husika na kuacha mitunguli mitupu isiyo na nguvu yoyote kama mikasha tuu
Mchawi wa kweli hawindiki na wale wanaojifanya kutoa wachawi, mkikaribia nyumba yake msipokutana na bahari basi mtakutana na msitu au kiwanja kitupu... ..na huyo anayefanya hiyo kazi ni lazima awe amejizatiti kwa kinga za kila aina na zenye nguvu kubwa sana
Hii ni kwakuwa uchawi una wataalam na madaraja yake . kwahiyo kama daraja langu ni dogo na nikiona kuna mapambano yanakuja haraka sana hutafuta msaada kwa aliye juu yangu au aliyenifundisha kazi...lakini hapo hapo pia naweza kuwa ninamiliki silaha zangu za kinga za maangamizi kwa yeyote yule atakayejaribu kunichezea!
Tunguli halisi haiungui kwa moto wa kawaida..upo moto wa kichawi ambao ndio unaweza kufanya hiyo kazi au moto wenye nguvu ya kimungu na ni aina ya moto ambao hauunguzi kingine chochote zaidi ya kilichodhamiriwa
Wale wabebao matunguli na kuyapeleka kanisani kuombewa kisha kuchomwa moto wanakuwa tayari(hata kama ni wakweli)hawana nguvu tena na walishafukuzwa kilingeni na kupokonywa nguvu zote. Ni wachache mno wanaoamua kutoka wenyewe tena kwa kutoroka na kwenda kupata ulinzi wa Kimungu kabla wenzao hawajawastukia kwakuwa wakijua juu hufiki popote
Hizi operations nyingi vijijini za kutoa wachawi ni ujinga tu wa jamii yetu na kutoelimishwa dhana nzima ya uchawi na jinsi unavyofanya kazi
Kanda ya ziwa Kumekuwa na mauaji mengi ya kutisha ya vikongwe wakihisiwa ni wachawi....ujinga mkubwa huu!!! Tuache maskhara mchawi wa kweli hukuona na kukuwahi kabla hujamfikia
Jinsi tunavyozidi kulipuuzia suala zima la uchawi na ushirikina ndio jinsi tunavyozidi kuiumiza jamii
Wenzetu ulaya wanafundisha uchawi kama somo hii imesaidia kuepusha matatizo mengi sana...tusifungwe na nira za kiimani na kuonekana kuzungumzia uchawi na ushirikina ni jambo baya sana..tunapotoka na kukosea sana...kwakuwa hata katika hizo imani zetu zinaukubali na kuukiri uchawi kama nguvu hasi inayofanya kazi
Hongera umejitahidi kufafanuwa kuwa watu wasipende kuchukuwa Sheria mikononi kuwauwa wakongwe watu wazima wenye macho mekundu eti kwa kisingizio cha imani ya uchawi. Uchawi ni elimu kama elimu zingine tu huku Ughaibunui hsawa nchini Ujerumani kuna shule ya kufundisha huo uchawi. Uchawi wa ulaya ni uchawi wa kimaendeleo uchawi wa kifrika ni uchawi wa kuumizana kudhuriana kwa hiyo kuna tofauti kubwa kati ya uchawi wa kizungu aka white magic na uchawi wa kiafrika aka Black magic asante kwa kuwafunguwa watu macho kuwa huwei kumkamata mchawi sio kai rahisi.
 
Ukifika kwa mchawi ambae ni mchawi asiye na mbwembwe huwezi kukuta uchafu kama huo. Wachawi waliitokana na mafunzo kutoka kwa ndugu au marafiki zao huwa hawana uchawi uliokomaa. Wanauchawi ambao ndo huo wa kuchoma matunguli n.k. mchawi aliyebobea huhifadhi dhana zake katk sehemu ambazo ni ngumu kuziona kama ww huna macho(kipofu-sina maana ya kipofu by real)
Kuna siku nitawaambia namna ya kuhifadhi dhana hatarishi za uchawi bila MTU yeyote kujua. Nitawaeleza ni namna gani ya kutumia fisi au ungo na namna ya kuwahifadhi .
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom